Nataka kujua, hivi LIBYA walikosa nini?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Enzi za utwala wa hayati Muamar Gaddafi, Libya ilikua ni ulaya ndani ya Afrika, watu walijengewa barabara kila kona ya nchi, waliletwa umeme wa uhakika,walijengewa shule nzuri, walijengewa miundombinu ya Maji,walijengewa mahospitali ya kisasa, uchumi ulikua maradufu wakajitosheleza na wakaanza hata kutoa misaada kwa nchi maskini Afrika, Vijana waliotaka kuoana waliwezeshwa na serikali yao, walipewa mitaji ya biashara.


Libya ya leo inechafuka,damu zinatapakaa kila Kona ya nchi, familia nyingi zinekua wakimbizi kwenye nchi za watu! Hakukaliki Libya, baba na mwana wanapoteana mchana kweupe.


Maswali yangu kwako Mdau,

1.Ni kweli Libya hawakupenda maisha waliyokua nayo?

2.Walikosa nini cha Muhimu hasa?

3.Unafikiri binadamu anahitaji nini ili aridhike nafsini mwake?

4.Hivi Mtu kama Gaddafi aliamini kua ipo siku atakufa kifo kibaya kama kile pamoja na kuwajengea walibya bustani ya Eden?

5.Unafikiri kuwaletea watu maendeleo peke yake ndio haki yao ya msingi itakayowafanya waishi kwa amani,unafikiri hakuna haki nyingine zaidi ya hiyo.
 
Hizi kauli kwa viongozi mataahira yaliyoko huku kusini mwa jangwa la sahara hawawezi zielewa!!
 
Hizi kauli kwa viongozi mataahira yaliyoko huku kusini mwa jangwa la sahara hawawezi zielewa!!
Hawa ni watu wenye akili timamu, nadhani saa zingine Mungu hua anawapiga upofu ili kuamsha hisia za watu mataifa yao yazaliwe upya.
 
Uchu wa madaraka na kurubuniwa na nchi za magharibi ambao kwa sasa hivi wamewakimbia hata hawataki kuwasikia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom