Nataka kuokoka

Ni jambo jema kabisa, Mungu azidi kukufanyia wepesi ktk yote!

Kisha hakikisha unadumu ktk kujifunza na kuyashika mafundisho ya Kristo daima!
 
Kuokoka ni kufanyika kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo,
Imeandikwa : enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi .

Mwanafunzi ni mtu anajifunza, na wakati mwingine hupewa mitihani ili akishinda avuke daraja
 
Jitahidi ujikane kwanza kisha ujitwike msalaba wako halafu mfuate Yesu Kristo.

Na kumbuka ukiokoka unakuwa barua isomwayo na watu.

Wengine wameokoka lakini wako sawa na wasiookoka.

Hawajajikana, wagumu kusamehe, hawajui kupenda wanachuki, washirikina, wazinzi,
N.k

Mavazi yao ndo utachoka kabisa, wanawake wengine juu ya magoti, mapaja wazi, migongo wazi, suluari
 
Kuokoka ndo kufanya nini?

Ni kumuamini Yesu Kristo kuwa alikufa na kufufuka na ktk wafu na kufufuka siku ya tatu na kupaa mbinguni,
Na yakwamba atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu !

Ni kumkiri Yesu kwa Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Mtawala (Bwana) wa milele.

Ni kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

Ni kudumu ktk kujifunza na kuyashika mafundisho ya Neno la Mungu
 
Kuokokaje sasa uzi muhumi kama huu unauleta apa jukwaa la jokes na udaku??acha kuja kutuleta ariff asee!!
 
Ni kumuamini Yesu Kristo kuwa alikufa na kufufuka na ktk wafu na kufufuka siku ya tatu na kupaa mbinguni,
Na yakwamba atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu !

Ni kumkiri Yesu kwa Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Mtawala (Bwana) wa milele.

Ni kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

Ni kudumu ktk kujifunza na kuyashika mafundisho ya Neno la Mungu
Kwenye zile amri, Kuna hata moja Ina neno "kuokoka" ???
 
Back
Top Bottom