Natamani hata hospitali wangeheshimu jinsia za watu kama yanavyofanya majeshi

kigogo1ivi

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
520
250
Unakuta mgonjwa ni mwanaume haijalishi ni mzee au kijana utakuta anahudumiwa na nurse au doctor wa kike tena kuna muda huduma itatolewa hata akiwa uchi na ni hivyo hivyo na hata kwa wanawake.

Sasa naomba kueleweshwa kwani haiwezekani pakawa na utaratibu wa kutoa huduma hii kwa kufuata jinsia.

Maana kinachoendelea ni mimi naona ni unyanyasaji kwa wagonjwa na mgonjwa kwa muda huo hawezi kujitetea maana yeye anahitaji kupona bila kujali kuwa heshima ya kutunza tupu zake ndio keshaipoteza hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
53,628
2,000
Mgonjwa mpaka anapelekwa hospitali ni katika jitihada za kuokoa uhai. Unawezaje kuchagua mtu wa kuokoa uhai wako?

Kutokana na imani za dini maombi kama hayo husikilizwa lakini mgonjwa anatakiwa kufahamu ucheleweshwaji wa huduma unaweza kutokea ili kufikia matakwa yake.
 
Coolhigh

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
1,000
2,000
Unakuta mgonjwa ni mwanaume haijarishi ni mzee au kijana utakuta anaudumiwa na nurse au docter wa kike tena kuna muda huduma itatolewa hataakiwa uchi na ni hivyo hivyo na hata kwa wanawake.

Sasa naomba kueleweswa kwani haiwezekani pakawa na utaratibu wa kutoa huduma hii kwa kufuata jinsia.
Maana kinachoendelea ni mimi naona ni unyanyasaji kwa wagonjwa na mgonjwa kwa muda huo hawezi kujitetea maana yeye anaitaji kupona bila kujari kuwa heshima ya kutunza tupu zake ndio keshaipoteza hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana. Ndiyo maana fani hiyo inapaswa kufanywa kwa weledi wa hali ya juu. Pia ili mtu aweze kuingia huko, baada ya kufaulu masomo, anaapishwa na kwa kiapo hicho ni kosa kutoa siri ya ugonjwa wa mgonjwa anayemhudumia hata kwa ndugu zake bila mgonjwa kumpa ridhaa yake.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
14,661

Hapo kwenye kiapo cha kutunza siri naona haupo serious mkuu. Siku hizi ukienda hospitali taarifa zako zinafika nyumbani unaumwa nini kabla hujarudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
4,095
2,000
Nan kakuambia majeshi yanaheshimu jinsia, kuna kipindi niliomba nafas za kuingia jeshini wakat wa kupima afya wanakuangalia kama kweli ni rijali , nikamkuta Dada anakushika kende kama kawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msonjo Khan

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
585
1,000
Ulicho kisema ni kweli lakini kutokana na mfumo tulionao haukuliangalia hilo suala kwa sura basi inakuwa ngumu kuliteleza,maana hao wauguzi wengi wao ni wanawake na madaktari wengi ni wanaume.
 
Lwiva

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
6,562
2,000
Kwani wanaume tunapo tongoza tunatakiwa tutongoze wanaume wenzetu au tunatongoza wanawake
Ukweli ni kwamba wanawake wanaujua uchi wa wanaume zaidi ya wanavyo jua uchi wa mwanamke hivyo hivyo kwa wanaume tunawajua wanawake zaidi kuliko wanaume
Unakuta mgonjwa ni mwanaume haijalishi ni mzee au kijana utakuta anahudumiwa na nurse au doctor wa kike tena kuna muda huduma itatolewa hata akiwa uchi na ni hivyo hivyo na hata kwa wanawake.

Sasa naomba kueleweshwa kwani haiwezekani pakawa na utaratibu wa kutoa huduma hii kwa kufuata jinsia.

Maana kinachoendelea ni mimi naona ni unyanyasaji kwa wagonjwa na mgonjwa kwa muda huo hawezi kujitetea maana yeye anahitaji kupona bila kujali kuwa heshima ya kutunza tupu zake ndio keshaipoteza hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coolhigh

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
1,000
2,000
Hapo kwenye kiapo cha kutunza siri naona haupo serious mkuu. Siku hizi ukienda hospitali taarifa zako zinafika nyumbani unaumwa nini kabla hujarudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nilichoeleza ni matakwa ya kisheria na weledi ya wauguzi na madaktari. Kinachofanyika ni jambo ambalo mimi na wewe hatuna uwezo nalo. Sawa na uwizi ni uvunjaji wa sheria ila watu wanaibiwa kila kukicha!! Imani yangu ni kuwa ukimshitaki muuguzi au daktari kwa kutoa taarifa zako nje, atakuwa na kesi ya kujibu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom