Nataka kwenda China kununua nguo na kuleta Dsm, Naombeni ushauri.

Mi nakushauri nenda nae ila inabidi kuwa mwangalifu,watu wanajali pesa siku izi sio utu.

Ondoa hofu kila kitu sa ivi ni kurisk,lasivyo utajikuta huna maendeleo kwa uoga.

Good luck

point. jamaa afanye utafiti wa kutosha na sio aende kisa ameona jirani yake kafanikiwa....... kila mtu ana siri yake ya mafanikio jamani tusifanye vitu kwa kufata mkumbo.
 
Kuwa makini unaweza bebeshwa sembe bila wewe kujua ukaishia kunyongwa
 
Heshima yenu wakubwa.
Wakubwa nina mil 10 ya kwenda kununua nguo china na kuja kuuza hapa mjini. Yupo rafiki yangu ambaye nyumba zetu zimepakana ameahidi kwenda na mimi na kunisadia huko China na mpaka tunarudi nitaweka nguo kwenye stoo yake palemwenge kwa muda na kuziuza kwa wateja wake hapa dsm ambao ni wateja wake wa zamani.

Huyu jamaa ni rafiki yangu sana hata watoto wake watatu wanakaa sana kwangu na mtoto wangu anachezna kwake.wanasoma shule moja. Sote tunaishi mbezi Tangi mbovu.

Yeye ni mfanyabiashara alianza na nguo akaja simu sasa yuko kwenye magari. Fedha zimemkubali. China anaenda mara mbili au tatu kwa mwezi. Anachukua vitu tofauti tofauti sana. Ana wateja wengi wa kila bidhaa.

Sasa naombeni ushauri wenu mtu ambaye watoto wetu ni marafiki, mimi na yeye na marafik, wake zetu ni marafiki nyumba zetu zimepakana na tuna miaka zaidi ya 6 kama majirani anaweza kunitapeli kweli? Au naombeni mnishauri risk ambazo zinaweza kunikuta ktk biashara hii. kwa wazoefu.Nimewahi kwenda nje ya bara la afrika lakini siyo kwa biashara. Asanteni kwa msaada wenu.

Duh, yaani huko koote tulikotoka na undugu wetu, leo unakuja kuhoji uaminifu wangu JF?!!
 
Kama kwenda china muende wote,ukajionee mwenyewe na ujue ujanja wao wanaotumia kupakia na kila ujanja wote!na huku uje ujue masoko yako wapi!na wanauzaje!kama wanakopesha wanakopeshanaje!
 
in Tanzania many businesses are actually not what you see on the surface. So, don't invest all your capital on one project like that China thing. Start with say 5m and grow up.
Remember: not all success you see around is from what appears on the surface.
 
Nakushauri nenda walau hata kwa kujifunza tuu na uende na kiasi kidogo cha huo mtaji uone mitaa yenye maduka ujue bei na gharama za ushuru afu badae ndo ufunguke rasmi
 
in Tanzania many businesses are actually not what you see on the surface. So, don't invest all your capital on one project like that China thing. Start with say 5m and grow up.
Remember: not all success you see around is from what appears on the surface.

nimekuelewa sana mkuu!kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia,japo hayanikatish tamaa
 
kaka angalia kwanza soko la kuuza hizo bidhaa zako baada ya kuzichukua kutoka china. risk kubwa iliyopo katika biashara ya nguo kutoka china ni kwamba wafanya biashara hizo ni wengi na unaweza kununua nguo halafu ukifika bongo unakuta tayari ni old fassion au zimeshajaa karikaooo kiasi ambacho kuziuza ni issue, hivyo fanya market survey kwanza, kama itawezekana ni bora mteja wako akupe sampo ya nguo anazohitaji na kiasi anachohitaji, kazi yako wewe iwe ni kuchukua tu nguo na kumletea.,nguo hasa za KINA MAMA, ZINA RISK HIYO. ila china kuna biashara nyingi sana ambazo unaweza kufanya mbali na nguo na simu, vipo vifaa vingi sana ambavyo huko kwetu hakuna na unaweza kuvileta huko na NAKUHAKIKISHIA WATEJA WAPO ni kiasi cha kujua NEEDS and WANTS za wateja wako pamoja na kuangalia PRICE, competition, na business position yako.
 
what a piece of advice from pangu pakavu

well done
 
Last edited by a moderator:
kwenda china kama umeamua kuingia kwenye biashara ni mhimu sana kama alivyo shauri muda hapo juu ili uweze kujua soko lilivyo lakini angalizo angalia usije ukabebeshwa sembe kama fidel alivyotahadhalisha mwezi mmoja uliopita alibebeshwa na akaandaliwa watu wa kumpekea yeye akajua ni ukarimu wa rafiki yake alipofika hong kong wakasubiri mpaka mtu anaekujakumpokea ndiyo wakawakama alikuwa analia kama mtoto mdogo
 
what a piece of advice from pangu pakavu

well done

Asante kaka, ila ni muhimu kuwapa tahadhari ndugu zetu wanaokuja huku, kiuzoefu wengi mitaji yao imekufa kwa kuwa na mawazo mgando ya kufanya biashara ya aina moja inayofanywa na kila mtu bila kuzingatia 4P's(Product,place,price and promotion) ya bidhaa wanazotaka kuzipeleka kwa wataja wao.Biashara si tu uambatane na mzoefu ila ni muhimu pia ku-consult wataalamu wa biashara kabla ya kuanza biashara,kitu ambacho watanzania wengi hatuna.
 
Heshima yenu wakubwa.
Wakubwa nina mil 10 ya kwenda kununua nguo china na kuja kuuza hapa mjini. Yupo rafiki yangu ambaye nyumba zetu zimepakana ameahidi kwenda na mimi na kunisadia huko China na mpaka tunarudi nitaweka nguo kwenye stoo yake palemwenge kwa muda na kuziuza kwa wateja wake hapa dsm ambao ni wateja wake wa zamani.

Huyu jamaa ni rafiki yangu sana hata watoto wake watatu wanakaa sana kwangu na mtoto wangu anachezna kwake.wanasoma shule moja. Sote tunaishi mbezi Tangi mbovu.

Yeye ni mfanyabiashara alianza na nguo akaja simu sasa yuko kwenye magari. Fedha zimemkubali. China anaenda mara mbili au tatu kwa mwezi. Anachukua vitu tofauti tofauti sana. Ana wateja wengi wa kila bidhaa.

Sasa naombeni ushauri wenu mtu ambaye watoto wetu ni marafiki, mimi na yeye na marafik, wake zetu ni marafiki nyumba zetu zimepakana na tuna miaka zaidi ya 6 kama majirani anaweza kunitapeli kweli? Au naombeni mnishauri risk ambazo zinaweza kunikuta ktk biashara hii. kwa wazoefu.Nimewahi kwenda nje ya bara la afrika lakini siyo kwa biashara. Asanteni kwa msaada wenu.

Hello Moriah ,umefikia wapi mwenzetu?Ni muda sasa umepita
 
kulikua na haja gani ya kumfungulia uzi mwenzako tena kwa kumdoubt atakutapeli? afterall ni kwamba una enda nae mguu kwa mguu atawezaje kukutapeli? have a "little faith" son!

God bless u na akupe mafanikio katika safari yako
 
Mwanzisha mada, aje atoe uzoefu wa safari + biashara. Mpaka sasa amefikia wapi?
 
Subiri JK akienda China. Honga ikulu uwekwe kwenye msafara. Kila kitu duty free airport. Msafara wa mkulu mara nyingi husheheno wafanyabiashara wa kariakoo hususan wamama
 
Nilivo iona Gwanzou huhitaji mtu we nenda hata pekee yako weusi wamejaa sana huko utajifunza mengi, afu wachina ni watu wa biashara ila chunga tu ufate ulichokusudia. jirani yako pia ni jirani ni lazima unamjua kama kweli anafanya biashara ya halali hawezi kuvunja ujirani kwa hiyo pesa yako.
 
Back
Top Bottom