Nataka kwenda Tunduma, je kampuni gani ina mabasi ya Scania? Ushauri tafadhali

Mkuu Mbeya kuna gari nzuri sana SCANIA GEMILANG za kampuni ya SAULI pia kuna BENZ za kampuni hiyo.

Zipo kila siku kazi kwako mkuu

Kwenye ligi nadhani ndo zinaongoza kufika Mbeya na Dar, Kwa ninavyosikia hao wachina njia hiyo wamesalimu amri sababu hizo Scania F360 huwa zinapanda kitonga kama zinashuka vile na kuna ule mluzi au whisle wa Scania unasikia na mafua yake kabisa.
Hako ka mluzi ata mi hua nakapenda balaa!
 
Majinja gari za kazi hizo hasa ile CSN Volvo na Scania BUL

kuna siku nilikua natoka Dar to Sumbawanga, nilikua na newforce golden deer.

ile show niliyoishuhudia wakimwagiana moto na ile BUL.

kama lingetokea la kutokea hakuna jiwe lingesalia.

sema Majinga kawekeza sana kwenye mambio lakini sio usafi na starehe wakati wa safari.
 
Back
Top Bottom