Nataka kujitolea kampeni ya chadema 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kujitolea kampeni ya chadema 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sir R, Jul 25, 2010.

 1. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ninapenda kujitolea kuifanyia CHADEMA kampeni bure mwaka huu. Ni kutokana na uhaba wa fedha CHADEMA na kwa kuzingatia kuwa mabadiliko yanahitajika Tz. Miaka zaidi 40 ya umaskini ni aibu kubwa kwa nchi yenye rasilimali nyingi.

  Ninaomba CHADEMA inisaidie kufahamu
  i. kujitolea kunaruhusiwa kuifanyia CHADEMA kampeni
  ii. Kuna utaratibu wowote uliowekwa na chama wa watu kujitolea kufanya kampeni.

  Binafsi nitafurahi kama CHADEMA wanaruhusu kujitolea na kama utaratibu upo, ni vema tukajulishwa mapema ili tushiriki katika shughuli muhimu. Ningependa kuwashawishi wote wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya utawala ndani ya nchi hii ili kuleta maendeleo, washiriki ipasavyo katika kampeni ya kujitolea kwa ajili ya CHADEMA.

  Tusisubiri kulipwa,, tutoe kile kidogo tulicho nacho kwa ajili ya wagombea kupitia CHADEMA. Si lazima fedha inaweza kuwa mawazo ya kujenga kama vile kuhamasisha wananchi kkushiriki kuchagua CHADEMA bila uwoga. Kama una fedha unaweza kutoa. Mimi ni raia wa kawaida mwenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli.

  Ninawahamasisha form six leavers wote na wanachuo wote kwa pamoja kujitolea kwa ajili ya CHADEMA; Tuwe sehemu ya mabadiliko, tusisubiri mabadiliko yatokee. wewe uyasababishe. Ni muda wetu kuleta mabadiliko ya kweli si wakati mwingine.
   
 2. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wakati wa kupigania Uhuru Mwl. J. Nyerere alichangiwa na watu maskini... mimi kama mmoja wa Watanzania walio nje ya nchi, nataka kuichangia uraisi wa Dr. Slaa: sio kwa hali tu bali kwa mali (kifedha) Je vipi naweza kuchangia? Chadema itengeneze mpango wa kuchangia mapema... Tusimwachie Sobodo tu!
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .............true....true.......true............sijui zile kanuni mpya za kuchangia kampeni zinasemaji ktk hilo..........
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bila shaka GS (Gender sensitive) atakuja kutoa jibu.

  Nafurahi kwa watu wanaojitoa sasa kwa hali na mali kwa ajili ya Chadema
   
 5. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajumbe nina mambo mawili tu

  1. Chadema kwenda 15710 inafanya kazi; mnapata hizi maana naona haipewi kipaumbele hili mhimu sana watu kujua na kuhakikishiwa na makao makuu mjue kufuatilia hizi fedha ; japo kidogo si haba;
  2. Pia wanazuoni wakae watoe veema utaratibu wa kujitolea wakati wa kampeni kama ilivyo m arekani na definitions zake zijulikane; kazi iliyo mbele sio ya kulala hata kidogo
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kuna thread naona iliwekwa namba ya kutuma sms ili kuchangia ,natumai wataweka na hapa.
  Ila hiyo haitoshi pekee ,kuna maswali mengi toka kwa mwazilishi wa mada yanaitaji kujibiwa kama lile la jinsi ya kujitolea.
   
 7. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Yu wapi huyo G S bado tunamngoja!
   
 8. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Tafadhali Tuunge Mkono

  CHADEMA kinaamini kwamba ili uongozi wa nchi uweze kuzingatia maslahi ya Watanzania kwa umakini na kwa dhati hatuna budi tuwe na siasa za ushindani thabiti. Yaani Bunge lenye wapinzani wa kutosha ambao ni wazalendo makini na jasiri, wenye uwezo wa kuikosoa Serikali bila woga pale inapozembea. Hali kadhalika mfumo wa serikali za wilaya, vijiji na mitaa ni laizma uwe na mazingira yanayowezesha kukosoana na kusahihishana kwa uhuru na uwazi bila woga ili kuondoa au kuzuia ubadhirifu wa mali ya umma, uzembe, uonevu, rushwa na papo hapo kuhakikisha tunakuwa na maendeleo ya kudumu na ya kuridhisha.

  CHADEMA inadhamiria kuhamasisha na kutoa elimu ya uraia mwema na elimu ya siasa kwa Tanzania nzima katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji wa 2009. Tunatarajia wazalendo wenye uchungu na nchi yao na wenye dhamira ya dhati ya kutatua matatizo sugu ya nchi hii, kuungana nasi katika juhudi hii. Uongozi wa CHADEMA unataka kujadili na wananchi, wakichangia mawazo yao kwa uhuru na uwazi. Kila kijiji, kitongoji au kata pawepo na sera na mikakati iliyobuniwa na wakazi wake inayolenga kuondoa kero zinazowakabili jamii husika.


  Ili kuwezesha uongozi wa CHADEMA katika ngazi zote - kuanzia tawi la kitongoji hadi taifa - uweze kutekeleza majukumu haya ya uenezi na uhamasishaji lazima pawepo nyenzo na vifaa. Kwa hiyo tunakaribisha Mtanzania yeyote mwenye kupenda nchi yake, na anayeamini katika ujumbe huu atoe mchango kadri ya uwezo wake. Naam, kimefika kipindi cha Watanzania wema kutusaidia.


  Wasamaria wema wametuchangia fedha, wengine wametoa sehemu za nyumba zao kama ofisi ya matawi ya chama. Wengine wamewakarimu viongozi au kuwapa malazi huko vijijini. Wengine wametukodishia kwa gharama nafuu magari yao au kutupa petroli bure tuweze kutembelea wilaya zao. Wengine wametupatia baiskeli tuweze kuwafikia sehemu ambazo magari hayafiki. Wako waliotuazima vipaza sauti tuweze kuhutubia mikutano yetu ya hadhara. Vilevile wengine wamehudhuria na kushangilia na kuwapa moyo wale waliowaeleza misimamo ya CHADEMA. Wote hao wamechangia na tunaomba waendelee mpaka hapo lengo letu litakapofikiwa. Tunawasifu, tunawashukuru sana na mungu awazidishie.


  Kama hutaweza kufika kwenye ofisi za CHADEMA basi tuma fedha katika akaunti zetu zifuatazo:

  Akaunti ya "CHADEMA"

  NBC Corporate Branch (Local currency) 011103010075

  NBC Samora Branch (Foreign currency) 012105019310


  au


  Akaunti ya "Freeman A. Mbowe and W.P. Slaa"


  NBC Corporate Branch (Local currency) 011101016268

  NBC Corporate Branch (Foreign currency) 011105010534
  Jambo muhimiu na la lazima ni kwamba ili kufanikisha lengo letu la kuimarisha utawala bora na maendeleo endelevu ya kuridhisha, hatuna budi kudumisha misaada hii. MwanaCHADEMA hakikisha kadi yako unailipia ada ya mwaka, na kama una uwezo changia tawi lako ili CHADEMA kiweze kununua makaratasi na mabango ya uenezi. Wewe mzalendo mwenye uwezo zaidi tupe mchango wa kweli utakaodhihirisha mapenzi yako kwa chama. Kila fedha itakayopokelewa CHADEMA itaambatana na stakabadhi yenye jina la mtoaji au jina la 'kificho' kama mtoaji atapendelea. Tunaelewa na tunaheshimu sababu zao wale wote wasiotaka majina yao yahusishwe na CHADEMA hadharani.

  Hivyo ndivyo kuchangia kwa hali na mali. Tunaamini na kudhihirisha kwamba hii ndiyo nguvu ya Umma.


  Changia CHADEMA! Changia Maendeleo endelevu!


  Asanteni sana


  Dk. Willibrod P. Slaa

  Katibu Mkuu
   
 9. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tutashukuru sana kwa kukiunga Chama Mkono. Nchi itajengwa na wananchi kila mchango unathamani kubwa.

  Akaunti ya "CHADEMA"

  NBC Corporate Branch (Local currency) 011103010075
  NBC Samora Branch (Foreign currency) 012105019310


  au

  Akaunti ya "Freeman A. Mbowe and W.P. Slaa"

  NBC Corporate Branch (Local currency) 011101016268
  NBC Corporate Branch (Foreign currency) 011105010534
   
 10. M

  Mutu JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kinepi-nepi thanks,
  tutachangia kadiri tuwezovyo kwa ambao tutaweza changia
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jul 27, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  International interbank wiring kwenye benki yangu huwa ni expensive sana hasa kama inahusu kutuma hela chini ya dola 1000, na siwezi kuchanga kiasi hicho. Kwa hiyo naomba utaratibu mwingine wa kuchanga ambao hautakuwa expensive kwangu, kwa mfano kutumia moneygram au westernunion. Nitaichangia CHADEMA kiasi kidogo nitakachoweza ingawa kinaweza kujaza mafuta ya helikopta kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Nime-bookmark thread hii na nitaendelea kuisoma kila siku hadi nipate jibu la swali langu hapo juu.
   
 12. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nadhani kichuguu umewakilisha vema our concern. Chadema ifanye urahisi kwa wachangiaji... ni nia yetu kuchangia... mie pia nangoja jibu...ila natoa wito kwa kila mtaanzania mwenye nia njema na nchi yetu awe tayari kutoa hata kama ni kidgo tu.... Obama aliwezeshwa na michango kidogo.
  CHANGIA TUMUWEZESHE DR. W. SLAA KUTUKOMBOA
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tunaomba tupatiwe IBAN na SWIFT codes za hizo accounts ili na sisi tuliopo nje ya nchi tuchangie.

  MUNGU BARIKI HARAKATI ZA KUMKOMBOA MTANZANIA!
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asanteni kwa walioko nje, naamini wahusika watafanya linalo hitajika ili michango yenu ifike. Binafsi nilikuw na wazo kwa tulioko bongo, kwamba tulipewa jinsi ya kuchangia kwa msg sh 300, hivi hamna namna nyingine ya kurahisha zaidi kwa kuweka mfano anaye taka changia elfu, tano atumie namba fulani, elfu kumi namba fulani, kuliko mtu kutuma msg nyiiiiiingi ili afikishe hiyo elfu 20 kwa mfano? kama hiyo IT ipo, tafadhali itasaidia sana kwa bongo, kuliko mtu kujipanga foleni kwenda NBC kutuma efu 50 ni rahisi kutuma msg 5 za elfu kumi kumi ukiwa nyumbani mwako.

  Wana IT please help out!
  Hii nchi ni yetu wote, lazima tushirikiane wote kuikomboa mikononi mwa mafisadi!
   
Loading...