Nyankuru Wankuru
JF-Expert Member
- Apr 22, 2018
- 1,199
- 1,346
Wadau mm kwa takribani mwaka nimekuwa nikihangaika kufuata familia yangu kwa kuomba uhamisho.
Taratibu zote za maombi zimefanyika
Cha ajabu nimejibiwa majibu yasiyokuwa na huruma na kibinadamu.
Sasa nimeamua kufanya maamuzi magumu kabisa.
Jumanne ya tarehe 9.4.2019 nitatembea kutoka mkoani pwani hadi Ikulu ya Rais jijini dar es salaam kwa lengo la kumuomba Rais wetu mpendwa kuingilia kati suala hili.
Wakuu naombeni ushauri wenu , niende ikulu kwanza au nianze kwa katibu mkuu.
Mimi nataka nikamwambie Rais wetu yote yanayotendeka pale utumishi.
Watumishi wa umma wananyanyasika sanaa na hawa watu wachache wasio kuwa na huruma na familia za watumishi.
Mtu anaomba uhamisho na anasema atajigharamia wao wanamuandikia barua isiyofuata taratibu za kiutumishi.
Sasa nimeamua kumfuata Rais wetu kumueleza yote. Na kumuambia manyanyaso watumishi wanayopata kutoka kwa mkurugenzi wa utumishi kurugenzi ya utumishi na uhamisho kwa watumishi.
Sent using Jamii Forums mobile app