Benaya-
JF-Expert Member
- Jul 31, 2019
- 4,417
- 7,609
Ninakuunga mkono, kukaa mbali na familia ni kuongeza mzigo wa maisha na hatari ya ndoa kuyumba.Nipo kwenye ndoa na mke wangu kwa muda wa miaka 5 sasa, mke wangu amekuwa nami bega kwa bega kwa kipindi chote hicho japo changamoto za hapa na pale ni kitu cha kawaida kwenye maisha.
Nimebahatika kujaliwa watoto wawili na mke wangu, wa kwanza akiwa na miaka saba na wiki Ana miaka miwili sasa, na ninamshukuru Mungu watoto wanaendelea vizuri.
Sababu ya kumuachisha mke wangu kazi ni moja tu, mke wangu ni muajiriwa serikalini na hivi majuzi alipata uhamisho wa kushtukiza kwenda Njombe kama kituo chake cha kazi, juhudi mbalimbali zimefanyika ili angalau ahamie karibu imeshindika. Mshahara wake ni wa kawaida.
Nimepanga kukopa mahali hela kama 50M ili nimfungulie biashara kama vile Duka la vipodozi, Vifaa vya ujenzi na Umeme au nimnunulie coaster ambayo itakuwa inamletea kipato kila siku huku akijishughulisha na biashara ndogondogo za hapa na pale hapa nyumbani. Hii ni baada ya kuona mwanamke akiwa mbali na familia uwezekano wa familia hiyo kupotea hususani watoto ni mkubwa kwani asilimia kubwa wanalelewa na dada wa kazi.
Naomba ushauri wenu tafadhali nipo njia panda.
Utalazimika kuwa na mchepuko uvumilivu ukikudhinda au hata yeye kuchepuka.
Lakini wazo la coaster halifai