Nataka kununua gari Zanzibar

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
2,291
4,033
Habarini wadau.
Kijana mwenzenu nimezichanga za kutosha tu ili nami nimiliki gari. Katika kuangaza huku na huku nimeonelea bora niingie zangu zenji nikanunulie gari iliyotumika huko kwani nasikia huko bei ni rahisi ukilinganisha na hapa dar, kingine nahisi ya hapa dar yamelamba mileage za kutosha tu ukikompea na zenji, pia nikiliingiza dar litapatiwa namba mpya hivyo hata wakati wa kuliuza sitopata tabu.
Naombeni wadau mnijuze basi itanigharimu sh ngapi kulisafirisha na kulisajili.
Je idea yangu ni nzuri ama niangazie tuu ya humu humu mitandaoni?
Ushauri wenu ni muhimu wadau ikizingatiwa ni gari yangu ya kwanza.
Asanteni.
 
Chaguo ni lako mkuu, fanya uchunguzi wa kutosha kati ya mtandaoni na Zanzibar wapi hautatumia gharama kubwa
 
Jiandae kukabiliana na watu wa custom mkuu..kuivusha gari kutoka Zanzibar mpaka bandari ya salama sio chini ya milioni tatu na ushehe, hali ni tete kwa sasa pale bandarini!
 
Nunua tu, ila jua ukija bara utalipia kiasi cha ushutu ambacho hukutozwa Z'bar. Kama calculator ya Z'bar inasema ushuru milioni 2, ya huku mil 4. Siku unalihamishia bara jua utalipia hiyo mil 2 ilobaki.
 
Back
Top Bottom