Nataka niishtaki bank kwa kutoa pesa zangu zote (dola 50,000) tokea mwaka 2017 bila idhini yangu na nimechukua bank statement

Restarting

Member
Jan 28, 2020
80
106
Nataka niishtaki bank imetoa pesa zangu zote (dola 50,000) tokea mwaka 2017 bila idhini yangu na nimechukua bank statement kweli inaonesha pesa ilitolewa toka 2017.

Vipi hapo kwa wataalamu wa sheria hii case imekaaje kwenye masuala ya kunilipa na je kutakuwa na compersation yoyote kutokana na usumbufu nilioupata kipindi hiki chote toka wanichukulie pesa zangu?
 
sio porojo Mkuu ni serious case kabisa, na ina story ndefu huko mwanzo...na bank statement sio kama nashindwa kuweka bali naona si vyema kuweka, muhimu nahitaji ushauri wenu...najua humu kuna watu wataalamu wa haya mambo
Sasa tokea 2017 umekaa kimya tu mkuu?
 
Hebu tiririka kwa kirefu tujue tunakusaidiaje?
1.Hela ulizipata wapi
2.Bank ilikupa sababu gani za kuzitoa hizo hela?
3.kwa kosa gani ulifungwa?
4.Why USD na sio TSH?
5.Unataka kupewa msaada gani humu jf?
Tiririka kwa kuyajibu hayo maswali niliyokuuliza ili tujue wapi pa kuanzia.
 
Hebu tiririka kwa kirefu tujue tunakusaidiaje?
1.Hela ulizipata wapi
2.Bank ilikupa sababu gani za kuzitoa hizo hela?
3.kwa kosa gani ulifungwa?
4.Why USD na sio TSH?
5.Unataka kupewa msaada gani humu jf?
Tiririka kwa kuyajibu hayo maswali niliyokuuliza ili tujue wapi pa kuanzia.
Namiliki lodge yakulaza wageni kisiwan znz, so nikajiingiza kwenye system ya booking.com ili niweze kurahisishia wageni kutoka angle zote za dunia kufanya booking kwa urahisi sana, nikafungua bank acc na wakanipa ile POS machine na wateja wakawa wanafanya booking from all over the world, ikawa ndani ya muda mchache nimepiga pesa nzuri maisha yakawa safi, sasa baadhi ya wafanyakazi wa bank sio waaminifu walipoona pesa ni nyingi, wakazuia account yangu...

Nilipo kuwa hapa dsm bila kujua nilienda kutoa pesa ikawa nashindwa pata huduma ikanibidi niingie ndani pale HQ ya bank kuulizia mbona siwezi kutoa pesa na acc yangu inapesa...nimekaa naeleza tatizo langu...mara ikapigwa simu wakaja baadhi ya wafanya kazi wa pale pale bank ambao mm nawajua coz hiko kimachine ninachotumia ndio walinikabidh wao, wakaniambia niingie ndani, nikaingia wakaniuliza kwann unaiibia bank...nikawaambia mbona sijafanya wizi wowote ule na kama pesa booking zote c munaziona, so nani nimemuibia after that wakavuta simu kinyemela kuwatwangia polisi wakaja kunibeba kutokea pale bank bila maaelezo hadi msinbazi, pale napo nikaambiwa nimewaibia bank...

Nikawaeleza kama nilivyowaeleza hapo awali watu wa bank...sasa nilichokuja kugundua wale wafanya kazi walikula njama na polisi, wahakikishe sichomoki na niende jela baada ya hapo watoe pesa wagawane, wakafanikiwa kwa asilimia chache sana coz sikufungwa ila nilikaa bahabusu kwa muda wote huo nikawa natokea gerezani kwenda kusikiliza kesi yangu mahakamani nikapambana nipate zamana nitoke gerezani kwa muda wote huo nikapata dhamana sasa hivi natokea home kwenda kusikiliza kesi yangu, na ushahidi kwa upande wao wameshatoa kama nimewaibia ila ushahidi wenyewe haujitoshelezi wameshindwa kumleta mtu yoyote yule aliyeibiwa na mm, na mimi kwa upande wangu nimeshajitetea tayari so next month naenda kusikiliza hukumu itakuwaje, ila chakushangaza pesa zilizopo kwenye acc walikwara zote kwakuhisi sitoweza toka tena...

Ila chakushangaza kwann case kama nimeiibia bank case wafungue wafanyakazi wa kawaida na sio mwanasheria wa bank, na bank kama bank haijui kama kuna case inaendelea mahakamani kuhusu kuibiwa kwa pesa...Hivyo sasa nilikuwa nasubilia case hii yao iishe ndio nifungue yangu but naona imechukua muda mwingi sana haijaisha hadi hivi sasa....nikapata wazo niishtaki bank moja kwa moja kwa nn imetoa pesa zangu bila ya ridhaa yangu....sasa ndio najiuliza hapa na nataka kusikia kutoka kwenu hii issue imekaaje hapa...

NOTE: Bank haina taarifa kama inacase na mimi zaidi ya wale wale wafanya kazi na nimejitahidi kuonana na MD wao wale jamaaa wanafanya kila aina ya nia nisionane nae na wamefanikiwa kwenye hilo coz kila nikienda nionane na MD wananizuia wanataka niwaeleze wao kwanza nini shida wakishindwa ndio iende kwa MD...natumai umenielewa coz mimi kwenye kueleza majambo najihisi sio mfasaha sana
 
Hata kama mtu akifungwa alieua, haki zake za msingi huwa hazipotei kisheria.

Kabla ya kukurupuka, jaribu kufatilia;

1) Account walii "FREEZE" baada ya kutokutumika kwa muda mrefu. Kama account walii freeze, basi ukii activate pesa yote inarudi.

2) Account haiku "SEIZE" ila pesa zilihamishwa kienyeji, na zilikwenda katika account ya nani na kwanini. Kama pesa zilihamishwa kienyeji basi nenda kwa wanasheria waiandikie barua bank kuomba sababu za kisheria kwanini walitoa ile pesa bank bila idhini yako, na uwape muda kama ni wa siku 14 au 21 wawewamekupatia majibu. Wasipokupa majibu ya kuridhisha, basi unawafungulia mashtaka na unashinda case (Utalipwa fidia pia).
 
Hata kama mtu akifungwa alieua, haki zake za msingi huwa hazipotei kisheria.

Kabla ya kukurupuka, jaribu kufatilia;

1) Account walii "FREEZE" baada ya kutokutumika kwa muda mrefu. Kama account walii freeze, basi ukii activate pesa yote inarudi...
imetolewa 2017
 
Kwanza pole sana mkuu, pili mshukuru sana Mungu umebahatika kupata dhamana na uko nje.

Tatu, hiyo kesi kwa hichi kipindi ikipelekwa inavyostahili utafungwa kwa utakatishaji wa pesa na uhujumu uchumi.

Nimeshuhudia watu wakiingiza familia zao matatizoni kwa mambo kama hayo, wengine kwa kutokujua na wengine kwa tamaa ya utajiri wa haraka haraka, sijajua wewe uko kundi gani.

Kwa mtu mwenye uwezo wa kumiliki lodge kuweza kutengeneza kiasi hicho cha pesa hii kesi ungeshaimaliza kitambo. Ulishindwa kutoa vielelezo vya chanzo cha hizo pesa.

Tafuta mwanasheria, mweleze ukweli wooote (achana na hii hadithi umeiandika hapa). Kisha atakushauri nini cha kufanya. Vyovyote vile, bank wana makosa kuchukua pesa wakati kesi inaendelea.
 
Kwanza pole sana mkuu, pili mshukuru sana Mungu umebahatika kupata dhamana na uko nje.

Tatu, hiyo kesi kwa hichi kipindi ikipelekwa inavyostahili utafungwa kwa utakatishaji wa pesa na uhujumu uchumi...
Hii tunaiita lodge ila ukifika hapo kwa watu wa huku mutaita hotel...but iko vizuri ina kila kitu...na everything is there ukifika hautoboreka na pesa tumezipata kiharali kabisa sijafanya ubabaishaji wowote ule
 
Namiliki lodge yakulaza wageni kisiwan znz, so nikajiingiza kwenye system ya booking.com ili niweze kurahisishia wageni kutoka angle zote za dunia kufanya booking kwa urahisi sana, nikafungua bank acc na wakanipa ile POS machine na wateja wakawa wanafanya booking from all over the world, ikawa ndani ya muda mchache nimepiga pesa nzuri maisha yakawa safi, sasa baadhi ya wafanyakazi wa bank sio waaminifu walipoona pesa ni nyingi, wakazuia account yangu..
Ukapiga pesa nzuri ndani ya muda mchache maisha yakawa mazuri,baadhi ya wafanyakazi wa benki Wakazuia account yako.je unaweza kutaja Jina la benki?
 
nikawaeleza kama nilivyowaeleza hapo awali watu wa bank...sasa nilichokuja kugundua wale wafanya kazi walikula njama na polisi, wahakikishe sichomoki na niende jela baada ya hapo watoe pesa wagawane, wakafanikiwa kwa asilimia chache sana coz sikufungwa ila nilikaa bahabusu kwa muda wote huo nikawa natokea gerezani kwenda kusikiliza kesi yangu mahakamani nikapambana nipate zamana nitoke gerezani kwa muda wote huo nikapata dhamana sasa hivi natokea home kwenda kusikiliza kesi yangu
Unaona unavyojichanganya sasa? Kwa maelezo umesema pesa haijachukuliwa yote, inakuwaje isome zero balance?
"ila chakushangaza pesa zilizopo kwenye acc walikwara zote kwakuhisi sitoweza toka tena "

Hiki ndicho alichokisema

Nimeshaona nilipojichanganya boss wangu. Namuomba radhi mleta mada. Alivyosema hawakufanikiwa kwa asilimia zote nikajua kutoa pesa. Nimeshamuelewa.

Benki kosa lao ni kutoa pesa, walitakiwa wasitishe miamala yeyote hadi kesi itakapofikia mwisho ( hukumu kutolewa)
 
Back
Top Bottom