Nataka kujilipua na CARINA TI nisaidieni bei za yard Bongo

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
759
1,004
Wakuu,

Baada ya kuhanya sana huku na kule na kuona mipango ya kuweza kujenga mjini kabla ya kununua usafiri inazidi kwenda kombo kwa upande wangu,

Nataka nijilipue tu ninunue gari ya watu wa uwezo wa chini tu,
Ambapo nitaisajili kuwa ya biashara ili niifanye Uber ambayo nitaendesha mwenyewe pindi nimalizapo mizunguko yangu binafsi (lengo ni kupata japo hela ya wese na services ndogondogo, badala ya kuipark tu).

Choice yangu ni CARINA Ti angalau ya mwaka 2001, yenye CC 1490.

Kwa nini CARINA Ti?
Kwa sababu nina lengo la kukaa nalo kwa zaidi ya minne (4) uzima ukiwepo na ikiwa halitapata hitilafu kubwa kwani inaonekana aina hii ni gari ngumu-

Na kwa kuwa uwezo na mpango wa kubadilisha ndani ya muda mfupi haupo,
Hii itanifaa kwani nitajikita sana kwenye kuzingatia zile services za msingi kwa wakati.

Sasa kwa kuwa sina imani sana kuhusu kununua ya mkononi kwa mtu (iliyotumika Bongo),
Naomba kwa wenye kujua mnijuze bei ya hiyo gari tajwa katika yard za Bongo na/au ikiwezekana gharama ya kuagiza (used from Japan) mpaka kuiweka barabarani.

(Kuhusu kupitwa na wakati/kutokuwa la kisasa- hilo nalifahamu, na halinipi shida)

Natanguliza shukrani.
 
Kuna uzi niliusoma hapa JF kwamba wanaonunua CARINA ni mabahili wa kiwango kilichotukuka.

Mimi ngoja nizichange jet itanifaa sana kwa misele ya hapa na pale.
 
Chukua TI mkuu ni gari ambayo ngumu na haishuki bei kama IST mkuu jiandae na milioni 11.5 hadi 12 unapata kisu kabisa ndani kinanukia harufu ile ya japan. Usisahau kwenda kwa dick sound magomeni kufunga mziki mkuu the rest enjoy life and welcome to the world. Alafu wale mademu wote waliokua wanakuzingua saizi utawagonja cha muhimu tembea na kondom kwenye gari mkuu.
 
Huyu dogo Dick Sound namwelewa sana!
 
Carina mziki wa nn?
 
Back
Top Bottom