Habari zenu wadau..
Napenda kilimo kwa kweli..huwa nikipita sehemu nikaiona ardhi nzuri na kando kando pana kijito cha maji..moyo wangu huwa unapepea.
Ni kwa muda nilikuwa nawaza ni kwa namna gani naweza kujikita katika kilimo hasa katika kigezo cha mtaji. Mtaji ulikuwa changamoto, ila namshukuru Mungu nimepata raia mmoja rafiki yangu amekubali kuniwezesha kiasi fulani.. actually atanipiga tafu hadi hapo nitakaposimama mwenyewe.
Nipo Dar.. ila naona kuna fursa shambani.. nimekuwa na mawazo ya kufanya kilimo(cha umwagiliaji) maeneo nje ya jiji ili baadae soko liwe hapa jijini na ikiwezekana na maeneo mengine. Nina ndoto za kuja kuwa mkulima mkubwa hapo baadae ambaye si tu nitaishia kuuza mazao moja kwa moja toka shambani bali kufanya "processing" ili kuongeza thamani..in short nina maono fulani hivi ya kufanya kilimo cha kisasa na usindikaji wa mazao hapo baadae.
Kwa sasa naomba ushauri wenu.. nianze na zao lipi ambalo soko lake linapatikana kiurahisi ukizingatia pesa nitakayopata ni Milioni 5.
maswali ninayojiuliza ni;
1. zao gani nianze kulima kwa kipindi hiki( miezi hii)?
2. Je, gharama zake ni kiasi gani(Kuanzia hatua ya kwanza hadi kuja kuuza) ?
3. Nikiuza nitapata faida kiasi gani?
4. Ni maeneo gani yanafaa kwa hilo zao?
5. etc etc
Naamini wapo ambao wanafanya kilimo nami si wa kwanza katika hili.. ninahitaji ushauri ambao si tu wa hewani-nikipata mtu ambaye ame-anafanya kilimo nitashukuru zaidi..Nimekuwa nikisikia habari nyingi kuhusu kulima VITUNGUU, MATIKITI MAJI, KAROTI,MATANGO na mazao mengine mengi
Nishaurini jamani, nimechoka kukaa sehemu na kulipwa vijisenti kidogo ambavyo havikidhi mahitaji.. najiona kama naji-underutilize mwenyewe wakati ningeweza kufanya vitu vikubwa zaidi ya hapa..
Karibuni..
Natanguliza shukrani..