Nataka kusomea urubani wa ndege, niende chuo gani Tanzania?

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,553
32,178
Wakuu nahitaji kusomea urubani niwe rubani maana nikiwacheki ile mijamaa inavyodunda pale uwanja wa ndege utafikri dunia yote yao.

Tafdhali mwenye kujua chuo cha Urubani wa Ndege (sio Ungo) anijuze ni-apply.
 
Nimeona mara kadhaa coastal aviation wakiwa na wanafunzi wa urubani. Sijui kama wnaaanzia kwao ama wanakuwa wanawapiga brush tu.

I should warn you though, fee yake ndefu! Angalia web yao uwapigie wakupe muongozo.
 
Wengi wamesoma nje ya Tanzania,halafu wanakuja hapa nchini kupata mazoezi kwa vitendo!

South Africa,USA ,CANADA! Sina uhakika kama bado SOROTI iko bomba kama zamani!!
 
Bongo saund jomba...hakuna chuo cha urubani. The nearest u can go ni Kenya...au Uganda-Soroti kama bado hakijawa gofu, maana kile kilikuwa mali ya EAC ya enzi hizo za Mwalimu.

Kama ulivyogusiwa na mdau hapo juu, hakikisha baba yako ni Fisadi, maana mazoezi yote ya field (guided na solo) ni lazima yalipiwe ili wese la ndege lipatikane...hapo ndipo gharama kubwa inapozaliwa.

Lakini pia hakikisha kichwa chako kiko sawa- yaani huchanganyikiwa ovyo, maana mazoezi yake ni kimbembe.
 
ninakutafuta kutaka kujua zaidi
 
Kaka hapo Egerton University, Kenya wanatoa Mafunzo ya Awali ya urubani.

Lakini wasi wasi wangu kama unasom,ea urubani ili uje kufanya kazi wapi? maana kama ni bongo sahau tuna ndege moja mpaka sasa
 
Sitofautiani na wachangiaji, Taaluma ya Urubani inakaugumu fulani na inachukua muda mrefu sana (Theories/Practicals), Hadi uwe rubani kamaili ni kazikwelikweli na gharama yake ni kubwa mno.

Halafu future yake kwa TZ ni msala!
 
Je umesoma PGM na kufaulu vizuri?

if YES

Nenda JWTZ.Utafanikiwa!Kila la kheri!
 
Tunakutakia Mafanikio Mema Endapo utapata nafasi Tanzania ya 2015 itawahitaji sana nyie....
 
Mkuu waweza ukaenda pale JKIA terminal1 kipo kinaitwa reginal aviation colledge but huwa wanatoa leseni ya ppl(private pilot licence) na arusha nasikia vipo ila sina full info
 
Mkuu waweza ukaenda pale JKIA terminal1 kipo kinaitwa reginal aviation colledge but huwa wanatoa leseni ya ppl(private pilot licence) na arusha nasikia vipo ila sina full info

vipi kunauwezekano wa kuanza na ngazi ya cheti? Mdogo wangu anataka aanze na ngazi ya cheti ilikuwa na msingi mzuri
 
Back
Top Bottom