Jakubumba
JF-Expert Member
- Mar 5, 2011
- 1,624
- 500
Wanajf nina jirani yangu kwa kweli ananikera sana kwa matusi yake nje na ndani ya familia yake mwenyewe! Najua hata humu watu kama hawa wapo hivo tuwape somo waachane na matusi.
Jirani ana watoto watatu na majina yao anayajua lakini anawaita majina ya wanyama;
mtoto wa kwanza anaitwa juma......huyu akimhitaji utasikia anasema wewe mbwa kuja haraka!
mtoto wa pili anaitwa Alli......akimhitaji utasikia anasema wewe nyani kuja haraka
mtoto wa tatu anaitwa anaitwa rose....huyu utasikia wewe nyang'au uko wapi?
Kilichotokea sasa! Juma alipigana na mtoto wa jirani yetu, kwa kweli jirani yetu alikasirika sana na akamfuata mama yake juma kumueleza amkanye mwanae, gafla akakutana na juma mlangoni, juma akamjibu vibaya sana ndo na yeye akaudhika akamwambia nataka kuongea na mwenye mbwa na sio mbwa. Kumbe mama yake juma anamesikia...Ulikuwa ni ugomvi mkali sana kwa nini mwanae aitwe mbwa!
Jamani wanajf tuwaitewatoto wetu majina tuliyowapa tusiwabatize majina kutokana na midomo yetu michafu!