Nataka kwenda Mombasa, Kenya nikiwa na dhumuni la kutumia passport ili niweze kuomba mpya kabla ya 2020

Hechinodemata

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,467
3,227
Habari za asubuhi wapendwa

Napenda kukuri kwamba nina pasi ya kusafiria niliyoikata mwaka 2014 na itaisha 2024. Nilikata passport nilitegemea kwenda Zambia kufanya kazi lakini baada ya muda ile kazi sikuipata tena baada ya kampuni husika kusitisha zoezi la kuajiri tena.

Kutokana na zoezi la Serikali yetu kubadili passport zote kabla 2020, nataka kutumia passport yangu( kuichafua) ili niweze kuomba mpya. Ikumbukwe sijawahi kuitumia tangu niipate 2014. Nimeplan kwenda Mombasa kutembea hata kwa siku moja dhumuni ni kuitumia hii passport.

Naombeni wajuzi wa mambo wanieleze natakiwa kuwa na nini zaidi ya passport. Je, kuna maelezo yoyote natakiwa kuwa nayo zaidi ya kutembelea rafiki au biashara?

Naombeni kujua lolote

Natanguliza shukrani
 
Chanjo ya homa ya manjano, senti kidogo sh.500/= unagonga unaingia unakwenda kwenye duka hapohapo mpakani hiyo chapaa 500 unahonga mwanamke unarudi uhamiaji unagonga pasi yako umemaliza, haitumii zaidi ya nusu saa.
 
Boss ila wanasema kama hujawahi itumia huwezi pewa mpya, pass sio kitambulisho ni kwa ajili ya safari za nje tu
Kama nia yako ni kupata passport mpya, hakuna ulazima wa kuisafiria kwanza hio uliokuwa nayo. Wewe timiza vigezo vyote vinavyohitajika kwa muombaji wa passport na uende uhamiaji watakupa pasi mpya. Ukiona anakukwamisha mtu njoo nijulishe hapa.
 
Kuna wataalam hapahapa Bongo wana Stamp za Nchi za Kiafrika zisizohitaji Visa.
 
Kama nia yako ni kupata passport mpya, hakuna ulazima wa kuisafiria kwanza hio uliokuwa nayo. Wewe timiza vigezo vyote vinavyohitajika kwa muombaji wa passport na uende uhamiaji watakupa pasi mpya. Ukiona anakukwamisha mtu njoo nijulishe hapa.
Tutakuona wengi sana mkuu
 
Hauna haja ya kupoteza muda na Pesa Eti uchafue passport.. For what reason? We Nenda Uhamiaji kashughulikie passport mpya utapata bila Tatizo... Document zile za muhimu Nenda Nazo..
 
Kama mnafuatilia taarifa mpya au nzee ni kwamba passport siyo lazima uende ofisi ya uhamiaji unaingia kwenye mtandao wa uhamiaji kila kitu unakutana nacho huko.
 
Sio kweli! Kwenye mtandao ni ku download fomu ya maombi tu, na kupata namba ili ukalipie bank ile 20,000,baada ya hapo ndio uendelee kuijaza fomu, lazima tu ufike ofisi ya uhamiaji na hizo documents na viambatanisho vingine kukamilisha, zoezi! Hizo finger prints, utazifanyia mtandaoni?
 
Ndiyo ukweli huo, unaanzia mtandaoni na sidhani lazima kila kitu hata fomu uende uhamiaji?
 
Habari za asubuhi wapendwa

Napenda kukuri kwamba nina pasi ya kusafiria niliyoikata mwaka 2014 na itaisha 2024. Nilikata passport nilitegemea kwenda Zambia kufanya kazi lakini baada ya muda ile kazi sikuipata tena baada ya kampuni husika kusitisha zoezi la kuajiri tena.

Kutokana na zoezi la Serikali yetu kubadili passport zote kabla 2020, nataka kutumia passport yangu( kuichafua) ili niweze kuomba mpya. Ikumbukwe sijawahi kuitumia tangu niipate 2014. Nimeplan kwenda Mombasa kutembea hata kwa siku moja dhumuni ni kuitumia hii passport.

Naombeni wajuzi wa mambo wanieleze natakiwa kuwa na nini zaidi ya passport. Je, kuna maelezo yoyote natakiwa kuwa nayo zaidi ya kutembelea rafiki au biashara?

Naombeni kujua lolote

Natanguliza shukrani
Hakuna haja hiyo. Una ya zamani, fanya maombi ya mpya.
 
Hakuna sababu ya kufanya safari isiyokuwa na tija kwa makusudi la kuifanya ionekane kuwa imetumika. Pasi za zamani zinabadilishwa kwenda kwenye zile za kielekroniki, hii ni sababu tosha ya kumfanya mtu aliye na pasi ya zaman aibadilishe hata kama hajafanya safari yoyote nje ya nchi. Anza mchakato wa pasi mpya ... ni haki yako!.
 
Back
Top Bottom