Uchaguzi 2020 Nataka nimpigie kura Dkt. Magufuli ila kwanza nijibiwe haya...

Peculiar

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
821
689
1. HOJA YA WANYONGE.
a)Magufuli amekua akijinadi kuwa yeye ni raisi wa wanyonge.
-Je anaweza kutuambia wakati anaingia madarakani aliwakuta wanyonge wangapi na mpaka asa wapo wangapi?

b)Kuwapandishia bei bidhaa ndio kuwasaidia wanyonge? Mfano sukari: alivyoingia madarakani ilikua inauzwa 1800/= ila sasa ni 2500/= na kuendelea.

c)Kuwauzia vitambulisho wamachinga kila mwaka 20000/= ndio kuwasaidia wanyonge?
Kama lengo ni kuwasaidia kwanini wauziwe bei juu halafu kila mwaka? Kitambulisho gani huwa kinatolewa kila mwaka?

2. HOJA YA UFISADI
Kama kweli Magufuli anapambana na ufisadi...
a)Zile trilioni 1.5 ambazo CAG aligundua zimepotea atuambie zimeenda wapi? na kwanini alimfuta kazi CAG baada ya kuonesha upotevu wa pesa izo badala ya kudili na waliosababisha pesa izo zipotee?

b) Kama kweli Magufuli anachukia ufisadi,inamana hajanusa harufu yoyote ya ufisadi na utakatishaji fedha/uhujumu uchumi katika masakata ya madini aliyoyapata bwana lizer hasa kwa kuzingatia hiki ni kipindi cha uchaguzi?

c)Yule aliyekula hela za tassaf alichulia hatua gani Kama kweli anachukia ufisadi?

3. HOJA YA UWAZI
a)Kama anavosema kuwa kilichofanyika kimefata Sheria.
Kwanini alipitisha Sheria ya bunge kutokuoneshwa mubashara/live? kwa faida gani?

b)Kwanini Miradi mingi aliyoianzisha haijajaliwa bungeni na hata iliyodiliwa ilijadiliwa harakaharaka na kupitishwa harakaharaka.
Miradi Kama

-Ununuzi wa ndege
-Ujenzi wa reli n.k.

c) Magufuli anasema ametekeleza kwa kishindo.sawa ni yeye anasema...
Je, miradi mingapi aliyoianzisha na imekamilika Hadi aseme ametekeleza kwa kishindo?

4. HOJA YA VIWANDA.
Humu JF tupo watu kutoka maeneo mbalimbali Tanzania. Naomba niwaulize wanajf
Viwanda vilivyopo maendeo unayoishi vingi vilijengwa awamu gani ya uongozi?
Maana Mimi huku niliko viwanda vilivyojengwa awamu hii ni vya kutafuta kwa tochi.

5. HOJA YA MAENDELEO KWA UJUMLA.
Maendeleo ya watu ni lazima ya husishwe na afya zao,uhakika wa kupata riziki,elimuusafiri, Uhuru wao na vitu Kama hivyo..
Je wanajf wenzangu huko mliko ni maendeo gani imewaletea awamu hii ya Magufuli ambayo kabla yake hayakuwepo?

6. HOJA YA KAULI ZA MAGUFULI.
kauli ya rais ni Sheria,anapoiongea walio chini yake hufanyia kazi kauli zake..
-je aliposema kuwa Kama" WAKURUGENZI AMEWATEUA YEYE,AKAWAPA GARI YA KUEMBELEA YEYE,AKAWALIPA MISHAHARA YEYE halafu kwenye uchaguzi waje watangaze kuwa mtu asiye wa chake ndio kashinda atawafukuza kazi" je alimaanisha Nini?

-aliposema (kwa ukali) kuwa wamiliki wa vyombo vya habari hawapo huru..., alimaanisha Nini..

-aliwa kusema hela kuwa adimu mtaani ndio maendeleo... real!!?

7. HOJA YA KUCHUKIA UONEVU
-clauds fm walivamiwa na makonda akiwa na Askari wenye bunduki mbona hakuchukua hatua stahili?

-nape alitishiwa bastola hadharani mbona hakulaani kitendo hicho?

-walioondoa camera,Askari wa zamu wa eneo alilopigiwa risasi tundu lisu nao bado hawajulikani? kwa nini yeye Kama raisi haoneshi kuguswa na hili.

8. KATIBA MPYA
awamu iliyopita ilianzisha mchakato wa katiba mpya ambao kimsingi ulifurahiwa sana na wananchi.
Je,kwanini hajahakikisha unakamilika na katiba mpya inapatikana hasa ukizingatia ni jambo zuri na limekwisha tumia gharama kubwa mpaka lilipofikia? Kuliacha tu juu juu hajaona Kama ni kuwanyima wananchi haki yao na kuinyima thamani pesa iliyotumika katika mchakato mzima?

9. HOJA YA AHADI ZA MAGUFULI
anasema ametekeleza kwa kishindo.
a)Je,zile milioni 50 kila Kijiji alizoahidi wakati wa kampeni huko kijijini kwenu mlishazipata?
b)zile laptop zenu walimu mlishapewa?
c)kwanini amekua mchoyo wa ajira ilihali yeye mwenyewe kaajiriwa?

10.Ni hospitali gani ya serikali huko uliko mwana jf ambayo ukiwa unaumwa ukienda kutibiwa utapewa dawa zote ulizoandikiwa na daktari?
-kwanini watu binafsi wawe na dawa kwenye maduka yao halafu serikali ikose? Inamaana serikali Haina hela za kununulia madawa kwa ajili ya watu wake walipakodi?

11. HOJA YA UCHUMI WA KATI
Magufuli anasema ametufikisha uchumi wa kati sawa hatukatai,lakini mpaka tulipofika Safari ilianza kabla yake
a) Je,yeye amtuvusha kutoka wapi mpaka wapi? Namba hazidanfanyi. Mfano: uchumi wakati iwe ni elfu moja(1000) nayeye wakati anachukua nchi tulikua kwenye 600 kwa hiyo hapo atakua ametuvusha kwa 400 Hadi kufikia lengo.
Je,yeye alitukuta tupo kwenye ngapi na Sasa tupo kwenye ngapi? Atuambie kwa namba maana namba hazidanganyi.kusema tu uchumi wa kati uchumi wa kati haileti mantiki bila ushahidi wa namba.

b)je,wewe mwana jf na wewe au watu wa huko uliko na wao uchumi wao umepanda mpaka kufikia uchumi wa kati tayari kuelekea uchumi wa juu kabisa?

12. DENI LA TAIFA
wakati Magufuli anaingia madarakani lilikua shingapi na Sasa limebaki shingapi?

HOJA ZIPO NYINGI SANA ILA NIKIJIBIWA HIZI CHACHE KWA UFASAHA MAGUFULI ATAJIHAKIKISHAI KURA YANGU.
karibuni
 
Wewe unahangaika kueleza matatizo ya watoto wako, unataka yawe ya Taifa zima: Hiyo ndo ignorance ya wapiga kura. Watu wanasema eti sipati mulo kwa siku, hilo nalo ni suala la mgombea urais?
 
Tumetenga zaid ya billion 250 kwa ajili ya afya,kila mwaka tunatao billion 420 kwa ajili ya elimu bure,tumetoa billion 480 kwa ajili ya mikopo kwa wanachuo,tumetenga billion 120 kwa ajili ya maji,billion billion billion billion billion nakuendelea.

Hamyaoni haya
 
Magufuli hafai kabisa Mkuu.
Huku kwetu alituahidi.

i. Alituahidi Ujenzi wa uwanja wa Ndege msalato. Hakjna kinachoendelea.

ii. Alituahidi ujenzi wa Barabara ya pete ring road hakuna kinachoendelea.

iii.Alituahidi ujenzi wa kiwanja kikubwa cha michezo akishirikiana na Mfalme wa Morocco Kimya

iv. Alituahidi ujenzi wa Hospital ya Uhuru tangu 2017 hadi leo.

V. Ujenzi wa soko la kisasa Dodoma hadi leo kimya.

Mwaga pombe 2020

NI YEYE
 
Tumetenga zaid ya billion 250 kwa ajili ya afya,kila mwaka tunatao billion 420 kwa ajili ya elimu bure,tumetoa billion 480 kwa ajili ya mikopo kwa wanachuo,tumetenga billion 120 kwa ajili ya maji,billion billion billion billion billion nakuendelea.........

Hamyaoni haya
Wanayatoa wapi hayo mabilioni?
Wajibu wao ni nini?
Yanafaida gani ikiwa wanayafanya hayo kwa masimango ubabe, kunyima watu kujadiri mambo ya taifa lao?
 
Wewe kura yako baki nayo tu..

Sisi hatuitegemei kabisa,tunae mtu pale anauteuzi atajua anafanyaje kuifidia.

Hizo hoja zako kaa nazo mkajadili vijiweni.
 
Back
Top Bottom