Nataka kuwa mjasiriamali mkubwa mwenye mafanikio makubwa

lumanija1990

Member
Jan 6, 2016
16
10
Jamani habari mana jf

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoliki mwenge kilichoppo Moshi nina chukua education (economics and geography). Kwanza kabisa mwaka wa 2014 nilikuwa UDOM nikichukua bachelor of business admistration, nilisitisha kozi kwa sabaabu sikuwa ma mkopo na maisha yakawa magumu kidogo. Baada ya kutoka UDOM nilitimkia Mpanda kuchukua mashamba ya mpunga nilikodi hekari mbili na nusu, nililima vizuri nizitunza vizuri, mwisho wa siku nikavuna nikapata gunia 56. niliamua nianzishe duka la nafaka kuzingatia kipindi hicho niliamua kupiga chini kusoma, na sikuwa na wazo kabisa la kuendelea masomo. kutokana na ushauri wa watu mitaani, wazazi, na watu wangu wa karibu niliamua kwenda chuoni, kwa hiyo nikaa kuapply hapa mwaka jana 2015 chuoni nikaachana na BBA nikakimbilia Education kwa sasa niko mwaka wa kwanza.
kwasasa bado naendelea na kilimo kule Mpanda-Katavi nilikodi hekari tatu ambazo nategemea kila hekari gunia 25, kwa hekari tatu ni gunia 75, niategemea million Tsh 4500000/= na ninatunza kamkopo kidogo, lakini nina ekari mbili za mpunga ekari moja ya choroko ambazo zinasimamiwa na wazazi huko kwimba-Mwanza(nyumbani). Ndugu zangu wana jf ninatamani kuwa na duka la nafaka hapa Moshi mijini, huku nikiendelea na kilimo changu cha mpunga huko katavi, sasa nlikuw nahitaji ushauri wenu ukizingati bado ninaendelea na masomo, je huu uamuzi wangu uko sahihi, jinsi ya kukuza mtaji wangu, nina imani ya kuwa mwanaviwanda(industrialist) wa viwanda vya kusindika mazao na kudiversify biashara yangu ushauri jinsi ya kufikia malengo yangu.

karibuni kwa michago yenye tija.
 
Thread hii ilikua nzuri sana sijui kwa nini haikupata wachangiaji, mkuu lumanija1990 ulifanikiwa ndugu yangu? nimependa mpango wako huu kama ungeufanyia kazi hakika ungefanikiwa sana. nakupa heko mr.
 
Acha chuo, ujikite kwenye mirdi yako kama unataka kuwa mjasiliamali mkubwa. Tatizo huna uhakika na ndoto yako ya Ujasiliamali ndio maana umerudi chuo.
 
Mkuu huu ndio muda muafaka wa kukamilisha ndoto yako.
Nshu ya njaa ifanye kama fursa kwako make si unaona wengi tumebweteka tu tukisubili chakula cha msaada.
Kodi maeneo makubwa zaidi na lima sana ili mavuno yawe mengi na bila shaka utatuuzia kwa bei kubwa zaidi maana watu si tunadai eti mtaani chakula hakuna.
chukulia hali ya uhaba wa chakula kama fursa kwako na nna imani utatimiza ndoto yako.
 
Jamani habari mana jf

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoliki mwenge kilichoppo Moshi nina chukua education (economics and geography). Kwanza kabisa mwaka wa 2014 nilikuwa UDOM nikichukua bachelor of business admistration, nilisitisha kozi kwa sabaabu sikuwa ma mkopo na maisha yakawa magumu kidogo. Baada ya kutoka UDOM nilitimkia Mpanda kuchukua mashamba ya mpunga nilikodi hekari mbili na nusu, nililima vizuri nizitunza vizuri, mwisho wa siku nikavuna nikapata gunia 56. niliamua nianzishe duka la nafaka kuzingatia kipindi hicho niliamua kupiga chini kusoma, na sikuwa na wazo kabisa la kuendelea masomo. kutokana na ushauri wa watu mitaani, wazazi, na watu wangu wa karibu niliamua kwenda chuoni, kwa hiyo nikaa kuapply hapa mwaka jana 2015 chuoni nikaachana na BBA nikakimbilia Education kwa sasa niko mwaka wa kwanza.
kwasasa bado naendelea na kilimo kule Mpanda-Katavi nilikodi hekari tatu ambazo nategemea kila hekari gunia 25, kwa hekari tatu ni gunia 75, niategemea million Tsh 4500000/= na ninatunza kamkopo kidogo, lakini nina ekari mbili za mpunga ekari moja ya choroko ambazo zinasimamiwa na wazazi huko kwimba-Mwanza(nyumbani). Ndugu zangu wana jf ninatamani kuwa na duka la nafaka hapa Moshi mijini, huku nikiendelea na kilimo changu cha mpunga huko katavi, sasa nlikuw nahitaji ushauri wenu ukizingati bado ninaendelea na masomo, je huu uamuzi wangu uko sahihi, jinsi ya kukuza mtaji wangu, nina imani ya kuwa mwanaviwanda(industrialist) wa viwanda vya kusindika mazao na kudiversify biashara yangu ushauri jinsi ya kufikia malengo yangu.

karibuni kwa michago yenye tija.
Yani wasomi wangekua kama wewe taifa lingeshapiga hatua,kwa mawazo hayo hata hapo shuleni unaweza kua unapoteza muda japo sikushauli kuacha masomo,maana ukichukua hayo mawazo ukajumlisha na bidii utafanikiwa sana kimaisha
 
Kama mwanzo uliweza sasa hivi kwa nini uwe na wasi wasi? Ukiweka bidii hakuna linaloshindikana hasa kwa wakati huu ukiwa bado na nguvu za kutosha!
 
My Simple Advice

You Have An Idea, Sets Your Goals and Write Them Down, Be Prepared For Work Hard and Long Hours and Lastly Be Smart

Don't Take Advice From People Cheaply, Business People Take Advice From KPI's, Who Made It Successful

All In All You Can Do Both Kusoma Na Biashara.

All The Best & Wish You Good Luck
 
Back
Top Bottom