Nataka kuwa Afisa Upelelezi wa kituo cha Polisi, je nikajieleze kwa Mkuu wa Kituo?

ukienda ccp ukitoka utaishia kuinda benki,watu wangu wanakufa kwa kukosa maarifa ,kuna provate firm kibao za mambo ya kipelelezi kama vipi fungua yako au omba ajira huko,kwa msaada mtafute IGP mtaafu maundi pale clocktower ana kampuni ya dizaini hiyo,angalizo we waweza kuta hauna element za mpelelezi bali mbea

Ahahahaaaa apo mwisho ndo uliponichekesha kuwa anaweza kuwa na element za umbeya na sio mpelelez
 
Shortcut zinaumiza hizo.Chamsingi Fanya application za jeshi LA polisi ili uende course then utaifikia hiyo ndoto yako
 
Haiwezekani mwenzako asote na mabio ya kupanda mlima wa Mr. Price kwa miezi kadhaa wewe utoke tu kwenu na mbwembwe nyingi za kufanya kazi ambayo hutaki kuingia gharama ya kuipata...mkuu wa kituo hatoi ajira iwe kwa raia au kwa mgambo bila utaratibu kufuatwa na kama ingekuwa hivyo basi jeshi la polisi au lolote lile lisingekuwa na maana ya kuitwa jeshi. jiulize kwa nini hadi mtu mwenye elimu kubwa tu ya digrii au master lazima aende depo...NENDA DEPO UKAKATE MAGEUKO NA MBIO ZA KUTOSHA ILI HAO UNAOTAKA KUWAPELELEZA WAKIKUSHTUKIA UWE TAYARI KWA LOLOTE.

Nyie wapenda mtelemko, someni hii coment na kuielewa vema kisha Mjipange sasa!!!
 
Mtoa mada upo km mm,
Incase ukpata njia mbadala zaid ya ccp tujuzane mkuu..
Upelelez wa kisasa na ccp vtu vwili tofaut ... Sema kbonhobongo cdhan km inaeleweka..
Some stay in da office,some perform in the field...#teamWork
Mkuu pamoja na yule wenzio, napenda mfahamu kwa ndoto yenu hio CCP is a must, lazima utie mguu.

Hivi utafanyaje upelelezi wako bila kufahamu ethics zake? Naomba nikuulize hivi inatokea upo kazi maalumu na kwa bahati mbaya unakutana na wapelelezi wenzio na hamfahamiani unategemea nguo yako ya ndani itachafuka tu kwa uoga.
 
Hizi muvi za kizungu zinawadanganya sana vijana, hivi unafikiri huko polisi kuna upelelezi gani wangelikuwa majambazi na wauza ngada wangetamba, kijana Subiri ukue uijue dunia na punguza kuangalia hizo movies.
 
Ndio maana mzee mmoja mwenye hekima alisema kipaumbele chetu ni elimu, elimu, elimu.....
nashangaa kuona graduate anaweza Mambo yamovie za western..
 
Acheni kuangalia hizi movie za wazungu jamani zinawaharibu...sijui ulikuwa unafatilia HAWAII-FIVE O au CIA INTELLIGENCE?!Hebu niambie ni season gani ulikuwa unaingalia wewe kijana?!
 
Nenda ccp ukafundishe vitu na jinsi ya kijihami utakapogundulika ujihami,

Unafikiri ccp ni mapambo utamalizwa mapema sana bila hayo makozi ya huko.
 
Wadau,

Mimi nimesomea fani ya ICT na nimeajiriwa lakini nina element za upelelezi na ufuatiliaji tangu ukuaji wangu. Nina motivation ya kuwa part ya Jeshi la Polisi kama Afisa Upelelezi lakini sijiskii kwenda Chuo cha Uaskari kwa miaka ingine kadhaa. Je, ni hatua zipi nifuate nifikie hii ndoto?

Ninapoishi kuna kituo cha polisi ambacho huwa natamani ningekuwa pale hata kuwasaidia kwa chochote. Nilifikiria kumface Mkuu wa Kituo na kumweleza lakini sijui kama ni sahihi.

Napenda maisha ya kumtrack mtu, shughuli za kiintelijensia na kujichanganya maeneo nikiwa kama mtu was kawaida kumbe ni Mpelezi.

Nifanyeje? nianzie wapi? Kuna uwezekano wa ku-jumpstart?
Unaanza aje kufuatilia mtu, ili ujue nini kumhusu yeye? Nchi nyingi watu kama wewe huitwa stalker na kuna sheria ukigundulika unaweza kufungwa. Haiwi kipaji ila ni kutojitambua fulani na kujikuta unataka kumfuatia mtu kwa kila anachofanya.
 
kuna njia nyingi za kutaka kutambua kati yetu nani niwamajeshi au polisi na nani raia nadhani nimeeleweka ila kwa post hizi jf ina askari wengi.
 
Back
Top Bottom