Nataka kujua Nguvu za mila hasa kwa wachaga

zhang laoshi

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
401
469
habari wakuu
kama title inavyosema nataka nijuzwe zaidi ya nguvu ya mila hasa kwa wachaga, mfano huwa wanasema ukifanyiwa wakati ukiwa mdogo au ukiwa unashiriki na baadae kuacha huwa unapata wakati mgumu sn kimaisha na hutoweza kutoboa au ukitaka ivunjwe ni lazima ukoo mzima uridhie na kazi yake si ya kitoto

leo nilikutana na mzee mmoja wa kichaga akaniambia tatizo la vijana wengi wa leo wametupa mila zao hawataki kufanya wanaona zimepitwa na wakati kitu ambacho si kweli wale wazee walikuwa wanafanya kazi kubwa kwa njia wanazoamini wao na walifanikiwa lakini weng wetu baada ya kuja mjini au kuzaliwa huku huwa tunaziacha na huwa zinatutesa sn kwan hakuna unachofanya ukafanikiwa mfano ajira au kibiashara

je ni kweli wapo walioenda kuwaangukia wazee kijijini na wakarudi town na kutoboa?

then wapo ambao walishahisi kupitia wakat mgumu kifamilia, ajira na biashara na tatizo likawa ni mila?
 
Mimi mchaga, hizo mila zilishapotea
Labda miaka ya 2000 kurudi nyuma ndio kulikuwa na mila na watu wakawa wanajali.. Ila siku hizi makanisa hasa ya kilokole yameshika kasi sana na wanawaambia watu matatizo waliyonayo yanatokana sijui na vifungo walivyowekewa ama kurithi kutoka kwa mababu zao na mila zinawafunga kwenye hivyo vifungo, hivyo wengi wanaogopa na kuacha

Kingine elimu, utandawazi na kuhamia mjini vimechangia sana kupungua kwa hayo mambo,

Mi nashangaa siku moja nilisoma habari eti smajani ya Masale yanachangia Wachaga kuwasamehe waliofanya uhalifu kama wa kubaka watoto wao, sababu ya kuwa lina nguvu sana mkosaji akikuomba nalo msamaha lazima umsamehe, ila kiuhalisia hayo mambo ni ya zamani sana na vijana wengi wa siku hizi hawajui hata kazi ya hilo jani
 
Mila ziko nyingi nz zina matokeo tofauti. Mfano, ukienda kuoa, na kwenye familia hiyo kuna mzaliwa wa kwanza mwanamke alifariki bila kuolewa basi, muoaji atatakiwa kumuoa mrehemu (wanajua wanacho fanya) kisha ndio uoe huyo uliyemchagua.Na hata watoto mtakao zaawanachukuliwa ni wa yule marehemu. Pale nao watakapo kuwa tayari kuingia kwenye maisha ya ndoa,yahitaji kipaji cha uvumilivu kuishi nao. Wengi ni Alfa female or Alfa male.
 
Back
Top Bottom