Nataka kusema kitu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kusema kitu !

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bikra, Jun 1, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 1, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nataka kusema kitu, bado nakifikiria,
  Nifikiri mara tatu, kisha nitawaambia,
  Ninachotaka kusema.

  Nimepatwa na ufyatu, mambo yamenizidia,
  Msiotwe roho kutu, mwapaswa nisaidia,
  Kuna kitu ntasema.

  Miaka makumi tatu, mie naikaribia,
  Nami kati yao watu, heshima naitakia,
  Mwaelewa nachosema?

  Na huu siyo upatu, nikaukurupukia,
  Nitawashangaza watu, ovyo kujiamulia,
  Niendelee kusema?

  Moyo wangu siyo butu, pekee kujikalia,
  Nao wahitaji kitu, kesho nitawaambia,
  Basi kesho ntasema.

  Au Niseme Leo ? Umefahamu nitakacho ?
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...duh!

  Mzee Mwanakijiji njooooooooo!!! lugha hii mwenyewe MM tu...
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Vipi na wewe ni Bubu ataka kusema? ha ha ha ha All the best just spit it out :)
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Sema leo,
  kesho haiji!
   
 5. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sema dada mpenzi
  usijikatili
  Usisubiri enzi
  hairudii
  Chungwa kugeuka danzi
  Unajidhili!

  Paaza sauti hata nyikani
  Kunako miti hata manyani
  Simba akikosa hula majani

  Ngoja ngoja huumiza tumbo
  Subiri kesho upigwe kumbo
  We jivute na hayo mafumbo
  Wenzio hawajivungi!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe hapo juu hio ndo nini?..lol
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  bado hujapata mtu, moyo wako kumpatia,
  akupe na wake utu, nawe kumstamilia,
  ipo nafasi adhimu moyo wako kuuweka.

  wapo vijana waseja, wanatafuta wema wenza
  tena wapo wakuja, na wenyeji wa kukutunza
  ipo nafasi adhimu moyo wako kuuweka.

  kama waweza subiri, tena kwa mwaka mmoja,
  Yoyo kaweka nadhiri, mwakani kufunga hoja,
  ipo nafasi adhimu moyo wako kuuweka.

  kuna vijana hadaa, hao kuwa nao mbali,
  wao hawataki ndoa, mfano huyu fideli,
  ipo nafasi adhimu moyo wako kuuweka.

  ni bora ukatulia, ubaki na yako bikira,
  utamnasa kitia, mume alo kuwa bora,
  ipo nafasi adhimu moyo wako kuuweka.

  ila nakupa hadhari, ni vijana wala tigo,
  vijana hawa hatari, wakija wape kipigo,
  moyo wako kuuweka usije mpa masanilo.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  this is SERIOUS!
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sema leo mwali kama ni arusi tujiandae kupokea posa ati
   
 10. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  hahahahahahahaha historia inakuhukumu mkuu masanilo
   
 11. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Burn kumbe na weye bingwa heeeh!........mbona umemsahau bro Fidel tena?
   
 12. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bikra,
  Sema tunakusikiliza.
   
 13. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sema leo dada unachotaka ukipate
  usipoteze mada, ukamezea tu mate
  sema leo dada, nina vyote hata mkate


  BRing it on!!!!
   
 14. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  Jipe moyo wewe mrembo, lakini kwa hadhari kuu
  Sinase kwenye urimbo, kwakupenda mambo makuu
  Salazo ziwe ni wimbo, awembeleyo mola mkuu
  Utajuta kumfahamu, ukingia kichwakichwa!

  Pia tunakuombea, upate kidume bora
  Kisichopenda umbea, hatakama cha tabora
  Upendo kujinomea, msingi wa famili bora
  Utajuta kumfahamu, ukingia kichwakichwa!
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  hahahaha...ngoja waje hapa......watu na fani zao!
   
 16. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wanaojitamba leo wengi, ili waweze kupata kitu
  kwa maneno tena mengi, lengo lao hicho kitu
  achana na hao wengi, njoo unambie kitu

  Bikra nena, neno lisikike
  nikusikie tena, leo jogoo awike
   
 17. M

  Misana Member

  #17
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Malenga wetu jamani - JF
   
 18. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,124
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ni nini kimekupata, mbona unasononeka?
  uso umeufumbata, kwa kiganja wafunika,
  sema linalokusibu.

  Waonekana mzuri, surayo yamereremeta,
  Umejitunza vizuri, bikira hukuifuta,
  Vyote hivyo huna raha?

  Kama ni mume wataka, hapo usikimbilie,
  Burn aliyoyaweka, manani uyatilie,
  Kama mengine useme.

  Au ni pesa wataka, utajiri wa haraka?
  una zake hekaheka, yatakuzidi mashaka,
  Kumbuka zile za EPA.

  Unanitia huzuni, unavyojitaabisha,
  usiliweke moyoni, jambo linalokuchosha,
  JAMII tutakupoza.

  Kesho ni ya mjukuu, ya kwako wewe ni leo.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kijana wa kileo,mwenye lahaja tamu,
  Makuu hajui kwao, mwepesi wa kufahamu,
  Mhitimu wa mapozo, tajiri wa ukarimu,
  Njoo kwa Abdulhalim, ajuaye kiuyo.


  Yo Yo hakuna lolote, huyu m'bara tapeli,
  Hutopoteza chochote, kibuti mpe Fideli,
  Ntakupeleka kokote,ukiwa wa kwangu mwali,
  Njoo kwa Abdulhalim, nikutibu maradhiyo.


  Tuliza moyo kwa Duli,penzi pasipo aleji,
  M-halimu wa ukweli, mpendaji mleaji,
  N'tulize yako akili, mtungini kama maji,
  Njoo kwa Abdulhalim, nifute yako miayo.
   
 20. GP

  GP JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  dah, hapa kazi ipo, ni mistari kwa mistari
  huyu bikra mwenzenu anataka na yeye, kwani hamjuiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii?
  aaarrrrrghhhhh
   
Loading...