Nataka kulisaidia Jeshi la Polisi; Muuaji aliyekimbia DSM anaishi hapa

Mnaweza kuona kama mtoa mada mnafki sijui hayamuhusu,mara mbea ngoja niwape kisa kimoja cha kweli nikiwa mkoa fulani alikuja kijana fulani mtaani kwetu alikua ametuzidi kidogo lakini baada ya kukaa kwa muda ndipo tukapata wasaa kidogo wa kumfahamu na tukaja kufahamu kuwa jamaa alipotoka aliwahi kuua mtu kwa kisa cha kipuuzi puuzi tu na kama alikuja kujificha kule na kuroga hivi,basi siku moja vijana wa mtaani wakiwa wnacheza mpira na mwenyewe akiwepo tabia za utotoni goli la kamba ya katani ndo mwamba wa juu so ikawa utata goli au si goli yule bwana akawa analazimisha ni goli na goli kipa anasema si goli basi bwana yule alipotoa panga hatujui ghafla tu akalizamisha kichwani kwa goli kipa paap ,ubongo nje.....nimejaribu kutoa kisa kirefu kidogo kwa maana ifuatayo mtu aliyemwaga damu isiyo na hatia mkono wa damu huwa unamuandama daima hata huyo wasipomuangalia atafanya unyama tena kikubwa tuheshimu uhai.
 
Polisi wanajisifu kua wana intelijensia kubwa waache wao wenyewe wamtafute mtu huyo. Polisi wetu wamezoea kila tukio hadi wapewe feeds toka kwa raia wema. Ila likija swala la siasa ndio kwanza wanapima hadi hisia za wananchi.
Anachokifanya huyu bwana ni sehema ya intelijensia ya Polisi. Huyu bwana inaonekana kama ni mganga wa kienyeji. Na asikwambie mtu, hao jamaa ni sehemu muhimu sana ya intelijensia ya Polisi.
 
Natumai mko poa wakuu,

Huwa nachukia sana wahalifu wanaofanya matukio na kukimbia mkono wa sheria, zaidi namchukia sana yule anayemficha muhalifu asiweze kukutana na adhabu anayoistahili kuipata baada ya kufanya uhalifu wake.

Huyu jamaa anaitwa Jumaa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga lakini kuna kipindi alihama na kuwa anaishi Dsm,ni mtumiaji na muuzaji unga mzuri sana AU TEJA. Wakati yupo Dsm alimuua mtu kwa kumchoma kisu haya maelezo alinieleza yeye mwenyewe na mama yake mzazi walipokuja ofisini kwetu kwa ajili ya kuua kesi hiyo eti isifuatiliwe tukawaambia hatuna uwezo huo. Ni kati ya Posta au Mburahat, sikumbuki vizuri lakini ni kama kwenye ugomvi wa bar ama maskani zao na ndipo alitoa kisu na kumshindilia mwenzake.

Sasa baada ya kuwa huko DSM anatafutwa akakimbilia Tanga nyumbani kwa mama yake. Yupo anaishi huku kwa amani kabisa ingawa ameshatoa uhai wa binadamu na mwenyewe anajitapa kwamba yeye hawezi kukamatwa na akikamatwa ataachiwa. Sasa hivi ana kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya na kesi yake itasomwa hivi karibu mahakama ya Tanga Mjini.

Naendelea kutafuta picha yake,nitaiweka siku si nyingi.

HUYU JAMAA AMEUA KWELI KABISA KWA MUJIBU WA MAELEZO YAO

Naanzaje kuisaidia Polisi katika ili wamrudishe mtuhumiwa wa mauaji akahukumiwe, kuliko kufichwa fichwa huku mtaani na mama yake huku akipewa hela za kuvuta unga na kusumbua raia?

Ama kama napata mawasiliano na wanausalama wa huko DSM wanaohusika na kusimamia kesi za mauaji ningewapa maelezo vizuri waje wamnyakue.
Nenda moja kwa moja kwa RPC-TANGA muone yeye mwenyewe personal mwelezee kwa undani, naimani atachukua hatua stahiki Kisha mtuhumiwa atakamatwa na kupelekwa polisi DSM ili kujibu kesi yake!

NB. Wakati unaondoka Kama tatizo ni nauli mwambie kabisa afande nauli sina I hope utapewa.

Endelea kuwa mzalendo kwa nchi yako
 
- Jiandae kuwa kwenye kaselo kadogo huku unaisaidia polisi. Hapa utaacha kazi zako nyingi kuhangaika na kesi ya mpuuzi mmoja.
Unaweza jikuta na wewe unapata kesi. Baada ya kugundua kwann hukureport kwenye kituo chochote?
- Siku ndugu zake wakijua kuwa wewe umemchomea ndugu yao, jiandae kwa lolote.
Sio kumchoma ni uzalendo
 
- Jiandae kuwa kwenye kaselo kadogo huku unaisaidia polisi. Hapa utaacha kazi zako nyingi kuhangaika na kesi ya mpuuzi mmoja.
Unaweza jikuta na wewe unapata kesi. Baada ya kugundua kwann hukureport kwenye kituo chochote?
- Siku ndugu zake wakijua kuwa wewe umemchomea ndugu yao, jiandae kwa lolote.
Yote hayo yanaweza kutokea lakini je vipi wakifanikiwa kumkamata sababu tu mtoa mada alitoa taarifa sahihi?
 
Hivi humu hakuna hata askari mmoja wa geshi la polisi akachukua hizi information kwa kwenda inbox kwa jamaa akapewa jina na mtaa anaoishi mtuhumiwa na jeshi likaanza uchunguzi kimya kimya maana tayari kuna taarifa za kunyooka zimepatikana kwa jamaa mwingine humuhumu..
 
Back
Top Bottom