Natamani CCM watangaze rasmi kukataa kura za watumia gongo

Kuna maneno au pang'ang'a humu jamvini yanayotolewa dhidi ya kinywaji cha gongo.Kule kenya kinywaji hiki kinaitwa CHANG'AA na kinalipia kodi na hivyo kuliongezea pato taifa la Kenya.SERIKALI YOYOTE ISIYO NA UWEZO WA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO NA UDHIBITI WA BIASHARA HATARISHI KWA JAMII ITAENDESHWA KWA SHURTI.Hivyo kutokana na maneno au pang'ang'a za maccm nadhani ni vema ccm itamke rasmi kuzikata kura za watumia GONGO NCHINI kama kweli wana ubavu.TATIZO LA CCM NI UNAFIKI KWANI WAPO VIONGOZI,WANACHAMA NA WAPENZI WA CCM WANAOTUMIA CHANG'A.SASA INAKUWAJE LEO MACCM MUIITE CHADEMA CHAMA CHA GONGO?DR SLAA MZEE WA GONGO?ENYI MACCM TAMBUENI KUWA CHADEMA TUNATAMBUA HAKI YA KILA KUNDI KATIKA JAMII,KILA KUNDI LINA HAKI YA KUTENGENEZEWA MAZINGIRA STAHIKI YA KUISHI.KIWANGO CHA GONGO CHA SASA HAKINA VIWANGO,DOLA CHINI YA CHADEMA ITAWASAIDIA WAANDAAJI WA GONGO ILI WAFANYE BIASHARA YA UHAKIKA PAMOJA NA WAO KULIPA KODI kama wenzao wa Kenya.TAIFA HILI NI LETU SOTE,NA ANAE KUDHARAU LEO SIKU MOJA ATAKUSALIMIA KWA HESHIMA.

CCM inaendesha nchi kwa shuruti-ilipiga marufuku usafiri wa bodaboda na Noah lakini imelegezwa na nguvu ya umma,ilikamata watu kwa uzembe na uzururaji leo hawathubutu,michango ya ovyo imekataliwa na kodi ya kichwa walilazimishwa kuondoa,hata gongo wataruhusu kabla ya 2015 kwa kulazimishwa na matakwa ya wengi. Wakati Slaa anaangalia maslahi ya umma wao wamejifunika blanketi la uhafidhina na mning'inio wa ukoloni mamboleo. Hebu wapokee changamoto hii na kuilaani gongo hadharani kwa msimamo wa chama chao-kuiponda mitandaoni ni uoga usiofanana na chama kinachotawala nchi. Hayo ya bangi na uasherati waidhinishe wao CDM imeelezea gongo. Kuna mifano lukuki ya namna ccm ilivyolazimika kutekeleza agenda za upinzani hususan CDM. Kuongoza nchi kwa mtindo wa zimamotohakuwezi kuwa endelevu, ni wakati sasa kwa wenye mawazo mbadala kutekeleza agenda zao kwa ridhaa ya wananchi. PEOPLE'S......
 
haya mambo yamefafanuliwa kwa upana sana humu , lakini vijana wa buku 7 fc wanapotosha sana .
 
Wanywa gongo hulipa ushuru kwa polisi! Kijijini kwetu kuna mama mmoja muuza gongo aligombana na mkuu wa kituo cha polisi baada ya polisi kuwakamata wateja wake!. Nao wanywaji walimwambia mama muuza kuwa kama hatawalipa polisi tozo lao wangehamia kwa wauzaji wengine wanaolipia biashara yao ya kuuza gongo
 
Ni kweli gongo yaweza kuruhusiwa na kodi ikachukuliwa maana sioni tofauti kati ya gongo na chibuku utofauti ni TBS tu basi. Na hukohuko kwenye gongo ndo askari wa maccm wanaenda kuchukua rushwa na kuwaacha wauza gongo waendelee japo kwa siri. Bangi hiyo ni noma kabisa hata akisikika kiongozi yeyote anasema iruhusiwe natamani apigwe chini hapohapo vinginevyo unakuwa na taifa la mateja.
 
Hata mimi siungi mkono gongo kuhalalishwa pamoja na kwamba ni kamanda machachari nyanda za juu kusuni.

Hayo ni mawazo ya Dk Slaa, sidhani kama ni msimamo wa chama.;

Kamanda naomba uelekeze mawazo yako kwenye mada,je ungependa maccm watamke rasmi kukataa kura za watumia gongo au la!
 
mmmmmmh,,, sasa inafiki kipindi mwanasiasa hata aongee nini watu watajenga hoja ionekane point,, huo ni mtizamo wake kwani ni juzi tu uruguay wameruhusu GANJA. inaonekana ni jinsi gani mmekuwa watumwa wa wanasiasa.
sisi wacocaine tutasema pia ikisimamiwa vizuri italiingizia kipato taifa "au vipi?" kwa sababu hata unga ukifanyiwa package nzuri na ikauzwa wapo watumiaji watabwia,, muache unazi huyu jamaa hata akisema ataruhusu unga+ganja mtasema yes???

unga (cocaine) huwa ni mtamu na unasteam kuliko kilevi chochote, "DK SLAA ruhusu nao basi tubwie hadharani" uongeze wigo wa kukusanya kodi na tanzania iwe pepo ya dunia.
 
CHADEMA na CCM kwenye suala hili la Gongo wote mnakosea,hakuna mwenye nafuu,Lengo lenu ni kupata kura tu,wala hamwadhamini raia.
 
mmmmmmh,,, sasa inafiki kipindi mwanasiasa hata aongee nini watu watajenga hoja ionekane point,, huo ni mtizamo wake kwani ni juzi tu uruguay wameruhusu GANJA. inaonekana ni jinsi gani mmekuwa watumwa wa wanasiasa.
sisi wacocaine tutasema pia ikisimamiwa vizuri italiingizia kipato taifa "au vipi?" kwa sababu hata unga ukifanyiwa package nzuri na ikauzwa wapo watumiaji watabwia,, muache unazi huyu jamaa hata akisema ataruhusu unga+ganja mtasema yes???

unga (cocaine) huwa ni mtamu na unasteam kuliko kilevi chochote, "DK SLAA ruhusu nao basi tubwie hadharani" uongeze wigo wa kukusanya kodi na tanzania iwe pepo ya dunia.

Stick to the issue,then tutaomba viongozi wa CHADEMA kama watakataa kura za mateja.
 
siyo ccm tu. yaani watanzania wenye hakili timamu hawaitaki kabisa gongo.kwahiyo mimi napenda niisemee ccm kuwa haitaji kura za munywa gongo au muuza gongo. ni kwasababu huwa anaenda kupinga kura hajitambui ina maana kura yamunywa gongo ni sawa na ya mtu ambaye hana hakili yaani kichaa. kwamaana hiyo kumutengemea mtu ambaye hajitambui akupatie kiongonzi aliye bora hiyo ni dodo ya muchana. kwanza utakuwa haujamutendea haki.mtu amepakia mzingo wote huo halafu unampa jukumu lakwenda kukutafutia mfumbuzi wa matatizo yako halafu yeye aendelee kulala ovyo huku akijikojolea nakujinyea hapo utakuwa umemumpunja kipita kiwango.ccm haitaki hizo kura za wehu. nanyie chadema na sillaa wenu kwakweli sasa hivyi mumefikia kwenye hali mbaya.kwasababu sasa hivi ulokuwa unaonekana niukweli kwenu kuusemea umeisha kabisa sasa mumeaza kuujaribu uhalamu kuuhalalisha. hiyo dhalau kubwa nanitusi. kwa watanzania kuwaona kuwa hawawezi kujua kuwa mumewakejeli.
 
Back
Top Bottom