Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

Kwanza hongera sana...

Ushauri wangu kwako ni kwamba ungepata agents au wakala mwamimifu wa huko dubai au china akununulie mzigo atume au kama unaweza kuagiza mtandaoni mfano alibaba wanauza simu za jumla kwa bei nzuri mnoo ila unapaswa kuwa makini

NB;mitandaoni napo si salama wahitaji umakini ukiagiza kwa mtandao maana utapeli wizi na vitu feki ni vingi

Pia maagents nao sio waaminifu mimi sifaham hili ila nilimuona faiza aly kule insta akitumia watu mizigo yao kutoka huko china
Faiza ni yule demu wa sugu sio?

Yule siwezi muamini hata sekunde.
 
Usikatishwe tamaa na ndugu zako hapo juu.hiyo 20mil ni pesa ndefu. Wengi wao wanakupigia masimu ya 200k ambayo Kwa ujumla soko lake wewe mwenyewe unalijua, Kwa hicho kiwango ni wastan wa USD 8600. Hata ukisema utenge pesa ya mzigo Tu USD 4500 itatosha kabisa kununua mzigo. Ukisema uchukue headphone, chaja, ni zile accessories nyingine Kwa usd 1000 Tu mzigo utaukimbia mwenyewe.
Kwa hiyo unamshauri akanunue simu za kuuza kwa mafungu au kilo?
 
Asante sana bos kwamawazo yako nategemea kupata mengi zaid kwako maana mimi bado mgeni kabisa
Usikatishwe tamaa na ndugu zako hapo juu.hiyo 20mil ni pesa ndefu. Wengi wao wanakupigia masimu ya 200k ambayo Kwa ujumla soko lake wewe mwenyewe unalijua, Kwa hicho kiwango ni wastan wa USD 8600. Hata ukisema utenge pesa ya mzigo Tu USD 4500 itatosha kabisa kununua mzigo. Ukisema uchukue headphone, chaja, ni zile accessories nyingine Kwa usd 1000 Tu mzigo utaukimbia mwenyewe.
 
Asante nayaamini maneno yako pia hongera sana hapo ulipofika inakuwaje usafiri kwenda nakurud pia malaz itacost kama bei gani
Kiongozi nenda china ndio uwakika. Na pia usikatishwe na hao GT P SALALY. Iyo ni pesa ndefu sana kwa kufanya bznes zako china.
Mm nilitishwa sana mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu kufata mzigo flani Dubai hatare mara kwa mtaji huo ni nauli na malazi tu mara kama unaenda kutembea sawa.
Ila baada ya kufika nilicheka sana mambo yako tofauti kabisa. Na kila mfanya bznes kama yangu nilie kutana nae na wazoefu uko Dubai wanasema mbona umekuja na kiasi kingi kwa bznes hii.
Tafta marifa sahihi kisha lianzishe mdau. Pambana tu kiongozi
 
20m ndo uende Dubai au china?
au unataka kwenda kutembea?
simu aina gani? kama unanua smart phone za laki mbili 20 unanunua simu ngapi?
una duka atayari au ununue ndo uanze tembeza?

Binafsi naona tafuta biashara ingine hapa ya uhakika mtaji hata 15m

5m nenda Dubai katembee ujionee na ujifunze
15 M hata Kkoo kwa wauzaji wa jumla unaweza pata faida
good idea...
 
Kiongozi nenda china ndio uwakika. Na pia usikatishwe na hao GT P SALALY. Iyo ni pesa ndefu sana kwa kufanya bznes zako china.
Mm nilitishwa sana mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu kufata mzigo flani Dubai hatare mara kwa mtaji huo ni nauli na malazi tu mara kama unaenda kutembea sawa.
Ila baada ya kufika nilicheka sana mambo yako tofauti kabisa. Na kila mfanya bznes kama yangu nilie kutana nae na wazoefu uko Dubai wanasema mbona umekuja na kiasi kingi kwa bznes hii.
Tafta marifa sahihi kisha lianzishe mdau. Pambana tu kiongozi

Boss umeongea Point kubwa sana
Kwa mfano
1. Nauli to China (Go & Return) Ticket ni kiasi gani?
2. Malazi ni kiasi gani per night ( equivalent na Lodge zetu huku za 25,000-30,000 kwa standards)
3. Gharama ya Mzigo usafiri mpaka unaupata Tanzania
4. TRA Cost ya nguo labda za 5 million
5. Kuna any other cost tofauti na hizo hapo juu
6. Etc ??
 
Back
Top Bottom