Nataka kuwashtaki mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kuwashtaki mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, May 4, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwamba baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa miungu watu katika mikoa na wilaya zao kiasi kwamba wakati mwingine wamekuwa wanawalazimisha watendaji wao kama vile wahasibu kukiuka taratibu za fedha na hata kujiingiza katika maamuzi ambayo kimsingi hawana mamlaka ilimradi tu kukidhi matakwa yao kikazi au binafsi, nitataja baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakisikika yanafanywa na baadhi ya watendaji wa baadhi ya mikoa na wilaya kinyume na taratibu.

  1.Kutumia rasilimali za ofisi ya Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa wilaya kwa kutimiza shughuli za chama cha siasa, kama vile kujaza mafuta katika Magali ya ya Chama cha siasa katika shughuli za chama cha siasa, kutumia magari ya ofisi ya mkuu wa mkoa au wilaya kufanya shughuli za chama cha siasa.

  2.Mhasibu wa mkoa au wilaya kujipa jukumu la kukopa bidhaa au huduma kwa niaba ya serikali ili kuharakisha matakwa ya hawa wanaodaiwa kuwa miungu watu ambao wengi wao inaaminika hawajui taratibu za matumizi ya pesa za serikali. Kwa ufahamu wangu Mhasibu wa mkoa au wilaya hana mamlaka ya kukopa kwa niaba ya serikali. Na ukifuatilia karibia kila wilaya hufunga mwaka wake wa fedha ikiwa ina madeni ambayo yaliingiwa kwa niaba ya serikali na watu wasio na mamlaka ya kufanya hivyo.


  Naomba ushauri hapa kwa wataalamu wa sheria mimi kama mtu binafsi nikiwa na ushahidi wa kutosha wa gari la chama cha siasa kujaza mafuta kwa kutumia pesa zinazotoka ofisi ya mkuu wa wilaya, nifanye nini ili niweze kupeleka mashtaka mahakamani?
   
 2. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waulize mwanahalisi kuna kipindi wanadai waliliona gari la mkuu wa mkoa linafanya shughuli za chama cha siasa na walikuwa na ushahidi lakini walijiridhisha kwamba watashindwa tuu ndo maana waliishia kupiga kelele kama wewe, kigezo walichokitumia ni kwamba gari lilikuwa na private number lakini kwenye vioo lilikuwa ni STK. huu siyo ushahidi wa kushinda kesi angalia usije ukaumbuka. mara nyingi sana serikali huuza magari yake kuukuu kwa watu binafsi hivyo wananunuzi hubadiri namba za magari lakini hawaoni ulazima wa kubadiri mpaka vioo vya magari kisa eti vina STK, STJ nakadhalika, huo ni ushauru wangu usije kujikuta unajiingiza kwenye matatizo
   
Loading...