Nataka kuvuna maji ya mvua, nitumie dawa gani yasiharibike?

kitotoro

Member
Jan 5, 2014
22
5
Wadau msaada nataka kuvuna Maji ya mvua ila nasikia yanaharibika mapema bila kuweka dawa, kama kuna mtu anajua dawa naomba anifahamishe.
 
yajengee mfuniko imara,mwanga usipenye,yatakaa hadi mwaka

Na mimi nasigiaga hii ndo dawa yake. Ila mkuu kusipokuwa hata na sehemu ya kupumulia si kisima chaweza pata nyufa kikavuja? sababu ya lile fukuto la shimoni?
 
na mimi nasigiaga hii ndo dawa yake. Ila mkuu kusipokuwa hata na sehemu ya kupumulia si kisima chaweza pata nyufa kikavuja? sababu ya lile fukuto la shimoni?

Breather na overflow pipes ziwekee elbow....

Navuna maji ya mvua mwaka wa 3 Dawasco nawasikia tu...nikisikia wanauza maji sh 500 kwa ndoo nadhani matapeli.

Jaribu na utafurahia...
 
Unaweza tumia water guard ipo na calcium hypochloride nadhan ni nzuri sana unaweka kila baada ya mwezi mmoja

Application yake ikoje maana kimo cha maji kina panda na kushuka kutegemea na wingi ama ukosefu wa mvua
 
Breather na overflow pipes ziwekee elbow....
Navuna maji ya mvua mwaka wa 3 Dawasco nawasikia tu...nikisikia wanauza maji sh 500 kwa ndoo nadhani matapeli.

Jaribu na utafurahia...

Mkuu hongera, vipi unavunia kwenye kisima cha ukubwa gani mkuu, manake najaribu kupata picha kama Dawasco huwatumii kabisa!!
 
kisima cha chini kinatunza 62500lts...nayapandisha kwenye Simtank 2@10000lts...nikijaza nakuwa na 82500lts

Wastani natumia 200 - 300lts kwa siku sawa na wastani wa siku 275.
Mvua zilizonyesha hapa kati zimejaza tayari, kwa hiyo tusipopata mvua kwa kipindi cha zaidi ya nusu mwaka bado sina hofu.

Kipindi cha mvua tunahakikisha Simtanks zimejaa kila siku ili kuruhusu kisima kipokee mzigo
 
Gharama za ujenzi wa kisima chako umetumia kiasi gani mkuu? Cz na mm nataka niwe natumia njia hii.
 
kisima cha chini kinatunza 62500lts...nayapandisha kwenye Simtank 2@10000lts...nikijaza nakuwa na 82500lts

Wastani natumia 200 - 300lts kwa siku sawa na wastani wa siku 275.
Mvua zilizonyesha hapa kati zimejaza tayari, kwa hiyo tusipopata mvua kwa kipindi cha zaidi ya nusu mwaka bado sina hofu.

Kipindi cha mvua tunahakikisha Simtanks zimejaa kila siku ili kuruhusu kisima kipokee mzigo

Mkuu bila Shaka umekichimba chini

Unaweza kunisaidia dimensions zake maana nami ni jambo niliotalo kufanya ninakojenga maana maji ni changamoto na nategemea kuishi kwa Maji ya kuvuna kwa mvua

Will appreciate
 
kisima cha chini kinatunza 62500ltss...nayapandisha kwenye Simtank 2@10000lts...nikijaza nakuwa na 82500lts

Wastani natumia 200 - 300lts kwa siku sawa na wastani wa siku 275.
Mvua zilizonyesha hapa kati zimejaza tayari, kwa hiyo tusipopata mvua kwa kipindi cha zaidi ya nusu mwaka bado sina hofu.

Kipindi cha mvua tunahakikisha Simtanks zimejaa kila siku ili kuruhusu kisima kipokee mzigo
Hii kitu ya kuvuna na kuhifadhi maji watu wengi hawaijui,au wanajua lakini wanapuuzia. Ninavuna maji ya mvua na kuhifadhi lita 50000. Kwa wastani familia huwa inatumia lita 150 kwa siku. Ukipiga mahesabu utaona ni muda gani sinunui maji wala dawasco hatusalimiani. Na hapo ikinyesha tena katikati,mambo yanakua murua zaidi!
 
hii njia Egypt
wanaitumia sana
 
kisima cha chini kinatunza 62500lts...nayapandisha kwenye Simtank 2@10000lts...nikijaza nakuwa na 82500lts

Wastani natumia 200 - 300lts kwa siku sawa na wastani wa siku 275.
Mvua zilizonyesha hapa kati zimejaza tayari, kwa hiyo tusipopata mvua kwa kipindi cha zaidi ya nusu mwaka bado sina hofu.

Kipindi cha mvua tunahakikisha Simtanks zimejaa kila siku ili kuruhusu kisima kipokee mzigo

Again hongera sana mkuu, umeinvest kwenye maji si mchezo, hizo tu Simtank 2 za lita elfu10 ni parefu sana, hapo bado hicho kisima cha chini khaa!! Hata hivyo inaonekana paa la nyumba lako ni kubwa so unakusanya maji ya kutosha hata kama mvua ni za muda mfupi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom