chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 19,666
- 22,674
Habari zenu wana-MMU!!
Kuna rafiki yangu ambaye naweza kumuita kaka pia maana tangu tukiwa wadogo tumeishi pamoja ila kadri muda ulivyokwenda kila mtu aliekea kule ambapo alipotegemea kujenga maisha yake,.
Huyu rafiki yangu tunaheshimiana sana nikimaanisha wote tumetokea mtaa mmoja tangu tukiwa wadogo hivyo tunaelewana kwa undani zaidi,
Tumekutana mjini na kuendeleza urafiki wetu tangu tukiwa wadogo, mara kwa mara tumekuwa tukijumuika pamoja kupata hata vinywaji huku tukijikumbushia mambo ya utoto kule kijijini,.
Lengo la kuanzisha hii thread
Huyu rafiki yangu amekuwa akinishirikisha matatizo yake mara kwa mara na pale ninapokuwa na uwezo huwa ninamsaidia maana naamini hata mimi kuna siku nitapata shida na nitaomba msaada wake,.
Mke wa huyu rafiki yangu alipata ujauzito na siku ya kujifungua huyu rafiki yangu hakuwa na fedha za kumgharamia mke wake hivyo aliniomba nimsaidie kiasi fulani cha fedha ambacho nisingependa kukitaja ili aweze kugharamia huduma hiyo huku akiniahidi kurejesha kiasi hicho muda si mrefu,.
Cha ajabu takriban miezi mitano imeshapita mpaka sasa hajanirejeshea fedha zangu pamoja na mimi kumsamehe nusu ya kiasi nilichomsaidia,.
Kila ninapompigia simu analia shida ilhali mimi najua kweli mtu huenda mambo yakawa bado hayajamuwia vizuri lakini nashangaa kwa nini hata nusu ameshindwa baada ya kumsamehe sehemu ya deni hilo,.
Kwa sasa nazihitaji hizi fedha ili na mimi niweze kuendesha mambo yangu lakini naona Jamaa hana dalili za kurejesha fedha zangu hata nusu,..
Mke wa rafiki yangu tunafahamiana maana Jamaa alishanitambulisha kwake mimi kama mdogo wake,.
Wana-MMU mnaonaje nikamshirikisha Shemeji labda huenda akanirejeshea fedha zangu!!
Je nimueleze vipi mke wake kuhusu deni hili?
Je nimwambie kwamba hizi hela nilimkopesha mume wake wakati yeye anajifungua?
Ushauri wenu ni muhimu kwangu wadau,..