Nataka kununua Alteza; ni bora ninunue KUPATANA au BE FORWARD?

Wakuu hivi kunatatizo la kiufundi au kiusalama ya kutumia Carina kwa safari ndefu mfano mtwara-arusha?niliplan kununua rav4 ila bajet imegoma

mkuu,hzo ndinga ni ngoma ngumu kinyama,nina mshkaji wng mjeda yupo kigoma,mara kibao huwa anapush TI lake kuja kumsalimia mama yake hapa moro,ni ndinga zinazovumilia sana hata long safari,kama upo willing nakushauri ununue hili gari
 
issue yako hapo ni beforward unaona ukiagiza kulisubiria unaona mbali... ila uzuri wa kuagiza hasa likiwa na inspection unapata gari lililo bora ulilochagua kwenye mtandao. hiyo kupatana ni bahati kupata gari lililo bora, Altezza sio mbaya kwenye ulaji wa mafuta maana kama likitunzwa halishuki Km10-9/Lt.

nimegundua unataste ya kupenda fancy car so hapo ujakosea ili mradi tu liwe limetunzwa kama utataka kununua hapahapa tz
 
Wakuu ninataka mwezi huu nipate kausafiri.. sasa nimeingia beforwad naona gari nzuri tu ila hata hii website ya kupatana naona Alteza afu bei nyepesi nyepesi. msaada wenu jamani
Altezza Zipo aina Mbili mkuu, 4 cylinder and 6 Cylinder. RS 200, RS 200 Z edition, (Sport Look Edition) L Edition. Kila Edition ina features tofauti japo muonekano wa Body ni ule ule, Hivyo kabla hujafanya maamuzi fanya utafiti. Ni gari nzuri sana na iko solid, na ni nzito sana. Iko poa sana
 
Altezza gari nzuri nimekaa nayo zaidi ya mwaka sasa nimesafiri nayo sana spea bei nafuu na ukipata four kama yangu haili mafuta ila ukileta ma speed inakuua gari inakimbia sana!!
 
ndio gari nnayo ipigia hesabu ingawa nimetishwa na watu kuhusu mafuta
Usihofu. Hazili sana mafuta, nadhani kwa mjini zinakwenda km 9 kwa lita. Kama unasafiri mbali zinakwenda inakula hadi km 12 kwa lita moja. Ni ngumu pia
 
Mimi ningekushauri Escudo kwasababu kwanza ni gari ngumu kuliko RAV 4 model yoyote lakini pia Escudo nyingi ni 4wd kwa hiyo ni nzuri pia maana popote wewe ni kwako kwenye tope mchanga kilima kikali nk
Mkuu Escudo au land cruiser ndogo ina 4wd na ina nguvu sana na ngumu hii gari apa mjini ikinyesha mvua huwa naitumia,tena kwa kijijini ndo utaipenda tafuta kati ya hizi tatu,Nomade,Vitara au Grand vitara na Jimmy hutajutia
 
Back
Top Bottom