johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,873
Unaweza ukadhani ni jambo dogo lakini kiukweli fedha nyingi ya kigeni imeokolewa kutokana na Rais Magufuli na Mawaziri wake kutosafiri nje ya Afrika ndani ya miaka mitano.
Tunakumbuka huko nyuma namna viongozi wetu walivyokuwa wakipishana angani kwenda Ulaya na America.
Tunakumbuka mikutano ya bodi ya mashirika ya umma iliyokuwa ikifanyikia Dubai ilivyoligharimu taifa.
Tunakumbuka namna wajumbe wa kamati za bunge walivyokuwa wanazurura hovyo huko duniani tena wengine wakiwaalika na wachumba zao kufaidi kodi ya walalahoi.
Awamu hii Rais Magufuli aliukataa kabisa huo unyonyaji wenye ufisadi wa kutisha ndani yake. Na badala yake viongozi wamekuwa wakisafiri kwa ruhusa maalumu bila kuongozana na misafara kama timu za mpira.
Dr. Mpango, najua umo humu. Nikuombe tu ikikupendeza lifahamishe taifa namna fedha ilivyookolewa kwa maamuzi haya.
Binafsi naamini fedha iliyookolewa inazidi gharama ya ujenzi wa ubungo flyover.
Maendeleo hayana vyama.