Nataka nijaribu kunywa pombe ila naogopa matokeo

ramona

Senior Member
Apr 3, 2017
174
264
Jamani muda mrefu nina hamu ya kujaribu kunywa pombe ila naogopa reaction yake isije nitia aibu nikaja fanya mambo ya ovyo.

Naonaga tu watu wanywa wachanganya na maji, sitaki shirikisha watu wangu wa karibu wengi wao waabudio dini hawawezi nipa ushauri niutakao zaidi watanishushia mistari ya kwenye vitabu.

Mimi nataka ninywe kidogo tu isinidhuru mpaka nikaja shindwa jitambua yaani nataka nitoe ka aibu nilichokua nacho nisiwe na aibu kabisa. Haya mnisaidie ninywe kiasi gani ili isinidhuru na kunitia aibu au kuropoka ovyo?
 
jamani muda mrefu nina hamu ya kujaribu kunywa pombe ila naogopa reaction yake isije nitia aibu nikaja fanya mambo ya ovyo. naonaga tu watu wanywa wachanganya na maji, sitaki washirikisha watu wangu wa karibu wengi wao waabudia dini hawawezi nipa ushauri niutakao zaidi watanishushia mistari ya kwenye vitabu. mimi nataka ninye kidogo tu isinidhuru mpaka nikaja shindwa jitambua yaani nataka nitoe ka aibu nilichokua nacho nisiwe na aibu kabisa. haya mnisaidie ninywe kiasi gani ili isinidhuru na kunitia aibu au kuropoka ovyo?
Nakushauri kama dada yako.

Usithubutu.
 
Kunywa chupa moja ya Serengeti lite au Castle lite hazileweshi kabisa.

Pili ukiwa unakunywa jaribu kuwa unachat ukiona umeanza kukosea spellings ujue zilishaanza kuingia. Au ukiwa unakunywa use unasimama kidogo ukiona mwili unajihisi mwepesi acha.

Baada ya hapo kunywa maji mengi sana pombe itashuka kiwango.
 
Nakushauri kama dada yako.

Usithubutu.
asante kwa ushauri wako ila nataka ninywe kidogo nitoe aibu. nina aibu sana nimejaribu njia za kawaida sijafanikiwa ndo maana nataka jaribu huku labda nitafanikiwa
 
Umechelewa sana had sasa hujawahi da! Kwa vile wewe ni ke anza na sengereti lite tano tu. Aisee pombe raha sana hutajuta, hutakuwa mbea-mbea maana utakuwa bize. We weita huoni Kama Castle Lager yangu kubwa imeisha? Lete ya vuguvugu
 
Beer huwa ni chungu lkn hailewesh haraka hvyo unauwezo wa kujicontrol wakat unaendelea kunywa.... Chukua lite beer (serengt lite, tusker lite au castle lite) hiz huwa zinakiwango kidog sana cha kilevi changanya na bitter lemon au sprite (hiz ni soda) kwa ajili ya kupunguza uchungu isije kuwa kama unakunywa dawa... Kunywa taratibu huku ukiskilizia mrejesho kichwan...
.
Hata mvinyo/wine na wenyew ni mzuri mno kwa kuanzia ila hiz mara nying huwa ni tamu hvyo zinahitaji umakin ukijisahau ukanywa kama juice itakufanya mbaya
.
Kwa mara ya kwanza unaweza kujaribu ukiwa hom kwako
 
Duh njoo tujifunze wote mi pia nataka ninywe serengeti lite naskia nzuri ila pia wanasemaga smirnoff ice huwa sio mbaya kwa watoto wa kike haileweshi haraka.
Kama unaweza njoo tujifunze weekend hii, hata tukinywa tatu tatu sio mbaya mi ntalipia usihofu na itakuwa siri yetu.
 
Kunywa chupa moja ya Serengeti lite au Castle lite hazileweshi kabisa.

Pili ukiwa unakunywa jaribu kuwa unachat ukiona umeanza kukosea spellings ujue zilishaanza kuingia. Au ukiwa unakunywa use unasimama kidogo ukiona mwili unajihisi mwepesi acha.

Baada ya hapo kunywa maji mengi sana pombe itashuka kiwango.
vipi kwa zile bia za kuzimuliwa na maji? ninywe kama glasi ngapi?
 
Nakushauri kama dada yako.

Usithubutu.
Ushauri wa hovyo kabisa huu....
Ebu mshauri kijana aingie kwenye chama chetu...
pombe+nooma.JPG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom