Nataka Kuwashitaki tiGO Msaada...

Eng Kimox Kimokole

JF-Expert Member
Jun 9, 2010
1,032
759
Wandugu nina tatizo kubwa sana hapa.

Mimi ninamiliki line ya tiGO toka 2009

Mwezi wa 10 nilipokea msg kwenye simu yangu ikisema "Mr. 714507507, Your service class changed from Tigo PPS to ConVen1, and the new service class effects on 2012-10-12"

Sasa baada ya ujumbe huo nikaanza kuona mabadiliko ya kimatumizi kwenye simu yangu. Leo nimekwenda tigo kuuliza badiliko hilo la Service wakaniuliza namba yangu na jina langu kamili, nikataja wakaniambia: "HII LINE SIO YA KWAKO" mmiliki wa hii line ni TANZANIA STANDARD (N) LTD toka tarehe hiyo tajwa kwenye msg.

Kiukweli niligombana na Customer Care kwa kuuliza kwa nini tiGO wamebadilisha umiliki wa line yangu kutoka kwangu kwenda kwa Kampuni bila kushirikishwa. Walipoangalia usajili wa tiGO Pesa ni kwa jina langu lakini Line ni kwa jina la hiyo Kampuni. Na usajili wa jina kwenye tiGO pesa ni wa zamani kuliko huo wa Kampuni. Nikawaambia warudishe umiliki huu kwenye Jina la awali wakakataa mpaka nipeleke kwao Barua ya Kampuni ili kubadirisha.

Sasa Wandugu nahitaji msaada hapa wa Kisheria na wanasheria wachangamkie deal hii tuwashitaki tiGO kwa kubadilisha umiliki halali wa line yangu bila ridhaa yangu mimi hivyo kufanya TAARIFA ZANGU ZOTE KUWA MALI YA KAMPUNI na wanayo mamlaka juu ya line ambayo toka awali haikuwa yao.

Naombeni msaada hapa.
 
Wazo Zuri la kuwshitaki Tigo wamevunja mkataba na wewe itabidi wakulipe Fidia hapo. Ninakushauri itabidi upate Mwanasheria akusaidia hiyo Deal na upate Advocate ili akupangie kesi ya madai na yeye huyo Advocate atakuambia ni jinsi gani utakavyo funguwa kesi yako ya Fidia utapatadonge nono hapo mkuu.@Kimox Kimokole
 
Kwani hii line haukuitumia kwa muda mrefu?mie pia line yangu ya airtel aligawiwa mtu mwingine na nilipouliza kulikoni walidai kwa kuwa sikuitumia siku nyingi..
Zion Daughter hii line haijawahi kuwa offline hata kwa lisaa limoja, siku zote iko ON. Mimi nafanya kazi kwenye hiyo Kampuni, na kampuni huwa ina utaratibu wa kutuwekea salio la tigo kila mwezi sasa kwa nini wabadilishe usajili wa line yaku kutoka kwangu kwenda kwa kampuni bila kunitaarifu, weka akilini kuwa nimekuwa na hii line kabla sijaja kwenye hii kampuni wala kupokea pesa zao
 
Last edited by a moderator:
Wazo Zuri la kuwshitaki Tigo wamevunja mkataba na wewe itabidi wakulipe Fidia hapo. Ninakushauri itabidi upate Mwanasheria akusaidia hiyo Deal na upate Advocate ili akupangie kesi ya madai na yeye huyo Advocate atakuambia ni jinsi gani utakavyo funguwa kesi yako ya Fidia utapatadonge nono hapo mkuu.@Kimox Kimokole

Nahitaji msaada wa Advocate hapa
 
Kinachoniudhi tigo ni kwamba wanapokea pesa zetu halafu wantoa sub standard mwanzo ilikuwa kwa kampuni moja Inaitwa Infinity sasa tatizo la Infinity ni kwamba wanaogopa kulipa watu mishahara kutokana na taaluma. Wanaenda kutafuta watu waliosomea computer corse na kuwapa kibarua matokeo yake wanavuruga kila kitu kwa watej wa tigo. Ndugu yangu huyo wakili mwenyewe akifika Tigo atapewa rushwa na kukusahau kabisa
Pole my Brother
 
Zion Daughter hii line haijawahi kuwa offline hata kwa lisaa limoja, siku zote iko ON. Mimi nafanya kazi kwenye hiyo Kampuni, na kampuni huwa ina utaratibu wa kutuwekea salio la tigo kila mwezi sasa kwa nini wabadilishe usajili wa line yaku kutoka kwangu kwenda kwa kampuni bila kunitaarifu, weka akilini kuwa nimekuwa na hii line kabla sijaja kwenye hii kampuni wala kupokea pesa zao
Washitaki....mie sio loya...Ngoja waje wakushauri..Kuna mmoja anaitwa somebody Ruttashobolwa yupo kule CC...labda anaweza kukusaidia
 
Last edited by a moderator:
Kinachoniudhi tigo ni kwamba wanapokea pesa zetu halafu wantoa sub standard mwanzo ilikuwa kwa kampuni moja Inaitwa Infinity sasa tatizo la Infinity ni kwamba wanaogopa kulipa watu mishahara kutokana na taaluma. Wanaenda kutafuta watu waliosomea computer corse na kuwapa kibarua matokeo yake wanavuruga kila kitu kwa watej wa tigo. Ndugu yangu huyo wakili mwenyewe akifika Tigo atapewa rushwa na kukusahau kabisa
Pole my Brother

Kwa hiyo unaniambiaje? Niache mtu mwingine awe anapata information zangu zote?
 
mtafute mwanasheria hapo dar ulipo
atawaandikia demand notice ya kukurudishia no. yako ndani ya siku 7 na fidia juu
wanasheria wanaelewa how to draft such letter
after 7 days kama hawajarudisha atafungua madai yako mahakama ya wilaya au mkoa kwa hakimu mkazi under certificate of urgency
since no yako ina watu wengi ataeleza na hasara unazopata kwa kukosa mawasiliano na kudai damage kubwa
na other reliefs deemed necessary as court may think so.

grounds to be relied on
breach of contract btn you and tigo.
breach of privacy policy btn you and the company
since hiyo no ni personal na unahaki zote
kukosa mawasiliano nayo ni foreseen loses both economically and socially
pia Tigo wako against na sheria za mawasiliano kwa walilokufanyia.
andaa doc za usajili wa number yako
nk.
hapo patamu kwa mwanasheria makini na hakimu makini hapo hamtakosa 70M au zaidi.
itakuwa fundisho kwa makampuni mengine yenye tabia kama hizo
kila la kheri katika kudai haki yako
KIMOKSI FANYA HIMA KESHO WAKUANDIKIE MAPEMA NA UWA SERVE TIGO KESHO HIYO HIYO
 
ndugu Dr F. Ndugulile nakuona hapo chini, msaada wako tafadhali

Mh. Dr F. Ndugulile
Mkuu Kimox Kimokole Mkuu.@Mh. Dr F. Ndugulile si Mwanasheria yeye ni Mbunge

wetu kule kigamboni tunangojea Daraja la kigamboni je Serikali watalijenga mpaka ikifika mwaka 2015

tutamuuliza
Mh. Dr F. Ndugulile Daraja la kigamboni limefikia wapi? Au ndio ahadi hewa za Serikali? Au ndio tutakula nyasi au kupiga mbizi? Mkuu

Kimokole tafuta Wana sheria wamo humuhumu ndani wanakusikia lakini hawakujibu ukipata Msamaria mwema

mwanasheria mmoja atakusaidia tu tatizo lako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom