Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,196
113,466
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Maxence kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hiyo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa Rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha Rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
 
JF ni Jukwaa linalofuatiliwa sana na viongozi.

Inasemekana baada ya viongozi kutoa matamko yao, huja huku haraka kuangalia maoni ya watanzania. Wanakuja huku kwa kuwa waliopo huku wanajielewa.

Vita dhidi ya JF ni vita dhidi ya wanao jielewaa.

Ila wakumbuke kuwa JF haijawahi kushindwa na haitoshindwaa!

[HASHTAG]#GREATJF[/HASHTAG]
 
Ubaya wa ukada ni unaona udikteta asubuhi ila jioni unaona huohuo udikiteka kuwa umahiri.
Ubaya wake ni pale ndugu yako au maslahi yako yakiguswa na kwa unafiki wa umri unampinga.
Ila akikamatwa fulani,kupigwa n.k ambaye hali chakula nawe,basi mdomo hutoa sifa tu kwa dikteta.
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom