Nataka kumshtaki rais na wabunge wa CCM naombeni msaada wa kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kumshtaki rais na wabunge wa CCM naombeni msaada wa kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ringo Edmund, Dec 6, 2011.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Waungwa naombeni msaada wa kisheria ili niwashtaki rais na wabunge wa ccm kwa kushindwa kulinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  Mkumbuke kwa mujibu wa viapo walivyokula ni kwamba waliapa kuilina na kuitetea sasa mamlaka ya kuanzisha mchakato wa katiba mpya wameupata wapi? Wameikanyaga katiba kama walitaka kuibadili katiba walitakiwa kwanza watunge sheria waiingize kwenye katiba ya sasa ili iwaruhusu kuibadili.

  Ni hatari sana kuwa na viongozi wa namna hii ma dk na maprof wanafanya makosa ya wazi namna hii tukiwachekea watakuja kuibadili hata hiyo wanayodai kuileta.

  Naombeni wanasheria mnipe msaada ni kesi ya muundo gani, ni pesa kiasi gani na ni mahakama gani natakiwa kisheria kuifungulia?

  Msinielewe vibaya kuna mambo mengi katika nchi hii yanaendeshwa kienyeji ili kuwa mfano nimeamua kuuza shamba langu ili kuwakumbusha utawala wa sheria ni vitendo na si kwenye vyombo vya habari.

  NB: sihitaji msaada wa kifedha.

  Nawasilisha.
   
 2. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu kwa Sheria zilizopo ni kwamba Rais hashtakiwi kwa jambo lolote alilolifanya kama Rais wa Nchi. Hata hivyo, kwa mambo yake binafsi huwezi pia kumshtaki mpaka atakapomaliza kipindi chake cha Uongozi.

  Kwa Wabunge, Sheria ipo wazi kwamba huwezi kumshtaki Mbunge (au Wabunge) kwa jambo lolote alilolifanya ndani ya Bunge. Sheria inaweka wazi kwamba hakuna jambo lolote linaweza kuhojiwa na Mahakama ambalo limefanywa na Bunge. Huo ndio upuuzi wa Sheria zetu!!
   
 3. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mchakato wa katiba hii ndio haswa mahari pakee pa kubadilisha sheria hizi,kwani ni afadhali huyu m.k.w.e.r.e mwenye ubongo mgado kuliko kuja kupata raisi mwenye tahira ya akili maana atauza hata ile nyumba nyeupe pale magogoni na akabaki huru.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  asante kaka nitasubiri katiba mpya ngoja niandae mashtaka niweke kabatini siku itakuja tu.
  na wewe hebu pekuapekua makabrasha yako ya shria ili ikiwezekana niwapeleke hata kule walipotupeleka dowans.
   
 5. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mtafute mtikila anaweza kukusaidia kwa hili huwa ni mzuri kwa kesi dhidi ya serikali
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kaka nina hasira utafikiri nini,
  mpaka nimeamua kuliuza shamba laangu kwani sioni haja ya kuwaachia urithi watoto ambao watakuja kunyanganywa na mafisadi kwa kigezo cha kwamba wameshindwa kuliendeleza.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naomba namba yake kaka.
  niko moto vibaya.
   
Loading...