Nataka kwenda Qatar au Dubai. Maisha ya huko yakoje?

MATTBOY

Senior Member
Jan 27, 2019
193
250
Habari za wakati huu wana JF,

Bila kupoteza muda mimi ni kijana wa Kitanzania ninayeishi nchini Kenya kwa sasa, maisha ya huku sio mbaya lakini kutokana na shauku yangu ya kutaka kufanikiwa kimaisha au kufikia malengo yangu niliyojiwekea, natamani tena nisonge mbele ya hapa nilipo.

Nilipokuwa nawaza pa kwenda nilipatana na rafiki mmoja aliyeniambia kuna fursa za kwenda kati ya hizo nchi mbili nilizotaja hapo juu.

Nikaona sio vema niende pasipo ichunguza vizuri, nikaona sehemu ya kuweza kupata msaada zaidi juu ya hizi nchi mbili ni hapa JF. So naomba ndugu zangu mnisaidie kuniambia kuhusu hizi nchi mbili kwa aliyewahi kuishi huko kikazi au kutembelea tu.

Kinachonipeleka Dubai au Qatar ni kwenda kufanya kazi ya Security.

Asanteni kwa ushauri wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
4,973
2,000
Nenda mkuu, nenda usirudi nyuma, sina uwakika na Dubai lakini Qatar kuna namba kubwa sana ya raia wa Afrika mashariki hasa kenya na Tz, kwa ambae amefika Doha miaka ya hivi karibuni atakubaliana na mimi, kimsingi usichague kazi, ili mradi iwe ya halali, ukifika Hamad I.A pale doha utakutana na vijana wengi wakisafisha maeneo ya Toilets huku wakiongea lugha ya kiswahili.
 
Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,412
2,000
Ujinga huanzia kwa madalali yaani wakati mnaondoka kichwani mwako kazi ni security ukifika kule mnapigwa mnada kwa maboss wa kiarabu so omba upate boss mstaaarabu na muelewa la sivyo yanatokea mambo ya kunyang'anywa pasport na kuwa mtumwa kwenye jengo ambalo linalindwa na walinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
unanikumbusha story moja inaotwa geza anasakwa auwawe. Jamaa alienda kutibua mipango ya mabosi kama hao wanaonunua watu kwenye minada na kuwageuza watumwa ndani ya jengo. Mnakaa hata miaka mitano bila kutoka nje na hakuna anaejua duh
 
MATTBOY

Senior Member
Jan 27, 2019
193
250
Ujinga huanzia kwa madalali yaani wakati mnaondoka kichwani mwako kazi ni security ukifika kule mnapigwa mnada kwa maboss wa kiarabu so omba upate boss mstaaarabu na muelewa la sivyo yanatokea mambo ya kunyang'anywa pasport na kuwa mtumwa kwenye jengo ambalo linalindwa na walinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana. Nasikia huwezi pesa passport na boss mpaka siku ya kurudi .na mkataba ni miaka 2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MATTBOY

Senior Member
Jan 27, 2019
193
250
Nenda mkuu, nenda usirudi nyuma, sina uwakika na Dubai lakini Qatar kuna namba kubwa sana ya raia wa Afrika mashariki hasa kenya na Tz, kwa ambae amefika Doha miaka ya hivi karibuni atakubaliana na mimi, kimsingi usichague kazi, ili mradi iwe ya halali, ukifika Hamad I.A pale doha utakutana na vijana wengi wakisafisha maeneo ya Toilets huku wakiongea lugha ya kiswahili.
Asante boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom