Nataka kuvuka Nina mbuzi, chui na majani nianze na kipi? Kisipotee chochote

1.Anza na mbuzi & majani ukishavuka yaache majani rudi na mbuzi....(ukimuacha nyuma chui atamfanya kitoweo]
2.vuka na chui ukifika muache huko hawez kula majani
3.vuka na mbuzi...mchezo kwisha
Kurudi na mbuzi tena mkuu Kuna mzunguko apo
 
mvushe chui, kisha nenda kachukue majani uyavushe yatakuwa salama kwa sababu chui hali majani, kisha kamvushe mbuzi.
 
Anza na Mbuzi mvushe hadi ng'ambo. Then beba Majani nenda nayo. Ukifika rudi na mbuzi acha Majani then beba chui nenda nae ukifika unarudi kumfata mbuzi wako. Hivyo tu
Hili ndio jibu. Amvushe mbuzi kwanza kwa sbb chui hali majani
 
Umekosea swali. . Na si majani tu, bali ni majani ya mbegu unatakiwa uyafikishe ukapande, kwa hiyo hakikisha unayalinda. Malizia kwamba mtumbwi wako unakubeba wewe na mzigo mmoja tu .Ukizidisha unazama.

Ambapo jibu lake ni hili.

Awamu ya kwanza, Nenda na mbuzi, muache huyo chui wako na majani.

Kamuache huyo mbuzi ng'ambo urudi tena. Safari hii uchukue, majani yako ya mbegu nenda nayo hadi ng'ambo aliko mbuzi.

Ukifikisha majani, yaweke majani umchukue mbuzi, urudi naye hadi aliko huyo chui wako.

Ukifika aliko chui, mwache mbuzi kule, beba fisi umpeleke ulioyaacha majani. Ukifika kule mwache fisi na majani.

Mara ya mwiso rudi kamchukue mbuzi wako mvushe, akaungane na chui wako, na majani yako ya mbegu, then endelea na safari.

Nipe zawadi.
Umeelezea vizuri ila huyo fisi katokea majini au?
 
mnataka tujifanye kua chui hali binadamu anakula tu mbuzi? hehe acheni utani.
Kama una chui basi lazima atakua kafungiwa ndani ya cage.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom