Msaada: Nataka kununua gari

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
52
Wajameni,

Kuna jamaa yangu katoka mkoani juzi, kaja na tuhela twake anataka kununua kausafiri. Amenitonya kuwa anazo TZS 5 mil lakini anaweza kujitanua (ku-stretch) hadi TZS 6 mil.

Juzi jumamosi nilimpeka pale mnazi mmoja sehemu ile ya kidongo (siku hizi kuna turubai la mama zain africa). Pale magari yalikuwepo ila yanaanzia TZS 8 mil, yaani yale anayoyataka yeye (4 cylinder, na muonekano kidogo). Ilikuwepo moja Ballon Mark II GX90, 6 cylinder, 1G, ya mwaka 1995 kwa TZS 5.8 mil lakini akaogopa hilo 6 cylinder.

Mjumbe hauwawi.
 
Kuna gari lilikuwa linatangazwa kwenye blog ya Mjengwa nadhani lilikuwa linatoka kwa 5 mil.
 
Mwambie asibahatishe, aende show rooms ziko nzuri zenye bei ya kawaida kabisa. Atauziwa kimeo kwa bei mbya mno!
Makumbusho show rooom, fire n.k pale bei zao sio mbaya ,ila pia usipokutana na mwenyewe utaambiwa bei za hovyo!
 
Tena kama mnaweza muende na qualified & experienced Auto-Mechanic ili aicheki gari fresh. Mnaweza kupigwa changa la macho kwa kuuziwa kimeo
 
Kama huyo jamaa yako hana uwekezaji wowote,
mshauri anunue gari la biashara kwanza.
Starehe inahitaji pesa wandugu.
 
Thanks to all who have shown interest in assisting. Jamaa amepata gari jana kwa TZS 4.8 m, Chaser Baloon, 4 cylinders ya 1995. Ni nzuri kwa bei hiyo, gari ilikuwa inatumika na mama mmoja wa kiarabu. Ninavyoandika saa hii jamaa anayoyoma kuelekea mkoani.

Nawashukuru wana JF wote kwa kufanikisha.
 
Aisee pale fire apafai kabisa kwani nilienda kununua gari jamaa wakaniuzia gari pajero mini kwa mil. 14....nikalipa cash ila mziki ulikuwa kusajiri gari kwa jina langu, hapo mandata wakanizunguka kinoma kumbe document nilizopewa za gari ni za pikipiki ambayo ipo zanzibar......niliporudi kwa jamaa pale fire akaniruka kana kwamba sikununua pale.....ilikuwa ni mziki wa aina yake ndugu.....so please kuwa makini na showroom....maana wengine wanaiba magari kutoka majuu
 
Kama hana haraka aagize toka Japan gari zimeshuka bei, acheki japanese trader car view kuna madelear wengi
 
Kwanini watu wanaogopa 6 cylinder, nilishawahi kutumia 4 na sasa natumia 6 sijaona tofauti afterall nikienda nyumbani (Moshi) na six nakuwa more comfortable coz in engine nzito so ina balance na mwendo wake pia ni mzuri
 
Kwa nn watu wanaogopa 6 cylinder, nilishawahi kutumia 4 na sasa natumia 6 sijaona tofauti afterall nikienda nyumbani (Moshi) na six nakuwa more comfortable coz in engine nzito so ina balance na mwendo wake pia ni mzuri

kaka 6 linakula wese vibaya mkuu! na likianza kuchoka ndo utalichukia kabisa.lakini inategemea na kipato chako kama kipo level''kifisadi'' huwezi kushtuka.
 
Kwa nn watu wanaogopa 6 cylinder, nilishawahi kutumia 4 na sasa natumia 6 sijaona tofauti afterall nikienda nyumbani (Moshi) na six nakuwa more comfortable coz in engine nzito so ina balance na mwendo wake pia ni mzuri

Mkuu nadhani ni woga na hearsay za watu tu, actually kwa mwendo wa safari ndefu ni nzuri kuliko 4 kama ulivosema, na una uhakika wa safari...na haisumbui sumbui kama na wewe unaipa matunzo yanayostahili!
 
Aisee pale fire apafai kabisa kwani nilienda kununua gari jamaa wakaniuzia gari pajero mini kwa mil. 14....nikalipa cash ila mziki ulikuwa kusajiri gari kwa jina langu, hapo mandata wakanizunguka kinoma kumbe document nilizopewa za gari ni za pikipiki ambayo ipo zanzibar......niliporudi kwa jamaa pale fire akaniruka kana kwamba sikununua pale.....ilikuwa ni mziki wa aina yake ndugu.....so please kuwa makini na showroom....maana wengine wanaiba magari kutoka majuu

August,
Kwani uliponunua hiyo gari hawakukupa hata risiti inayoonyesha details zote za gari ikiwemo namba za chasis na injini?
 
Habari JF.
Nataka kununua gari nina kiasi ya shilingi Milioni tano tu, Gari ninayoitaji iwe Corolla, Au Rav4 Old model,
Kwenu wadau.
 
Habar jf.
Nataka kununua gari nina kiasi ya shilingi Milioni tano tu, Gari ninayoitaji iwe Corolla,Au Rav4 Old model,
Kwenu wadau.

...hongera mkuu! "kwenye blue" ni magari mazuri, lakini jiandae kulipa Dumping cost TRA (pricing policy) - model hii iko nje ya miaka 10 ya TRA,

...kiasi cha fedha yako unaweza pata 3doors!
 
weka mara mbili upate gari ya uhakika, kwa hyo hela yako utakuwa fundi magari pia
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Hela yako ni ya pikipiki unataka kununua gari. watakuuziaugonjwa wa moyo mtumba kwisha kazi utuwekee ucku barabarani. ushauri wa bure kanunue Sanlg mbili. moja yako nyengine fungua business ya boda2
 
Back
Top Bottom