Nataka kumuachisha mke wangu kazi. Naombeni ushauri katika hili

Kwani nani ameupima?
Acha ujinga na wewe.

Nimesema kwa upande wangu Mimi nitawarudishia wazazi fadhila..hata kama ni kwa kiasi kidogo.
Ni kama tunavyomtolea humu sadaka,hakuna Cha thamani kinachoweza kutosheleza kutoa ila tunafanya hivyo kwa vidogo hivyohivyo

Si lazima wote tukawa na mtazamo sawa.
Usianze kuniona nina shida kwa kuwarudishia fadhila wazazi wangu..huo ni msimamo wangu na upendo wangu tu.
Wewe kama hutaki kufanya basi usiwaone wanaofanya ni wajinga.
Tuliza na acha kisebu sebu, kama husomi na kuelewa nachokiandika bora uwe mvumilivu na ukisome unachokiandika.

Haya ndiyo matatizo ya kujadiliana na watoto mambo ya kikubwa.
 
Kama wewe unavyowatunza na mkeo anawatunza hivyohivyo.

Kumbe kuacha ni ngumu?
Kwanini umuambie mwenzio aache?

Kila mtu ana kusudi la kulitimiza hapa duniani na kila mtu kuna nafasi Mungu amempangia asimame akae
Mwanamke na Mwanaume hawako sawa, usinilinganishe mimi na wewe, na haitokaa kuja tukawa sawa.

Kuwatunza wazazi siyo lazima wewe utoke ukatafte hela.
 
Aisee juzi Niliona baadaye nikasema nitakushauri kadri nitakavyoweza ila nilikuja kupitiwa na leo nimeona tena nikasema hapana nitajaribu kukushauri na sio lazima ufate kila ushauri wa mtu humu ila na wewe una akili zako na plan zako mpaka hapa ulipofikia.
Kwanza kabisa nikushukuru kwa kusema mko bega kwa bega na wife wako. Ni jambo la kumshukuru Mungu maana ndio msingi mwema wa kupata maendeleo.
KUHUSU BIASHARA ZA KUFANYA NA BIASHARA ZA KUTOKUFANYA
Kila biashara ina changamoto zake na kila biashara inafaa kufanya ila inategemeana na vipindi na mtu na mtu na usimamizi.
VIPODOZI:- Hii ni biashara nzuri kwa huo mtaji wa 50m ni biashara nzuri na nadhani utafungulia sehemu yenye mchanganyiko wa watu wengi
VIFAA VYA UJENZI:- Katika biashara yenye faida ya haraka na nzuri ni hii ya vifaa vya ujenzi nakushauri kuwekeza na wala hutojuta ni biashara inayohitaji usimamizi wa kwako mwenyewe au mke na biashara hii hutokuja kujuta endapo utakuwa umepata sehemu nzuri. pia mtaji unapozidi kukuwa unauwezo kuuza mpaka tofali na uzuri ukitengeneza uaminifu mzuri kwa jamii inayokuzunguka utakuta mtu anawekeza hela kwako ya kujenga nyumba wakati huo huo pesa yake unaizungushia kwenye mtaji wako. Mfano. mtu anakuja anakwambia naomba nilipe milioni 3 za tofali nitachukua mwakani uniandikie risiti sasa pesa ile ile unaenda kuinunulia cement nondo na zingine mchanga unapiga tofali akija mwingine unamuuzia ndivyo watu wengi wanafanya kwa hawa wenye maduka ya vifaa vya ujenzi
COASTER:- Katika biashara ambayo sikushauri kuifanya ni hii ya gari tena asimamie Mke wako kaka maamuzi ni ya kwako ufanye au usifanye Ila mimi kama mimi nisingefanya au kumfungulia mke wangu mradi huu. Ni mradi unaohitaji mtu mkatili mwenye kukosa kauvumilivu maana kuna wakati madereva wanakuwa pasua kichwa kabisa anakwambia leo amekosa hesabu kumbe yeye anaenda kulipia ada ya mwanae au anasingizia gari imeharibika kumbe sio. Nikupe kisa kimoja kaka yangu alikuwa na DCM Mbagal mwenge kutokana na kazi zake za biashara alikuwa anashindwa kufuatilia mara kwa mara hivyo kupelekea kupigwa sana na madereva nakumbuka kuna siku aliambiwa gari imeharibika wakati natoka shule nakutana na gari imekodiwa. siku nyingine kaambiwa gari imeuwa pump anatuma hela kumbe uongo basi kukawa na visa vingi mpaka akaniambia naiuza. wakati huo nilikuwa nasoma veta mambo ya magari. Nikamwambia shida nini? akaniambia gari inamsumbua sana mara kwa mara kuharibika. nikamwambia niachie mimi maana yeye ndiye alikuwa ananisomesha, Nikamwambia ukiambiwa gari imeharibika nijulishe basi siku iliyofata broo akanipigia simu gari imeharibika nikatoka shule nikapanda gari mpka mwenge na nikarudi nikashukia magomeni nikakaa kama masaa matatu bahati nzuri nikakutana na konda ninayefaamiana naye nikamuuliza gari x umeiona wapi akaniambia nenda gest flan maeneo flan nimeiona imepakiwa pale. Nikaenda nilipofika nikaiona gari nikamwambia broo piga simu waulize wako wapi dereva akasema gari lipo Garage na konda yupo hapo hapo garage ila yeye ameenda kutafuta kifaa hivyo atume laki moja maana yeye alikuwa na kama elfu 50.basii nikamwambia asitume nikasubiria baadaye wakatoka Konda na demu wake dereva na demu wake. yalioendelea siwezi kuendelea kuhadisia ni mengi.
Hitimisho kwenye hii biashara usifanye hii biashara kwa kumwachia mke wako wala rafiki yako simamia mwenyewe na pia sio biashara ya kutegemea hapo kila kitu ila biashara hii ya coaster ni nzuri pale ambapo unafanya ukiwa nazo mbili kuendelea ndio utaona faida yake maana kumbuka milioni hamsini unazosema hazitoshi kununua coaster labda ununue kwa mtu maana kuagiza used itakuwa hiyohiyo fedha bado kuja kusajili vibali na mstari nadhani ni zaidi.
DUKA LA DUKA LA MADAWA: -Ni biashara nzuri yenye faida kubwa sana ila ina masharti mengi sana ukiyakamilisha hutojuta kuifanya nakushauri pia.
Huo ndio ushauri wangu kwako. Ushauri sio lazima kuufata. ila kukaa mbali na mke hakuvumiliki nakuunga mkono swala la kumwachisha mke wako kazi kwa maana umesema mko bega kwa bega. pia cheki kipato chako na cha kwake kipi kikubwa kama cha kwake ni kikubwa basi hata wewe unaweza kuacha na kufata mkewo angalia pia security ya kazi yako na ya kwake je ipi ni nzuri. Nakumbuka kuna mtu alinishaurigi mimi kwanini umeajiriwa na je mshahra wako unazidi milioni 3 nikamwambia hapana akasema kwa nini sasa unaendelea kuajiriwa nikamuuliza nifanye nini akaniambia nianzishe kilimo na ufugaji nikamcheka sana nifuge mimi kweli nitapata milioni 3? akaniambia tena zaidi ya hiyo. fuga kuku utaniambia nikamwambia tokea kijijini tumekuwa tukifuga sijawahi kuona wamefika 100 kideri kinapita kinabeba kadha na kufa akanicheka sana akaniambia ukafuge utaniambia nunua mitete 10 nikanunua baada ya muda wakaanza kutaga walipoanza kulalia ukapita ugonjwa wakafa 6 nikabakiwa na wanne nikamfata Mama nilichokuwa nakwambia njoo ukione wamekufa 6 nimebakiwa na wanne tuu akanicheka akaniambia nilitaka uanze ukwame ndio sasa nianzie hapo akaniambia nunua vifaranga 100 mimi nikanunua akaniambie nenda ukanunue dawa x+x+x Maduka ya mifugo nikanunua tukawapa kwa formula za huyo mama basii ilienda hivyo mara kwa mara kila baada ya miezi 3 mpaka kuku wakawa wakubwa nilipata kama kuku 80 wengine walikuwa wanakufa kwa uzembe paka naye akijiokotezea kadhaa kicheche naye na wengine walikuwa kwa kukosa maji maana mimi nilikuwa mbali kikazi na wife naye ni mwajiriwa hivyo shughuli za kulisha zilikuwa dada wa kazi ila kwenye dawa lazima niwepo basi walipoanza kutaga niliuza mayai na vifaranga nikaona kazi ya kufanya ndio hii basi niliendelea hivyo mpka nikapata kuku 200 kwa usimamizi mdogo na wakiibiwa nilikuwa sijui hata ukiwauliza wanasema hawajui maana walikuwa wanachanganya huwezi kujua yupi yupo yupi hayupo hivyo ilikuwa kazi sana baadaye kwa sababu pale nilikuwa nimepanga tukahamia niliojenga hivyo tuliwauza baadhi na wengine nikahamishia sehemu nyingine na muda nikauza nikafetua tofali kama 800. hivyo ninachojaribu kusema biashara ni usimamizi wa wewe mwenyewe au mtu wako wakaribu ambaye ni mke wako.Pia nilimtembelea yule mama siku moja na kujionea mifugo yake alikuwa na mifugo wengi sana ambao walikuwa wanamtengenezea zaidi ya milioni 3 kwa mwezi bimana alikuwa na kuku wa kienyeji akiuza mayai na vifaranga, ngombe wa maziwa 6 wanene na wakisasa wakuto maziwa mengi, kuku wa nyama zaidi ya 2000 kuku wa mayai ya kisasa.
 
Tuliza na acha kisebu sebu, kama husomi na kuelewa nachokiandika bora uwe mvumilivu na ukisome unachokiandika.

Haya ndiyo matatizo ya kujadiliana na watoto mambo ya kikubwa.
Unaonaje ungeacha wewe hicho kisebusebu?
Na wewe kama husomi na kuelewa nilichoandika ungekaa kimya na kuwa mvumilivu.

Hivi kumbe mtoto anaishia miaka mingapi?
Naona unaanza kunipeleka Tena kwenye utoto we engineer Zurri.
Una miaka 29,nina miaka 24
Hakuna aliye chini ya 18 hapo.
 
Nipo kwenye ndoa na mke wangu kwa muda wa miaka 5 sasa, mke wangu amekuwa nami bega kwa bega kwa kipindi chote hicho japo changamoto za hapa na pale ni kitu cha kawaida kwenye maisha.

Nimebahatika kujaliwa watoto wawili na mke wangu, wa kwanza akiwa na miaka saba na wiki Ana miaka miwili sasa, na ninamshukuru Mungu watoto wanaendelea vizuri.

Sababu ya kumuachisha mke wangu kazi ni moja tu, mke wangu ni muajiriwa serikalini na hivi majuzi alipata uhamisho wa kushtukiza kwenda Njombe kama kituo chake cha kazi, juhudi mbalimbali zimefanyika ili angalau ahamie karibu imeshindika. Mshahara wake ni wa kawaida.

Nimepanga kukopa mahali hela kama 50M ili nimfungulie biashara kama vile Duka la vipodozi, Vifaa vya ujenzi na Umeme au nimnunulie coaster ambayo itakuwa inamletea kipato kila siku huku akijishughulisha na biashara ndogondogo za hapa na pale hapa nyumbani. Hii ni baada ya kuona mwanamke akiwa mbali na familia uwezekano wa familia hiyo kupotea hususani watoto ni mkubwa kwani asilimia kubwa wanalelewa na dada wa kazi.

Naomba ushauri wenu tafadhali nipo njia panda.

Kama nyumba mnayoish ni ya kulipa kodi na watoto wanaenda shule day maliza kodi yako iliobaki wapange nyumba huko ambako amepata kazi aishi na watoto na Kama ni boarding ndio vzur zaid watoto wakirud likizo wanajua tu nyumban ni njombe na ww unabaki hapo unapofnya kazi cku ukijickia kwenda unenda tu kama weekend au likizo au mwez Mara moja au Mara mbili wewe tu na nauli yako na muda wako sisi graduate huku hatuna kazi nyinyi munaacha kazi
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mwanamke na Mwanaume hawako sawa, usinilinganishe mimi na wewe, na haitokaa kuja tukawa sawa.

Kuwatunza wazazi siyo lazima wewe utoke ukatafte hela.
Mimi wangu lazima niwatunze kwa namna yoyote.
Kama nitakaa nyumbani basi huyo mwanaume awe tayari kuwatunza kwa kiwango kilekile ambacho ningefanya Mimi na nihakikishe hilo mapema.

Bado narudi palepale
"KUSUDI"

Sijui nyie Muhammad amewafundisha vipi hukusu hili ila huku kwetu kila mtu duniani ana kusudi lake na limefungwa ndani ya muda.
 
Nipo kwenye ndoa na mke wangu kwa muda wa miaka 5 sasa, mke wangu amekuwa nami bega kwa bega kwa kipindi chote hicho japo changamoto za hapa na pale ni kitu cha kawaida kwenye maisha.

Nimebahatika kujaliwa watoto wawili na mke wangu, wa kwanza akiwa na miaka saba na wiki Ana miaka miwili sasa, na ninamshukuru Mungu watoto wanaendelea vizuri.

Sababu ya kumuachisha mke wangu kazi ni moja tu, mke wangu ni muajiriwa serikalini na hivi majuzi alipata uhamisho wa kushtukiza kwenda Njombe kama kituo chake cha kazi, juhudi mbalimbali zimefanyika ili angalau ahamie karibu imeshindika. Mshahara wake ni wa kawaida.

Nimepanga kukopa mahali hela kama 50M ili nimfungulie biashara kama vile Duka la vipodozi, Vifaa vya ujenzi na Umeme au nimnunulie coaster ambayo itakuwa inamletea kipato kila siku huku akijishughulisha na biashara ndogondogo za hapa na pale hapa nyumbani. Hii ni baada ya kuona mwanamke akiwa mbali na familia uwezekano wa familia hiyo kupotea hususani watoto ni mkubwa kwani asilimia kubwa wanalelewa na dada wa kazi.

Naomba ushauri wenu tafadhali nipo njia panda.
Acha wewe kazi, mkeo aendelee na kazi
 
Kuna wanaume wenzio hawajafikiria yote hayo.
Halafu bado wanajiona wana akili kubwa.

Unajua katika ndoa kuna milima na mabonde..kuna maudhi pia.
Mkianza kupita kipindi upendo umepungua..hasahasa mume akipunguza upendo basi huyo mwanamke hakuna rangi ataacha kuona
Yeah,we're human kuna kuachana pia.......then usiwalaumu mm nimekulia kwenye single parent.....Baba alikuwa ni mwajiriwa wa serikali mwenye post fulani , miaka ya 1980's baba alianza kumwambia mama aache kazi wakati wanawatoto 3,wakubwa zangu
...alikuwa Nurse....mama akagoma,tukazaliwa jumla 6.....kabla wengine hatujafika popote mzee mwaka 1998 akafariki....Mi nilikuwa drs la 5 na wadogo zangu wa2......yes mzee aliwekeza wekeza hapa na pale ila kale kakibarua ka mama ndiyo kamatubeba Sana mpaka alipostaafu 2013........kumwachisha kazi anaweza ila akiwa anajua anainvestment kubwa isiyoteteleka Ila siyo haya ya wivu tu wa kuibiwa maana hiyo inaweza kuwa ni tabia tu ya mtu,hata mkiishi wote anaweza chepuka tu
 
Mkuu
Huna haja ya kuingia kwwnye mkopo mzito kiasi hicho wakati hali ya biashara nchini unaijua

Nakushauri kama mpambanaji na mwanaume mwenzangu

Tafuta milioni 10 tu kisha ingia kwenye biashara ya mazao.

Kwa mfano, msimu wa KARANGA unawadia huko TABORA mwezi ujao

Kilo moja huuzwa max 1800 Tshs
Hivyo gunia linaenda mpaka 180,000

Hizo karanga zinakuja kuuzwa Kaha shinyanga kwa Tsh 2300 max.

Unaweza kuona difference ni Kubwa per kg.

Kadri unavyokuwa na mtaji mnene ndivyo unavyopiga hela.

Gharama za biashara sio kubwa sana.

Mimi nimejikusanya hapa nina laki 7 tu mwezi ujao namtumia ndugu yangu akakuze biashara.

Kumbuka hii ni biashara ya miezi miwili mitatu tu kisha unahamia kwenye mchele.

Huko kwenye mchele according to my bro faida kwa gunia 1 ni Tshs elfu 10 mpaka 14

Ukiwa na gunia 100 per round una one million.

Kwa mwezi unaenda round 3, maana kuna ukusanyaji usafirishaji n.k

Msimu wa mchele ukikata tunahamia kwenye ng'ombe..

Kaka amka!!
Utajiri upo kwenye biashara za mazao

Kodi huko ni almost hakuna
Biashara ya mazao kwa sasa hailipi mazao mtaani ni mengi mipaka imefungwa nafaka za mwaka jana na mwaka huu tunakutana sokoni, demand yake iko chini

Usikurupuke atalia na kusaga meno

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mimi wangu lazima niwatunze kwa namna yoyote.
Kama nitakaa nyumbani basi huyo mwanaume awe tayari kuwatunza kwa kiwango kilekile ambacho ningefanya Mimi na nihakikishe hilo mapema.

Bado narudi palepale
"KUSUDI"

Sijui nyie Muhammad amewafundisha vipi hukusu hili ila huku kwetu kila mtu duniani ana kusudi lake na limefungwa ndani ya muda.
Kazi yangu nimemaliza.
 
Yeah,we're human kuna kuachana pia.......then usiwalaumu mm nimekulia kwenye single parent.....Baba alikuwa ni mwajiriwa wa serikali mwenye post fulani , miaka ya 1980's baba alianza kumwambia mama aache kazi wakati wanawatoto 3,wakubwa zangu
...alikuwa Nurse....mama akagoma,tukazaliwa jumla 6.....kabla wengine hatujafika popote mzee mwaka 1998 akafariki....Mi nilikuwa drs la 5 na wadogo zangu wa2......yes mzee aliwekeza wekeza hapa na pale ila kale kakibarua ka mama ndiyo kamatubeba Sana mpaka alipostaafu 2013........kumwachisha kazi anaweza ila akiwa anajua anainvestment kubwa isiyoteteleka Ila siyo haya ya wivu tu wa kuibiwa maana hiyo inaweza kuwa ni tabia tu ya mtu,hata mkiishi wote anaweza chepuka tu

Sina haja ya kuongeza neno tena.
Wewe ni mwanaume..itoshe kusema hivyo.
Ningekuwa na zawadi ningekupa
 
Biashara ya mazao kwa sasa hailipi mazao mtaani ni mengi mipaka imefungwa nafaka za mwaka jana na mwaka huu tunakutana sokoni, demand yake iko chini

Usikurupuke atalia na kusaga meno

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Jifunze kitu kimoja

Kula ni lazima, masuala ya inflation sijui price fluactuation wafanyabiashara wazoefu wanajua KWENDA NA NYAKATI.

Labda uniambie ni zao gani la chakula kuanzia mchele maharage karanga n.k ambalo haliendi.

Mchele kilo 1 mwanza mabatini inafika 900, dukani ni 1000 mpk 1100.

Njoo na figure mkuu tuzidi kuelimishana
 
Wewe unaleta nadharia wenzako tupo field tunalia na nafaka zetu

Tena huko hiyo biashara usifanye kabisa kama kilo ni 900 kumbe afadhali ya huku tunauza 1200, 1300 1400 super 1700

Na faida yake imepungua sana ni 50 to 100 per kg na mzigo hauendi haraka yaani ni majanga mchele mtaani ni mwingi

Kama unabisha jitose kwenye hii biashara utanipa mrejesho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo watupe hela kunisomesha..tena wengine tumetoka familia za Kawaida sana wazazi wamehangaika mno ili tupate kusoma.

Halafu napata kazi naacha au siyo?!
Kwanini usiache wewe mwanaume ili unifwate uanze hiyo biashara ya coaster na vipodozi..
Hawezi kukujibu wallah,
 
Kwanza ni dhambi mbele za Mungu.
Ulipewa kazi kufanya bahati mbaya hujafanya kwa sababu za kijinga tu!

Ni dhambi pia unakuwa umewafanyia wazazi waliohangaika na wewe kwa miaka karibia 20 kukutunza na kukusomesha.

Mwanaume wa kweli anatakiwa awe chanzo cha ndoto zako kutimia.
Yani mwanaume anayekupenda ataku support aisee, sasa huyo anaacha kaxi, vipi hao watoto kuanzia bima, Ada za shule biashara ikibuma, au mwanaume akaoa mke mwingine, nadhani kazi akiacha mwanaume inapendeza maana wao kutelekeza familia huwa ni rahisi na hawana uchungu kabisa
 
Kwani mkianzisha mradi wenu binafsi huwezi saidia familia yako unayodai ilikusomesha kwa shida?

Je ni kazi pekee ya kuajiriwa inayokuweka mbali na familia yako ndio inayoweza kukufanya kuisadia familia yako iliyokusomesha?
Kwanini wewe usianzishe mradi kuliko ku force mwenzako aache kazi, tena Zama hizi za uncle ambapo uchumi huko ICU watu wamefunga biashara haziendi
 
Najua kuna wanawake wa namna yako,wenye mawazo weak namna hii, na wewe ni mwakilishi tu, naamini either una matatizo ya 'kisaikolojia' yaliyosababishwa na mahusiano au ni kukosa malezi bora tu katika familia.
Yani mwanamke kugoma kutumiza ndoto zake ni udhaifu eeeh, Basi karne hii wadhaifu ni wengi sana
 
Back
Top Bottom