Natamani CCM ingetoweka kabisa ktk fikra za watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani CCM ingetoweka kabisa ktk fikra za watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SOKON 1, Apr 20, 2011.

 1. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Fedha ndiyo kigezo kikuu ktk uongozi kauli hii alitamka Wasira ndio maana ni vigumu kuwajali wanyonge.
  Pindi nisikiapo ccm natamani ningekuwa kiziwi ama kipofu ili nisikutane na hili neno CCM kwani wapo tayari kuhujumu uchumi kwa hela za wanyonge wanaokusanya kodi zao kwa maslai yao.
  Kitu kilichonifanya hadi niandike hii thread ni pindi nilipokuwa naona PT ZA POLISI zikija Udom na kuwachukua wanafunzi na kuwafukuzisha chuo kwa amri ya JK na kila mda wa usiku unapofika wanaUDOM macho wazi kama bundi wakisikilizia ni yupi anayefuata kipindi wakidai haki yao fedha kutoka bodi ya mikopo ila shukrani kwa Tundu Lisu kwa kusimamia kesi yao mahakamani kuwatetea na kuwarudisha chuo baada ya miaka miwili tangu wafukuzwe.
  Mda huu wanaUDOM wanajiandaa na uchaguzi wa chuo ila ccm kwa kuona Udom sio tegemeo lao tena wameamua kuwekeza fedha nyingi ili zile nafasi muhimu za chuo za uongozi waweze kuzichukua ili kuzuia harakati zozote zitakazo tokea chuo kwani mda huu wanapata wakati mgumu pindi wasimamapo na kujulikana ni wana ccm.

  My take:
  Fedha sio kila kitu kwani kuna mda utafika watu watasimamia haki kwani ni vigumu kuwapa wote fedha ili wakufuate ndicho kilichopo Udom kwani wapenda haki wamejitolea kupambana na magamba kwa nguvu yoyote kwa kuhakikisha wanaelimisha na kusimamia haki bila kuangalia cash zao. Kwani hali ni tete kila upande unajaribu kutumia nguvu yoyote ili iweze kushinda kati ya ccm na cdm ila hawa chama cha magamba sumu ni ile ile.

  Wao wanapesa sisi tuna Mungu

  Nawasilisha
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM isipotoweka yenyewe itatoweka tu kwa nguvu ya umma. Huko Misri chama tawala kwa miaka 40 cha NDP juzi kilivunjwa rasmi na watawala wapya -- na hiyo ilitokana na nguvu ya umma pale Tahrir square. CCM nini bwana? Just a matter of time!
   
 3. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Huyasemayo ni kweli ila kwa mara ya kwanza kusikia ccm watawekeza pesa uku Udom ili kuwapa vijana wao uongozi wa chuo nilipuuzia ila kwa hii ya mara ya pili tena watu wakitoka ktk vikao vyao ikanibidi niandike hii thread ili wana JF watoe mtazamo wao jinsi ccm wanavyotumia ela kuwa sifa ya uongozi bila kumjali anayetoka jasho la damu mnyonge anapofanya kazi kwa bidii pindi alipapo kodi ila marejeo ni ufisadi.
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Niiwahi kusema sehemu, CCM kwa maana ya chama cha mapinduzi na kwa huku bara enzi hizo kikifahamika kama TANU.
  Ni chama ambacho kidhamira na malengo yake kwa sasa ni kama kimeshamaliza kazi yake, kwamba kazi yake kuu ilikuwa "ukombozi" toka kwenye makucha ya mkoloni sana sana baada ya hapo Mwalimu (pamoja na mapungufu yake) alijaribu na kwakiasi fulani alifanikiwa kujenga misingi ya taifa hili kwamba angalau alikuwa anamaono makuu juu ya taifa hili, kwamba alifikiria (japo kufikiria) kwamba siku moja nchii ije kuwa "TAIFA KUBWA" duniani...
  Tuje leo sasa, kazi zote hizo kwa ccm hawana tena ukizingatia Mwalimu kafa na ndoto zake hata siku za mwisho wa uhai wake alikuwa ni mlalamikaji (japo ye alikuwa na influence) tu kama sisi.
  Saiv, mkoloni hayupo..... hamna mwenye ndoto kubwa (japo kwa ajili ya watoto wetu tu), so hamna wa kusimamia kitu tena.
  CCM ni genge la wanyang'anyi, wanaojipongeza kwa "kazi"
  Hii nchi haitakuja kuendelea chini ya ccm, nayasema haya chini ya ushahidi wa miaka 50 ya uhuru na hali ya umasikini wa taifa na watu wake!
  So, kwenye mjadala wa kuelekea Tanzania mpya, CCM ni lazima itoke kwenye fikra za watanzania.
   
 5. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kama ilivyoonekana dalili toka mwanzo kupunguza nguvu za wanafunzi pindi wanapodai haki zao kwa kuweka viongozi wanaowataka wao ili wasipitishe jambo lolote.
  Hawa ndio viongozi waliopitishwa ktk kitivo cha sayansi na jamii na wengine kuchinjiwa baharini kwa kutokuwa na vigezo wanavyotaka wao.

  1. Mwesiga
  Huyu ndiye aliyetoa tamko la wabunge wa chadema waliotoka nje wakati wa hutuba ya rais waombe msamaha

  2. Abubakari
  Huyu ni ndugu yake Bashe yule aliyeambiwa sio raia wa Tanzania na pia ni mfanyakazi wa Rostam Azizi na kunahabari amempa hela za kutosha kuhakikisha anashinda

  3. Deborah
  Huyu amekuwa akionekana ktk mikutano ya ccm na pia alishiriki ktk kampeni za JK.

  Wasiwasi wangu ni kupata viongozi vibaraka wa ccm kama ilivyokuwa kwa raisi wa kwanza wa chuo pindi alipogoma kuungana na vyuo vyote Tz ktk madai ya mikopo ya elimu ya juu.
   
 6. x

  xman Senior Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka usiwe na hofu muda sio mrefu hiki chama cha zamani kitapotea, WHY? kwasababu kimecha dhumuni kuu ambalo ni kuwa tetea wafanyakazi na wakulima, ambapo ndio maana kilianzishwa. Chama cha K.A.N.U kenya, hakikuwa kinategemea kama kingedondoka, lakini ndio yaliyotokea.
   
Loading...