Natamani binti zangu waje wawatazame Ester Matiko, Ester Bulaya na Halima Mdee kama 'role model' wao

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Hua napenda kuona wanawake waliofanikiwa wakipambana sio kwa kutumia maumbile yao au miili yao bali akili zao.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu ambapo wanawake wengi hawataki kujishughulisha wala kushughulisha akili zao bali hutaka kushughjlisha miili yao ili wafanikiwe, hili sio kwa hao niliowataja hapo juu.

Hao wanawake wameonyesha kwa vitendo kua kila kitu kinawezekana, hawaogopi na wala hawateteleki. Bulaya alimpiga chini waziri na kiongozi wa muda mrefu toka Nyerere, ndugu Wasira tena akiwa waziri, hakujali uwaziri wa Wasira wala mwili wake mkubwa, yeye alienda kupambana nae na akamshinda mchana kweupe jua limewaka, wasira akakimbilia mahakamani bado E. Bulaya akambwaga.

Sipendi kuona wanawake wanategemea kubebwa, tena wengine wana hadi phd kama caster seemenya wa Mbeya, walikuwepo kina Migiro nk.

Ester Matiko alikua mwalimu UDSM, hakujali kua yeye ni mwanamke na wala hakujali ajira ya kudumu(kama wanavyoita waajiriwa wa serikali-security) bado akaamua kuachana na security akaenda kupambana. Halima mdee alimpiga chini msomi na mwanasiasa mkongwe nchini bwana Mbatia mchana kweupe.

Napenda nikija kupata binti ajifunze kupambana na kutegemea akili yake na sio mwili au makalio yake kufanikiwa, napemda sana courage na hao wanawake, those girls have got balls. Bila kujali mazingira magumu ya upinzani hapa Tanzania ila wanapambana, jana wanapelekwa gerezani ila bado unaona mioyo yao haijakata tamaa. Wabarikiwe sana wanaume wa hawa wanawake.

Update ya leo Tarehe 26.12.2020.
K
uanzia leo nimefuta huu ujumbe wangu dhidi ya hawa wanawake, Esta Matiko, Bulaya na Mdee.

Mwanangu bora ajifunze kutoka kwa Amba Ruti ila sio hawa wanawake.
 
Ester Matiko sawa. Lakina Ester Bulaya na Halima Mdee!! Mmmm lakini kila mtu na uamuzi wake.
 
Hushauriwi mwanao kumpa jina la mtu aliye hai, muda wowote anachange. Ona Wazazi waloita watoto zao Jaden Wiliam Smith, sasa watoto wanajisikiaje kufananishwa na kijana anayetambulisha boyfriend jukwaani.
 
Kwa kweli hao mabinti ni zaidi ya wale wanawake wa viti maalum wote 115 waliopo bungeni.

Jamani wengine tupo huku kwenye siasa tunaona! Ukiona mpinzani amepata ubunge kazi iliyofanyika sio ya kitoto.
 
wazazi nyie mnachagulia watoto hadi ma role model

kweli hizi zama za zinzilelaaaa...
 
Baba Jesca mwenyewe anatamani "KIROHO" jambo hili kama wewe, anatamani Jesca awatazamie kina Halima Mdee, Ester Matiku na Ester Bulaya kama "ROLE MODEL" wake..

"Msifuate na kumuiga nyayo za Ndalichako, mtakula hasara, fuateni nyayo za ujasiri kwa Halima Mdee & Co". (In Baba Jesca's Voice).
 
Hao watoto wako wakiwa Kama Hawa Hawataolewa kamwe, Hawa wote hawana wanaume, wanawake wanaharakaati hawawezi ndoa
 
Hushauriwi mwanao kumpa jina la mtu aliye hai, muda wowote anachange. Ona Wazazi waloita watoto zao Jaden Wiliam Smith, sasa watoto wanajisikiaje kufananishwa na kijana anayetambulisha boyfriend jukwaani.
Familia ya Will Smith inasikitisha yaani mtoto wa kiume ni shoga halafu wa kike ni msagaji😫🤐
 
Back
Top Bottom