Nataka kutoka CWT. Je, Kuna chama gani kingine cha waalimu?

KAKSIGABA

Member
Oct 24, 2015
17
8
Wakuu kwema?

Nataka Kahama chama cha waalimu Tanzania (CWT) Je, Kuna vyama gani vingine mbadala tofauti na CWT? Kama Kuna mtu anavifahamu naomba anipe na mawasiliano ya Viongozi wa hivyo vyama.
 
Kwa nini unataka kuhama mkuu?

Vuta subira watakuja kukupa muongozo
 
1. Unaruhusiwa kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

2. Siyo lazima chama hicho kiwe na neno "Walimu" kwenye jina lake.

3. Unaweza kuamua kuendelea na utumishi pasipo kuwapo kwenye chama chochote kile cha wafanyakazi.
Mkuu Naomba na vifungu vya sheria hasa ambayo hainibani mimi kujiunga na chama cha wafanyakazi
 
Mkuu Naomba na vifungu vya sheria hasa ambayo hainibani mimi kujiunga na chama cha wafanyakazi

Kujiunga na chama cha wafanyakazi ni hiyari.
Hata wao wanajua hawatakiwi kumlazimisha mtu kujiunga kwenye chama.

Sheria ya vyama vya wafanyakazi ina sisistiza kujiunga uanachama ni HIYARI.

Mimi sipo kwenye chama chochote cha wafanyakazi. Kwa yanayoendelea, hawawezi nishawishi kujiunga.
 
Mimi sikutaka kabisa kujiunga na chama chochote na wala hatukujadiliana nao kuhusu hilo lakini kila Mwezi wananikata asilimia mbili ya Mshahara wangu!

Nikimwendea mwajiri ananiambia trade union ni lazima inikate makato hayo kwa kuwa mimi nanufaika na kazi zinazofanywa na hiyo Trade union
 
Back
Top Bottom