Nataka kununua mchele wa mwaka huu halafu niuuze baadaye

chama mpangala

JF-Expert Member
Sep 3, 2015
508
702
Poleni wanaJF kwa majukumu na mapambano ya CORONA tukumbuke kufuata maelezo ya wataalam.

Kama kichwa cha Habari kinavyoele naomba ushauri wenu wataalam wa Biashara ya Mazao. Nataka kununua mchele wa mwaka huu niuhifadhi niuze hapo baadaye.

Je, kuna athari yoyote?
 
Jambo zuri,lakini kama hali zitakuwa hivi na hii Corona, usitegemee kupata pesa badala yake itakuwa ni mwendo wa Goods to goods,yaaani utashangaa MTU atakupa gari kwa gunia moja LA mchele.

Hapa ndipo kutaibuka Matajiri wapya ktk nchi,haswa wauza nafaka na wakulima
 
Nakupongeza kwa wazo zuri ingawa sijafahamu una lengo gani mara baada ya kununua huo Mchele.

Mimi nimenunua mchele siku kama 2 hivi zilizopita kutoka sengerema leo usiku mzigo unatua hapa mjini na lengo ni kuuza kwa jumla na rejareja.

My take:Mjasiriamali mwenye akili hutengeneza pesa wakati soko/hali imekuwa mbaya.
 
Kutokana na hili janga, uwekezaji kwenye biashara yoyote ni changamoto.... uhai kwanza, pesa zipo tu
 
Back
Top Bottom