Nataka kununua kiwanja, ila kwanini viwanja vya Chanika ni bei rahisi hivyo?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,820
18,812
Wakuu nimejipanga na bajeti ya milioni 5 hadi 8 kwa ajili ya kununua kiwanja, maeneo ya DSM au Pwani kulingana na upatikanaji utakavyokuwa, bahati nzuri mimi nafanyia kazi nyumbani so hata eneo likiwa nje ya mji halitaniletea shida endapo litakuwa na intaneti

Baada ya kufanya utafiti wangu nimeona maeno yenye viwanja vya angalau sqm 800 ni maeneo ya Kigamboni, ambapo unaweza kupata eneo la kujenga nyumba nzuri na uwanja ukabaki

Sasa kilichonishangaza ni maeneo ya Chanika kuwa na viwanja na nyumba za bei chee sana tena maeneo yenye watu wengi tu, hili ni kwa nini?

Pia naomba kujua ni taratibu gani za kufuatwa ili kuepeukana na matapeli
 
Kaka karibu Kigamboni mwembe mdogo kiwanja mita 35*35 mil 5.5 na pia ukihiitaji heka unapata

IMG_4795.jpg
 
Wakuu nimejipanga n bajeti ya milioni 5 hadi 8 kwa ajili ya kununua kiwanja, maeneo ya DSM au Pwani kulingana na upatikanaji utakavyokuwa, bahati nzuri mimi nafanyia kazi nyumbani so hata eneo likiwa nje ya mji halitaniletea shida endapo litakuwa na intaneti

Baada ya kufanya uatafiti wangu nimeona maeno yenye viwanja vya angalau 20x20 mara mbili ni maeneo ya Kigamboni, ambapo unaweza kupata eneo la kujenga nyumba nzuri na uwanja ukbaki

Sasa kilichjonishangaza ni maeneo ya Chanik kuwa na viwanja na nyumba za bei chee sana tena maeneo yenye watu wengi tu, hi;li ni kwa nini?

Pia naomba kujua ni taratibu gani za kufuatwa ili kuepeukana na matapeli
Nenda Goba, kuko poa, too modern!
 
No, misongamano ya kiswahili ndio sipendi
Unapoenda kununua 20*20 tena kwa miguu na vijibarabara vya mita 5 ..mkuu nasikitika kukuambia hicho ndicho unachokitafuta eneo lenye msongamano.. na litakuja kusongamana nguvu zishaisha na huna tena uwezo wa kuanza moja mahali kwingine.

Ardhi ni utajiri/mali. Wekeza kwa akili. Tafuta washauri consultant session ya dk 25-45 ni elfu 30000 tu uliza maswali yote muhimu, na atakusaidia kufanya preliminary checks kuhakikisha hauingizwi mkenge kwa kuuziwa maeneo ya wazi au yenye matumizi mengine ya umma auaeneo yaliyovamiwa yenye upimaji.

Ukitaka kwenda site kufanya full analysis na kukushauri juu ya bei sahihi inayoendana na thamani.. inalipa kuanzia sh. 200,000/- site visits inclusive.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo bei yako nakushauri, tafuta kiwanja Bunju mpaka Mapinga, utapata kiwanja siyo chini ya sqm 800 kwa Mapinga, hapo unaweza kuweka hata garden na mabanda ya mifugo, kiwanja cha sqm 400 ni kidogo sana, BRT Phase 4, inasogea mpaka Bunju, unaona joto la bandari ya Bagamoyo linavyopanda...
 
Kwa hiyo bei yako nakushauri, tafuta kiwanja bunju mpaka mapinga, utapata kiwanja siyo chini ya sqm 800 kwa mapinga, hapo unaweza kuweka hata garden na mabanda ya mifugo, kiwanja cha sqm 400 ni kidogo sana, BRT Phase 4, inasogea mpaka Bunju, unaona joto la bandari ya bagmoyo linavyopanda...
Ndio mkuu, kiwanja cha sqm 400 kidogo sana, nipe connection na wauzaji wa huko kama unao
 
Back
Top Bottom