Natakiwa kufuata taratibu zipi kwenda kujitambulisha kwa wachaga?

Naomba nizungumze kulingana na uzoefu nilioupata coz mimi nimeoa huko huko uchagani lkn kwa sasa ndoa hakuna tena na niliamua kwenda kuoa nyumbn kijijini....iko hivi mtafute mchaga mwenzao awe mshenga wako na hakikisha anajua kuongea vizuri asiwe muoga

Pili hakikisha wakati unafanya maandalizi hayo uwe tyr umeshayasoma mazingira ya hao wakwe zako ili mjue mnaingia vipi siku iyo maana wachaga kwa shughuli ndio zao

Tatu unatakiwa kufahamu wachaga kitendo cha kumuozesha mtoto wao hupenda kufanya shughuli ingawaje gharama za iyo shughuli ni zao lkn na wao kupitia iyo shughuli watataka pesa yao ya kumkuza uyo mtoto iweze kurudi kwa kiasi flani

Nne na la mwisho japo si kwa umuhimu kumbuka hapo si kwenda kutoa barua tu wanategemea unaenda kutoa na mahali kabisa sasa hapa mzee jipange coz huwa inategemea na familia yao mimi niliambiwa mahali milioni tatu cash na kama anamimba ujue kuna faini pia unatakiwa uwende na creti la bia moja pamoja na la soda moja na pia huwa wanakuwa na faini za kishamba kwa mfano mkichelewa kwa tukio faini maana yake hapo ela na kuna mafaini kutoka kwa makaka zake na faini za kumpa ujauzito kabla ya ndoa.

Nb;Wachaga wanapenda sana baada ya mahali mfunge ndoaaaaaaaaaaa kabisa hapo ndipo niliposhindwa mimi na kuamua kughairi lkn mahali nilishatoa
pole mkuu. kwanini hukufunga ndoa?
 
Nimeona mamba familia yenye maisha mazuri mahari binti ndio alipanga ya kichaga,sikumaliza milioni....shida dada zangu mnapenda kuolewa sana ila mahari wazazi wenu wanataka kunalizia shida zao mara 3m
Hapana. Nadhani sababu kubwa ni kwasababu wanajua money value. Wanajua wameinvest kiasi gani. Sidhan kama mil 3 ama 2 inamaliza matatizo kwahiyo hapa utakua unakosea kaka. Ijapokua sipendelei kuolewa kwa mahari kubwa hivyo. Lakini gharama huja kubw akutokana na mahitaji yote kwa ujumla kama mablanket etc.
 
Andaa lita 10,000 za mbege.
Kipato chako kikoje hilo swali utaulizwa linakera sana lakini ni muhimu. Wanataka assurance ya maisha ya binti yao.
 
Wewe hukutaka kufunga ndoa au ilikuwaje?

Mkuu swala la ndoa za kanisani hasa sisi wakristo ni maagano hivyo nilihitaji kukaa nae kwanza ili kujilizisha nae je itakuwaje kama hazai si nitatakiwa kuzaa nje na ikitokea hivyo uyo mtoto ni haramu
 
Kwa wale waliovuka hii stage, naomba uzoefu wenu wa namna ambavyo natakiwa kufanya ili nikajitambulishe Kwa mke wangu tarajiwa Moshi, kufupisha story ni kwamba huyu binti ni mjamzito sasa, wazazi wake wananikomalia niende wakamfahamu baba wa mtoto ambaye ni mimi.

Nimeukwepa sana huu mtego lakini nimeona tu nikaitikie wito. Naombeni mnipe mbinu,bajeti, na yanayojiri kule ili nisiwakwaze.
Anaitwa nani
 
Mbege debe kadhaa, kreti 2 au 3 za bia, soda maybe kreti 2au 3, kuwa na hela kiasi kwa ajili ya kupunguza yale ya lazima mfano blanketi la mama unaweza toa hela, mbuzi unaweza toa hela at least ukiwa na 1m utatembea parefu Sana, uchagani hamnaga mbwembwe nyingi man
bora maana sio kwa matisho aliyopewa, eti milioni 2 za mbege tu jaman?

wamuache shemeji yetu aje kujitambulisha bhana
 
Kwa wale waliovuka hii stage, naomba uzoefu wenu wa namna ambavyo natakiwa kufanya ili nikajitambulishe Kwa mke wangu tarajiwa Moshi, kufupisha story ni kwamba huyu binti ni mjamzito sasa, wazazi wake wananikomalia niende wakamfahamu baba wa mtoto ambaye ni mimi.

Nimeukwepa sana huu mtego lakini nimeona tu nikaitikie wito. Naombeni mnipe mbinu,bajeti, na yanayojiri kule ili nisiwakwaze.
Huku uchagani tunatofautiana tofautiana kidogo
inategemea ni mchaga wa wapi
Marangu, Machame, Rombo, Uru nk ila kwa urahisi tu tafuta mzee moja wa kichaga hapo mtaani kwako atakusaidia kila kitu
Wachaga wapo kila mahala tanzania hivyo huwezi kuniambia umekosa...
Angalia hata mangi hapo dukani...
 
Kwa wale waliovuka hii stage, naomba uzoefu wenu wa namna ambavyo natakiwa kufanya ili nikajitambulishe Kwa mke wangu tarajiwa Moshi, kufupisha story ni kwamba huyu binti ni mjamzito sasa, wazazi wake wananikomalia niende wakamfahamu baba wa mtoto ambaye ni mimi.

Nimeukwepa sana huu mtego lakini nimeona tu nikaitikie wito. Naombeni mnipe mbinu,bajeti, na yanayojiri kule ili nisiwakwaze.
Mrejesho
 
Yaani andaa pesa
 
Back
Top Bottom