Nataka nikamnunulie Mpenzi wangu Kufuli, ni aina gani ya kufuli ni nzuri? Nisaidieni

Tamati

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,085
1,956
Habari zenu wanaJF, ni matumaini yangu mpo salama salimini huku mkiendelea na kupambana kupata cha kupeleka kinywani. Kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine hawako salama, Mungu awajalie mpate kuwa salama na kurejea kwenye majukumu yenu ya kila siku.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nilimuahidi mpenzi wangu kumnunulia kufuli(chupi) kama kama miongoni mwa zawadi za hapa na pale kwenye kuimarisha mahusiano yetu.

Muda si mrefu kuanzia sasa nitasafiri kwenda kumsalimia na kumpelekea hiyo zawadi. Jana nilikuwa nachati naye akanikumbusha hii ahadi niliyomuahidi aliniuliza Unakumbuka zawadi angu my?



Nikamjibu kwa utani nikamwambia sikumbuki, nikumbushe....

Naombeni mnitajie aina nzuri za kufuli, sehemu(machimbo yake) na hata bei zake kwa maeneo ya jiji la Dar es Salaam, ukiambatanisha na picha itakuwa bora zaidi.
 
Hiyo na pasiwedi unamwekea
IMG_20181112_111307_091.jpg
 
Back
Top Bottom