Nataka kununua bidhaa kupitia Jumia, naomba kujua uaminifu

Mickih Tutu

Member
Mar 8, 2014
26
6
Nataka kununua bidhaa kupitia JUMIA naomba kujua uaminifu na uhakika wa hii huduma kama kuna ambaye aliyewhi pata huduma hii anisaidie
 
Wako vizuri kiongozi wakisha kuletea bidhaa ndo unalipa wako makini sana kikubwa wape location ulipo watakupigia nakukuletea order yako
 
Wako poa ila jumia ya sasa sio kama zamani kipindi inaanza.

Mwanzoni wao ndio walikuwa wanauza bidhaa lakini tofauti na sasa.

Kwa sababu kwa sasa imekuwa kama soko (market place).

Hivyo madalali wamejaa kwa unaweza kuuziwa bidhaa kwa bei ya juu.

Mfano niliwahi tafuta flash za imation
gb 8 ambapo maduka ya mtaani ni chini ya tsh 14,000 lakini jumia kuna baadhi ya wauzaji wanauza 32,000.

[
Screenshot_20190423-213451.png


So unaweza check jinsi bei isivyoendana.

Kwa hiyo kuwa makini na bei za jumia inaweza isiwe msaada kutokana na uwepo wa madalali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom