Nataka kusoma masters; Je ni kozi gani itanisaidia kupata ajira kwa urahisi nikiisomea?

G 4real

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
449
250
Nimesomea degree ya ualimu nikapata gpa ya 3.0 "lower second" kwa masomo ya kiswahili na political science.
Kutokana na hali ngumu ya ajira nimeona niendelee na masomo ya masters.
Je ni kozi gani itanisaidia kupata ajira kwa urahisi nikiisomea?
 

kabunda88

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
2,666
2,000
ajira hamna bd watu wanataka kusoma kwa lengo la kuajiriwa ni wakat wa kubadil mtazamo sasa
nakushaur jiajir kwanza thn ukiwa vizur jiendeleze
 

G 4real

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
449
250
ajira hamna bd watu wanataka kusoma kwa lengo la kuajiriwa ni wakat wa kubadil mtazamo sasa
nakushaur jiajir kwanza thn ukiwa vizur jiendeleze
Mkuu mawazo yako ni mazuri ila naomba tu assume niko vizuri unanishauri nisomee Kitu gani ili kukabiriana na changamoto iliyopo
 

kabunda88

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
2,666
2,000
Mkuu mawazo yako ni mazuri ila naomba tu assume niko vizuri unanishauri nisomee Kitu gani ili kukabiriana na changamoto iliyopo
uwalimu na profession za afya mfno Dr,Nursing etc ndio zilikuwa kipaumbele cha Serikal kuajir sasa hawaajir kipind hik may be baadae endelea kusoma masters ya ualimu serikal ikitoa ajira utapata na kupanda daraja ni rahis kuwa mkuu wa shule kwaelim yako hiyo ni plan ya baadae ila kwa sasa km huna ajira jiajir tu
 

xungura

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
279
250
Mkuuu tafuta kazi yoyote angalau iwe experienced work then ukasome masters maaana soko la ajira la sasa hivi bila work experience ni sawa na bure tu
Cc waziri Wa viwanda.
 

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,346
2,000
Huo mda na pesa ya master jarbu kuwekeza kwenye kilimo kwa njia yoyote ile then urudi kuleta feedback
 

ngomeu

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
326
250
Mbona mnamkatisha mwenzenu tamaa,ye kajipanga kuchukua masters na we unamuambia anapoteza mda awekeze kwenye kilimo?
 

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
2,207
2,000
Mbona mnamkatisha mwenzenu tamaa,ye kajipanga kuchukua masters na we unamuambia anapoteza mda awekeze kwenye kilimo?
Kweli..mana yeye sio mtoto mdogo..anajua anachotaka kukifanya..ndio mana kaomba ushauri juu ya hilo suala.
 

Chachata

Senior Member
Apr 29, 2011
195
250
Masters inaendana na background yako kwa mana ya ya undergraduate ulisoma nini, uli umaste vitu hapo utasoma MA kiswahili,au MA zote zinazoendana na societies kama MA community Devpnt, au political science kama ya polepole .sasa kuhusu ajira kwanza hakuna na ni mtazamo wa kizamani sana kusoma ili upate ajira
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,964
2,000
hela ya masters ifanye mtaji ndugu... zama za ajira za kuajiriwa zimeisha.. hizi ni zama za ajira yako mwenyewe... utafanya masters yako wahindi watakuajiri wakupe laki 2 tu na manyanyaso kibao.. unabaki unatoa macho tu
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
10,756
2,000
Kasome monitoring and evaluation. Bongo wanajitajika sana Hao watu wako wachache sana haswa serikarini. Fanya uchunguzi utaniambia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom