Fahamu mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia ili kunenepa au kuongeza uzito wa mwili (Kilo)

Usiruhusu kuskia njaa kula kwa kutumia "kichwa" yani kila ukiwaza kula chukua chakula chochote kula, uwe na juisi kubwa la azam na mkate, baada ya tea kabla ya lunch unagonga silesi kadhaa na juice,baada ya lisaa baada ya lunch silesi kadhaa na juisi, kabla ya mlo wa jioni kunywa bia moja.Miezi mitatu utajikataa
 
Kila la kheri mtoa mada,usisahau mrejesho
tapatalk_1510456373773.jpeg
 
Nilikuwa mwembamba nikawa nachukia sana wembamba Baadae nikapata pesa nikawa nakula milo hata mitano kwa siku, nyama kwa wingi, nikawa bonge la mtu sasa nahangaika gym kupunguza mwili mpaka najuta, najinyima kula lakini wapi, mleta Mada utakipata unachokitafuta na utafurahi kwa miaka michache then utajuta Nakwambia, wembamba ndo afya
 
Usiruhusu kuskia njaa kula kwa kutumia "kichwa" yani kila ukiwaza kula chukua chakula chochote kula, uwe na juisi kubwa la azam na mkate, baada ya tea kabla ya lunch unagonga silesi kadhaa na juice,baada ya lisaa baada ya lunch silesi kadhaa na juisi, kabla ya mlo wa jioni kunywa bia moja.Miezi mitatu utajikataa
Bila kusahau blue band na jam kwenye mkate, apake kila kipande kwa kujaza
 
Afya yangu juzi kati ilizorota kidogo nikawa nmekonda ila saivi nimeeanza kugain weight sema tatizo linakuja nanenepa na kitambi nacho kinasogea mbele ya upeo wa macho yangu

Kiukweli nahitaji kuongeza weight bila kupata kitambi na wala sitaki kufanya mazoezi ya tumbo...

Anaejua solution ya kunenepa bila kutoka kitambi atusaidie
 
Kula chakula mdo mdo, sio unakula kingi kwa wakati mmoja,

Usile masaa mawili au matatu kabla ya kulala,

Lalia upande wa kulia au chali

Kunywa maji mengi

Usile mavyakula ya Artificial sana na vyenye sukari nyingi kma majuisi na mayai ya kisasa

Mwisho ujue sio kila mtu ananenepa, wengine sisi hata iweje bado ni vimbau mbau.
 
Yeah!
Usile vyakula vya wanga kwa wingi(carbohydrates). Maugali na wali kula kidogo sana.

Usinywe bia (safari lager, Kilimanjaro, and the like).
Kwenye bia hapo nakubali,mwili wa mtu kama una asili ya fat halafu akiwa anakunywa bia na anakula fresh mwili unaumuka na kitambi hakimuachi.Kuondoa tatizo lazima muhusika afanye mazoezi ya kupunguza tumbo.
 
Back
Top Bottom