Nataka kujua bei za mihogo, shamba lipo kibaha, ekari tatu

agritterk

New Member
Jun 10, 2017
4
4
Kwa wale wazoefu, nataka kujua bei ya mihogo niuzaje shambani, shamba lipo kibaha, nililima mwezi wa 3 mwaka jana, ile mbegu ya kukaa muda mrefu shambani (ndope). Ni mikubwa na mitamu. Lakini sijajua bei ya soko ikoje sasa hivi, naomba ushauri wenu.

Shukrani!
 
Mkuu agritterk kama hujapata bei basi jaribu kwenda kwenye masoko makubwa mf . Kwa Dar nenda Soko la Tandale, Stereo au Buguruni kisha ulizia bei kwa wale wanaouza kisha utajua bei sahihi ya kuweza uza mazao yako....pia wakati unaulizia bei hapo hapo unatafuta wanunuzi, wahi kwa siku hizi ambazo Mfungo wa Ramadhani ukiwa bado haujaisha
 
Asante kwa ushauri, ila nilijaribu kufanya hivyo kwa hapa dar, wameniambia hawanunui mihogo ya kibaha mpaka mwezi wa 8 na 9 wakati mihogo mengine imehadimika. Lakini nimeshapata mtu kutoka mlandizi, namuuzia TShs 600/- kwa kilo, nafikiri sio mbaya sana!
Kwahiyo kwa sasa wananunua mihogo ya wapi ?
 
Asante kwa ushauri, ila nilijaribu kufanya hivyo kwa hapa dar, wameniambia hawanunui mihogo ya kibaha mpaka mwezi wa 8 na 9 wakati mihogo mengine imehadimika. Lakini nimeshapata mtu kutoka mlandizi, namuuzia TShs 600/- kwa kilo, nafikiri sio mbaya sana!
Mkuu embu tupe ufafanuzi kuhusu mihogo ya wapi wananunua muda huu na aina gani ya muhogo wanahitaji sokoni kwa sasa?
 
Mimi nina shamba mwalusembe huwa nauza kwa heka moja 2m kama mihogo ni michache sokoni lakini kama itakuwa mingi heka moja za kwa 1.5-1.8m, huku wananunua kwa heka ni siyo kilo
Unauzia shamba mkuu? Ni mihogo aina gani wanapendelea sana sana?
 
Mimi nina shamba mwalusembe huwa nauza kwa heka moja 2m kama mihogo ni michache sokoni lakini kama itakuwa mingi heka moja za kwa 1.5-1.8m, huku wananunua kwa heka ni siyo kilo
Basi huko biashara inaelekea ni nzuri sana! Kwa mahesabu ya kibaha hekari ni TShs. 750,000/-, kwa mbegu ya ndope!
 
Back
Top Bottom