Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

benjamathayo

Member
May 22, 2018
75
77
Mabaharia wafanyabiashara nimepata mpunga kidogo kama 20m kwamara yakwanza nataka kwenda dubai au china kununua simu hasa smartphone

Nimekuja kwenu kuomba ushauri mliowahi kwenda china au dubai kununua simu au vifaa vyaumeme naomba munieleweshe

1-Gharama zandege kwenda nakurudi

2-Nisehemu ipi nzuri kununulia mzigo kati dubai na china

3 -Kusafiri kutoka dsm hadi china au dubai huwa inachukua mda gani navipi hoteli zakule zabei yakawaida kwamfanya biashara mdogo anayeanza gharama zake zikoje

4 -Utaratibu wakusafilisha mzigo ukoje
Natangiza shukuran kwakuwa naamini mtanipatia maelekezo yakutosha namtanikumbusha na hata niliyoyasahau kwakuwa mimi itakuwa mara ya kwanza kabisa kifupi sijui chochote pia msisahau kuhusu huo mtaji ambao nahitaji kwenda nao itatosha kuanzia au inakuwaje
 
20m ndo uende Dubai au china?
au unataka kwenda kutembea?
simu aina gani? kama unanua smart phone za laki mbili 20 unanunua simu ngapi?
una duka atayari au ununue ndo uanze tembeza?

Binafsi naona tafuta biashara ingine hapa ya uhakika mtaji hata 15m

5m nenda Dubai katembee ujionee na ujifunze
15 M hata Kkoo kwa wauzaji wa jumla unaweza pata faida
 
Usikatishwe tamaa na ndugu zako hapo juu.hiyo 20mil ni pesa ndefu. Wengi wao wanakupigia masimu ya 200k ambayo Kwa ujumla soko lake wewe mwenyewe unalijua, Kwa hicho kiwango ni wastan wa USD 8600. Hata ukisema utenge pesa ya mzigo Tu USD 4500 itatosha kabisa kununua mzigo. Ukisema uchukue headphone, chaja, ni zile accessories nyingine Kwa usd 1000 Tu mzigo utaukimbia mwenyewe.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa mtaji ulionao unatosha kabisa hata kama ungekuwa na milioni 4 asije MTU yeyote akukubeza na mtaji wako, maana MTU ukimwambia unataka kuanzia biashara atakwambia uanze na bilioni mbili,ni wapuuzi watu hao wapuuzie
Mbona umeishia tu kutoa pongezi amna la maana uliloandika, kwani mtoa mada kasema ana shida na pongezi
 
benjamathayo, Kwanza hongera sana...

Ushauri wangu kwako ni kwamba ungepata agents au wakala mwamimifu wa huko dubai au china akununulie mzigo atume au kama unaweza kuagiza mtandaoni mfano alibaba wanauza simu za jumla kwa bei nzuri mnoo ila unapaswa kuwa makini

NB;mitandaoni napo si salama wahitaji umakini ukiagiza kwa mtandao maana utapeli wizi na vitu feki ni vingi

Pia maagents nao sio waaminifu mimi sifaham hili ila nilimuona faiza aly kule insta akitumia watu mizigo yao kutoka huko china
 
Kiongozi nenda china ndio uwakika. Na pia usikatishwe na hao GT P SALALY. Iyo ni pesa ndefu sana kwa kufanya bznes zako china.

Mm nilitishwa sana mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu kufata mzigo flani Dubai hatare mara kwa mtaji huo ni nauli na malazi tu mara kama unaenda kutembea sawa.

Ila baada ya kufika nilicheka sana mambo yako tofauti kabisa. Na kila mfanya bznes kama yangu nilie kutana nae na wazoefu uko Dubai wanasema mbona umekuja na kiasi kingi kwa bznes hii.

Tafta marifa sahihi kisha lianzishe mdau. Pambana tu kiongozi
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom