Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

20m ndo uende Dubai au china?
au unataka kwenda kutembea?
simu aina gani? kama unanua smart phone za laki mbili 20 unanunua simu ngapi?
una duka atayari au ununue ndo uanze tembeza?

Binafsi naona tafuta biashara ingine hapa ya uhakika mtaji hata 15m

5m nenda Dubai katembee ujionee na ujifunze
15 M hata Kkoo kwa wauzaji wa jumla unaweza pata faida
Unaweza kununua hiace kwa hiyo pesa, ukiendesha mwenyewe uwezo wa kulaza 80-100 kwa siku unao kwa 100%.
 
Nauli toka Dar hadi Guangzhou ni kuanzia dollar 1200 hapo inategemea na siku hiyo ni go return

Nashauri pakia Ethiopia maana inatoa Kg nyingi.

Hii waweza book na kulipia mwenyewe au utembelee ofisi za Ethiopia. Mawakala huwa wanaongeza dollar 100 kwa kila ticket.

Ukifika Guangzhou uamuzi ni wako
Ukipakia Taxi utalipa hela nyingi inaweza fika 100 hadi 300yuan kama Laki hivi ili ufike Kati kati.

Au utumie Train yenyewe ni bei rahisi nadhani ni yuani chini ya 50

Hotel pia uchaguzi ni wako zipo ambazo utakuwa watu weusi ndio wengi na hizo bei zake ni ndogo kwa siku na zipo hotel za bei kubwa kazi kwako.

Kuhusu chakula kuna kihotel kwa Mtz wanapika chakula cha Ktz hapo Guangzhou.

Kutembezwa sokoni kuna Watz wako huko ila ndo hivyo ukienda nao wanakuongezea bei.

Kutuma mzigo unaweza kuja nao ila TRA airport hawatakuacha salama.
Au
Unalipia kwa Kg hao watz wanakutolea kwa dollar 10 kwa kila mzigo au 20000 kwa kila simu.
Wao wanajua wanavyofanya huko airport.
 
Kiongozi nenda china ndio uwakika. Na pia usikatishwe na hao GT P SALALY. Iyo ni pesa ndefu sana kwa kufanya bznes zako china.
Mm nilitishwa sana mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu kufata mzigo flani Dubai hatare mara kwa mtaji huo ni nauli na malazi tu mara kama unaenda kutembea sawa.
Ila baada ya kufika nilicheka sana mambo yako tofauti kabisa. Na kila mfanya bznes kama yangu nilie kutana nae na wazoefu uko Dubai wanasema mbona umekuja na kiasi kingi kwa bznes hii.
Tafta marifa sahihi kisha lianzishe mdau. Pambana tu kiongozi
Kwangu hii ndiyo ushauri mzuri
 
Watanzania wengi ni watu wawivu mno

1. Nauli kwenda na kurudi: USD 1,200

2. Chakula kwa siku: USD 22

3. Hotel Single Room: USD 50

4. Nauli ya mizunguko town: USD 49
(Taxi+Metro+Daladala)

5. Mzigo wako unaotaka kununua: (Na
hii tukupe jibu?): Minimum USD3,500
 
Kiongozi nenda china ndio uwakika. Na pia usikatishwe na hao GT P SALALY. Iyo ni pesa ndefu sana kwa kufanya bznes zako china.
Mm nilitishwa sana mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu kufata mzigo flani Dubai hatare mara kwa mtaji huo ni nauli na malazi tu mara kama unaenda kutembea sawa.
Ila baada ya kufika nilicheka sana mambo yako tofauti kabisa. Na kila mfanya bznes kama yangu nilie kutana nae na wazoefu uko Dubai wanasema mbona umekuja na kiasi kingi kwa bznes hii.
Tafta marifa sahihi kisha lianzishe mdau. Pambana tu kiongozi
SALALY ndiyo nini mkuu? rudi shule hata ya watu wazima unatuaibisha mabaharia
 
Back
Top Bottom