Natakiwa kufuata taratibu zipi kwenda kujitambulisha kwa wachaga?

Njo Pm ntakupa taratibu zote mpaka utafurah mwenyewe mambo ni simple sana Mimi mwenyewe ni mchaga nimelipiwa mahari juzi na mtu wa kusini na Pete tumevalishana, nimeguswa sana kukusaidia kiushauri kuhusu hili swala lako
Kwa wale waliovuka hii stage, naomba uzoefu wenu wa namna ambavyo natakiwa kufanya ili nikajitambulishe Kwa mke wangu tarajiwa Moshi, kufupisha story ni kwamba huyu binti ni mjamzito sasa, wazazi wake wananikomalia niende wakamfahamu baba wa mtoto ambaye ni mimi.

Nimeukwepa sana huu mtego lakini nimeona tu nikaitikie wito, Naombeni mnipe mbinu,bajeti, na yanayojiri kule ili nisiwakwaze.
 
Mtu wa kusini Mmakonde au Mnykyusa(Nyanda za juu)
 
Wachaga hawana shida,mtume kwanza mtu wa makamo akutane na wazee wa binti wamwambie vitu kwa ajili ya mahali ambavyo havizifi milioni moja. Kikubwa zaidi siku ya kulipa mahali muoaji ndo unagharamia ile shughuli yaani chakula na vinywaji ambavyo vinakositi kama laki tatu hadi nne
 
Kuna baadhi ya mambo aliniambia na nimeshaanza kuyatekeleza ila sasa si unajua asije akawa anataka tu jambo lake litimie, nikaona bora nije jukwaani hapa kwa wataalam

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
Mwambie awaambie wazazi wake wakupe mahari ya kichaga,yani humalizi hata laki 5...ila wakija na zile hesabu za 2m au 3m waachie binti yao
 
Kama una pesa.., sio hela ni pesa.., wewe nenda haina shida. Ila kama huna ....!! Jichange change upate za kutosha kisha kakodi gari ya kujiendesha mwenyewe, tafuta suti peya mbili tatu, uwe na bajeti kwa ajili ya wakwe. Ukishatoka huko hakikisha humuonani mpaka umemfyatulisha mamsapu fasta fasta watoto watatu. Kisha watumie nauli waje wapaone uswasi mnapoishi, chumba kimoja kimetenganishwa na pazia. Watamaindi ila watapoa maisha yatasonga...
hiyo sio chumba ni stooo,yani humo ndani kila kitu kaweka,ndoo za maji masufuria ,jiko etc
 
Mbege debe kadhaa, kreti 2 au 3 za bia, soda maybe kreti 2au 3, kuwa na hela kiasi kwa ajili ya kupunguza yale ya lazima mfano blanketi la mama unaweza toa hela, mbuzi unaweza toa hela at least ukiwa na 1m utatembea parefu Sana, uchagani hamnaga mbwembwe nyingi man
Mahari ya kichaga hata laki 6 haiishi,shida ni wazazi kutaka kumalizia shida zao kwa watoto...ukikuta mzazi anaejielewa humalizi hata hiyo milioni
 
Huo ni ujinga mkubwa sana unaotaka kujaribu kufanya. Huyo mtoto utamsahau maana atalelewa na bibi na babu wa kwa mama yake.

Ukimpa msichana ujauzito lazima kwao wakufahamu. Hapo utapigwa faini na mengine wao ndio watakuelekeza ya kufanya. Kajitambulishe acha uboya. Tanguliza mshenga kwanza ndio uje uende na wewe ili upate kujua kinachohitajika. Kila nyumba na mambo yake.
Hakuna kinachoshindikana sema usijimwambafai kwa kutaka kupata sifa. Be humble
Daah kila mtu na ntu wake,faini inategemeana na mtu kuna wengine ukiwaletea hizo wanakuachia binti yako,wazazi wenye njaa ndio huendekeza hayo unakuta gharama zinafika 2m au zaidi
 
Huwezi ukaita taratibu na mila zetu za kishamba. Jitafakari mkuu. Na kama ni ndoa kwanini uliamua kumuacha? Haukua unampenda? Si kuna hata zile ndoa za mkesha kama huna hela ya sherehe jamani. Roho si inakuuma sana? Umawezaje mwachia mtu unayempenda hv jaman. Ama tabia mulishindwana?
Pole sana. Mungu ni mwema. Huenda pia akawa na sababu zake. Huwezi jua
Mshiki ukiona ndoa hakuna jua sio fungu lako,ndoa hailazimishi inatoka rohoni...shida ingine dada zangu ni viburi sana
 
Mshiki ukiona ndoa hakuna jua sio fungu lako,ndoa hailazimishi inatoka rohoni...shida ingine dada zangu ni viburi sana
Dah, umesema vyema msasha. Ila jamaa inaonekana anampenda sana na inamuumiza kumkosa. Mwenyezi Mungu ampe nguvu katika hili qpate amani ha moyo. Viburi kweli tunavyo ila malezi ndo tatizo. Tumelelewa tofauti
 
Kwa wale waliovuka hii stage, naomba uzoefu wenu wa namna ambavyo natakiwa kufanya ili nikajitambulishe Kwa mke wangu tarajiwa Moshi, kufupisha story ni kwamba huyu binti ni mjamzito sasa, wazazi wake wananikomalia niende wakamfahamu baba wa mtoto ambaye ni mimi.

Nimeukwepa sana huu mtego lakini nimeona tu nikaitikie wito, Naombeni mnipe mbinu,bajeti, na yanayojiri kule ili nisiwakwaze.
Tafuta mtu anayejua mila za uchagani,mshenga,baadhi ya ndugu zako,tia timu,kule ni kula misosi tu,.
Mi nilienda na mjomba,shangazi,kaka zangu,mjomba ndie aliyetoa utambulisho,kwa sababu na yeye ameoa uchagani,maisha yalikuwa poa.
 
Shukrani sana kiongozi kwa mchango wako

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
Dah, umesema vyema msasha. Ila jamaa inaonekana anampenda sana na inamuumiza kumkosa. Mwenyezi Mungu ampe nguvu katika hili qpate amani ha moyo. Viburi kweli tunavyo ila malezi ndo tatizo. Tumelelewa tofauti
Nimeona mamba familia yenye maisha mazuri mahari binti ndio alipanga ya kichaga,sikumaliza milioni....shida dada zangu mnapenda kuolewa sana ila mahari wazazi wenu wanataka kunalizia shida zao mara 3m
 
Muulize unayekwenda kujitambulisha kwao. Atakueleza kile wazee wake wanachotaka, kazi kwako kutekeleza.
 
hii ni trick simple na utanishukuru baadae wachana na mambo ya pesa nyingi ila usikose 500k at least, na ufanye hima kuonana na baba mkwe wako kabla ya mfumo wote then ujue weakness yake kwanza,uyo ndo serikali kuu na ukifanikiwa kumweka chini basi unaoa
usiende kichwa kichwa
hahaha. we jamaa jinga sana!! kwa hiyo atafute kiini kwanza sio
 
Back
Top Bottom